Mkuu
Glenn , naheshimu maoni yako hata kama sikubaliani na wewe, huu mtazamo wako kuwa mimi ni mwandishi na mwanasheria nisiye jielewa, naomba pia niheshimu msimamo wako.
Kwanza ni kweli sisi media ni kama refa, ila kwenye uzalendo kwa nchi yako, sometimes refa unaingia uwanjani na kuwa kocha mchezaji, kuisaidia timu yako kushinda, unaingia!. Hii kwenye media ndio kitu kinachoitwa objectivity.
Sio kila hoja ninatia pua, ukiona tuu nimetia pua kwenye hoja yoyote, ujue hiyo hoja ina maslahi kwa taifa.
Mimi sina makala zozote za akili, nina makala za Kwa Maslahi ya Taifa, zinaendelea magazetini.
Mimi ni mwananchi wa kawaida kabisa kama wewe!.
P
Pascal Mayalla
Kwanza nikushukuru kwa kuona nisivyopendezwa na michango yako jukwaani siku hizi.
Nisiwe mnafiki hili ndilo nilililolitaka ulione.
Haya mawe yote ni mbinu zangu ili ushtuke na uje tuongee ana kwa ana.
Tena nilitamani ukasirike uje pm.
My brother, to be honest....huu sio uzalendo.
Umepofushwa na rushwa, tamaa ya vyeo na ukata.
Ninakusoma hatua kwa hatua.
Najua ulipoangukia...hali tete ilikushinda na katika hili ninaongea kwa ujasiri na ( moyoni mwako utakiri japo jukwaani utakana)
JE PASCHAL NI KILAZA?
Hapana, una akili njema, mchambuzi mzuri, una upeo mkubwa sana, hii imetokana na uzoefu ulio nao wa kufanya kazi na watu wa kada mbalimbali.
TATIZO NINI?
Ulipoamua kuingia siasani ndipo ilikupasa ujifanye chizi ufanane nao ili upate unachokitaka.
NJAA NA UKWELI HUKAA PAMOJA?
Ni nadra mtu mwenye njaa kuwa na msimamo thabiti, ni mara chache sana mwenye njaa asigeuke msaliti ili aishi.
Kumbuka njaa sio lazima ya kukosa chakula au pesa bali hata shauku ya kuwa mtu flani...cheo nayo ni njaa.
NINI ULICHO NACHO SASA?
Umebaki kama Sauli yule wa kwenye biblia baada ya kuachwa na Mungu.
Hskuwa na nguvu tena na alikufa kifo cha aibu kutoka kuwa mfalme wa heshima.
Paschal: unaweza kutuchukulia poa sisi tuliokuamini lkn hakika sisi tulikuwa miungu kwako, tulipokuunga mkono kwenye mada zako uliendelea kusitawi.
Na sasa tunakuacha kidogo kidogo jinsi unavyoendelea kutuupuza...kama Saul ambavyo aliachwa hatua kwa hatua na Mungu.
Bro. Achana na huu ujinga.
Nadiriki kuuita ujinga kwasababu hata wewe ukweli unaujua lakini umekaza shingo.
Zaidi ya yote uchaguzi ni wako.
Chagua uchawa, njaa na usaliti upotee au
Uchague kuwa mkweli uishi hata ukiwa umekufa.
Nitakukosa na jiwe au mshale lakini kwa neno la kweli nitakupata.
Wazee
T14 Armata
Lusungo Mmawia
Kama ninamuonea niambieni niombe radhi
Glenn