Kuabudu mizimu na kulamba miguu ya wazungu ndio unakuita kula bata!
Kama huko ndiko kula bata, mi njiwa wananitosha!
Hao bata kuleni wewe na
Nyani Ngabu pamoja na his brother from another mother mkataa nasaba
Kiranga
Mtaka nyingi nasaba, hupata mwingi msiba
Muenda nyingi lakaba, hupata nyingi ghiliba
Muoga nyingi janaba, hupata kwingi kuvimba
Kuiza wengi madada, usambe hivi ujinga
Safiri ndugu safiri, upate na kutalii
Safiri japo kafiri, sibaki kuwa chalii
Safiri sawa tahiri, uondoe ujahili
Safiri upate dili, ondoa zako bahili
Utukutu wa mawazo, na kauli za utovu
Kujitia hamnazo, na shabikia uovu
Ama ni hali pumbazo, chafuzi kama utomvu
Nakuwekea mkazo, utosi acha uchovu
Wahenga waliokwenda, umoja walitambua
Binadamu anapenda, mafao yanochanua
Vipi watuweka kenda, kumi tusije chukua?
Wovu kutoa udenda, kwa kukosako kujua?
Karaha kwa waungwana, sio jambo la johari
Balaa la kutukana, hutunzi kwenye bohari
Bora hata kujikana, baharia wa bahari
Mie kwangu kote sana, katika hii sayari
Mzungu anajifia, dunia yaendelea
Wewe unamuhofia, kama kwelea kwelea
Gurudumu kikwachia, utaweza kuelea?
Acha dhana za ghasia, weka zaidi welewa
Kaditama nishafika, malenga wataelewa
Unyonge wa muafrika, kutaka sana chelewa
Nautoa kwa hakika, kwa kujitia behewa
Na hivi hii dakika, naua vyako melea