Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum atenguliwa

Na kashfa ya kuwala wanawake waliokuwa wanaenda kuomba talaka
Muhamasishaji wa Amani na Uzalendo aliyasafiri kwenye nchi zaidi ya 20 duniani, Mwenyekiti na Mjumbe wa kamati zaidi ya 10 za kidini na Kitaifa tena mwenye tuzo zaidi ya 15. Suala la kutengua uteuzi wa Sheikh wa mkoa wa DSM yani Alhad Mussa Salum limewaacha wengi na maswali.

 
Kumbe mufti naye keishaikwaa Phd!
 
Nakumbuka alivyowahi kumsifia Magufuli kuwa yeye ni zaidi ya Yesu na Mohammad (S.A.W).
 

Kitaifa




Bakwata yamng’oa Sheikh Alhad Dar​

Alhamisi, Februari 02, 2023

By Juma Issihaka

Muktasari:​

  • Baraza la Ulamaa limetemgua uteuzi wa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum na kumteuwa Sheikh Walid Omar kukaimu nafasi hiyo.
Dar es Salaam. Baraza la Ulamaa limetemgua uteuzi wa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum na kumteuwa Sheikh Walid Omar kukaimu nafasi hiyo.

Uamuzi wa kumtengua Sheikh Alhad umekuja ikiwa imepita wiki moja tangu, kiongozi huyo alipotangaza kuivunja ndoa hiyo ya mtaalamu wa tiba mbadala, Juma Mwaka Juma maarufu kwa jina la Dk Mwaka na mkewe Queen Masanja Januari 25 mwaka huu, kufuatia ombi la mwanamke huyo kudai talaka.
Hata hivyo, siku mbili baadaye, yaani Januari 27, Baraza la Ulamaa lilikutana kwa dharura na kubatilisha uamuzi huo.
 

Attachments

  • Screenshot_20230203-073100_Facebook.jpg
    158.2 KB · Views: 3
Sawa, katolewa ila asiletwe sheikh mhafidhina na mfia dini ya kigeni wakati ni muafrika mweusi tii. Anatakiwa sheikh mwenye msimamo wa wastani juu ya dini hiyo anayoiamini
Ni vyema shura ya maimamu ishirikishwe kwenye kumchagua sheikh mpya wa kuziba hiyo nafasi.

Mohamed Said ana maoni gani kuhusu hili?....
 
Asikubali, akapinge kutumbuliwa mahakamani.

CCM tusikubali kumuacha peke yake Sheikh wetu, ni sisi ndio tuliompa kiburi cha mpaka kufikia kushindana na baraza la ulamaa ambalo ni superior kwake na hata mufti analiheshimu.
 
Atoke tu kadumu hadi vitoto vinakuwa na watoto akwende.
 
Mufti kafanya maamuzi sahihi.
kiongozi wa dini ni kioo cha maadili na nidhamu ya kiwango cha juu kwa waamini wake na hata jamii kwa ujumla.

Pongezi kwa shek wa mkoa mpya aliyeteuliwa.
Hata hivyo bado mheshimiwa Mufti amemvumilia sana sijui huenda alikua anamuonya ndani kwa ndani mjivuni huyu
 
Kwa hiyo Juma anazani itasaidia kughairi kuachwa?

Moyo ukishakataa na kumkinahi mtu ndio basi tena!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…