TAYADI nabashiri namna ulivyo pindua maumbile alokuumba kwa makusidi kwayo Mwenyezi Mungu.
Weye watumia makalio kufikiri na kichwa kwa kuketi, sasa ndo maana sipati ghadhabu juu ya kukutanabahisha kunako majambo....!
Nafahamu wachelewa sana kufahamu namna inavyotakikanika kufahamika.
Huu ni mfululizo wa visa vipatavyo vinne vya kikatili ambavyo vimefanyika Zanzibar, vikiwalenga watu maalumu katika kipindi cha miezi 10 iliyopita.
Desemba mwaka jana, watu ambao bado hawajafahamika wamlipiga risasi Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar na kumjeruhi vibaya.
Februari mwaka huu aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani, Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki katika eneo la Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Hawa wote ni wanyama?Agosti mwaka huu wasichana wawili, raia wa Uingereza waliokuwa walimu wa kujitolea, walimwagiwa tindikali na kujeruhiwa kifuani, shingo na uso.