Mohamed Said , nifafanue 'unafiki' nilioandika hapo juu. Nafahamu wazi kuwa huwezi kuwa rafiki wa jamii kama ukisema ukweli. Kwangu mimi kuwa public enemy ni sehemu ya maisha yangu. Nina amini kile kilichosawa kwa mtazamo na maoni yangu. Mimi kama wewe ninatumia nafasi yangu katika jamii kama ilivyo kwa mwingine pia.
Waambie vijana wako kuwa wewe kuwa moderator haina maana kuingia na kufungia watu . Nimesema kwa uwazi kwa umri wako na nafasi yako kwa jamiiiwe ndogo au kubwa, kwa mila zetu unalojukumu la kijamii la kusimama na kumkanya kijana au awaye. Hiyo ndiyo privilege ya uzee wenye busara na hekima.
Nimeitumia nafasi yangu kusema kuwa unalo jukumu la kuwakumbusha watu wasitoke nje ya theme yako. Lengo lako lilikuwa tribute kwa nduguyo na rafiki yako. Bila kujali maono na mtazamo wa kila mmoja, unabaki kuwa na haki kwa tribute ya Ilunga.
Ili tribute hiyo uliyoiandika kwa mtazamo na uelewa wako ilete maana, inajuzu vijana waitendei haki. Kuitendea haki ni kuwa na mjadala endelevu ukiangalia maisha yake,success ambazo umezionyesha, failure ambazo hukuzisema na legacy kwa vijana ambao umewataja kama sehemu ya pigo la kifo cha Ilunga.
Nasimama kusema kuwa kama legacy ya Ilunga kwa vijana ni hii tunayosoma hapa basi sikutambua hilo.
Tribute inapokuwa matusi, kashfa na kejeli ina 'adulterate' maana na kusudio lako kama nitakuwa sahihi.
MS, waambie vijana kuwa mtu akikuita mshenzi na ukamrudishia lile neno baya la mama, basi lile la mama linaeleza ushenzi wa aliyetukanawa na si aliyetukana.
Hivi adabu na heshma za mnakasha ndizo hizi tunazozisoma hapa? Na hakika umeendelea kuvutika na kutoka nje ya mada ukiogelea katika dimbwi la majitaka pengine kwa kuhisi upo mbali na vijana katika dimbwi hilo basi utatakata.
MS ukiwa katika dimbwi hakuna usafi.
Kwavile mimi ninaogopa kuoga na watoto mtoni nikijua sitataka kwa michezo yao ya kuchafua mto, ninaishia hapa nikukunasihi tena, angali nafasi yako katika jamii na ujiridhishe kuwa haya yanayofanyika ukiwa kimya tena mengine ukiyaunga mkono yanalingana na wasifu na wajihi wako.
Nimetumia haki na nafasi yangu katika jamii kukushauri, lau kana ushauri huu ni mbaya, hewala na samahani.
Huko kwa vijana sipo na sitakwenda. Nilisha feli mtihani wa kuchagua na kuandika insha za matusi, kwa umri huu sitarajia kufanya supplimentary.