Sheikh Mkuu Zuberi jenga shule kubwa badala ya misikiti mikubwa

Jua fahamu,chuo chochote cha dini,huwa kinafuata imani ya dini husika,katika ibada,mavazi,itikadi nk.Kwa upande wa kikristo kuna madhehebu mengi sana,lakini upande wa uislamu 99.9 asilimia ni Suni.Katika hao Suni ndio kuna Taasisi tofauti.Wanafunzi wa hizo Taasisi wanaweza kusoma chuo chochote,kilichoasisiwa na Taasisi yoyote bila mgongano.
Lakini katika ukristo,msabato akisoma chuo cha Kikatoliki,upo mgongano,mfano mdogo tu,msabato hafanyi kazi yoyote siku ya jumamosi,je kukitolewa mtihami siku ya jumamosi,katika chuo cha Kikatoliki,atafanya huo mtihani?(Na imewahi kutokea hiyo,katika chuo fulani).
Hata katika ibada,wapo wakristo,wanahesabu baadhi ya vitu vinavyotumika katika madhehebu mengine,ni ibada za sanamu.Kwa hiyo kila dhehebu linakuwa huru zaidi,wanafunzi wake kusoma chuo cha dhehebu lake.
Yapo madhehebu,hayatambui sikukuu za madhehebu mengine,je wakiweka mtihani siku ambazo,ni sikukuu kwa wengine,hapo hapajatokea migongano?
Hayo ni machache tu,kwa kukupa mifano.
 
Waislamu wapo mbele sana kielimu,usijindangaje,ila waislamu wengi,wamejikita kwenye biashara,na kufanyakazi kwenye kampuni za kibinafsi,na wengi huwa wanavyamia soko la ajira katika nchi za nje ,sana.Waislamu kuwaachia dini nyingine,kushika nafasi,za ajira nyingine,sio kwamba hawakusoma,ila muelekeo wa wengi,wako kwenye biashara,wako sekta binafsi,wako kwenye ajira za nje ya nchi.
 
Wana chuo kinaitwa MUM kilichojengwa kwenye jengo la TANESCO walilopewa na Hayati BW Mkapa.
 
Hebu ACHA UONGO ndani ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan, eti Mwanafunzi wa dhehebu moja la kikristo hawezi kusoma katika chuo cha dhehebu lingine???

Umelitoa wapi hili?
 
Hawa wanaitwa Wana wa Kulalamika, mahala pa kutumia akili wanatumia Jazba, Malalamiko na Milipuko

Ndio Uislam wao huo, wana wa Mwamedi
 
Mimi nimeongelea kuhusu uwiano wa dini vyuoni na kazini, sio vibaya na wewe ukaongelea elimu kwenye makabila, mikoa na kanda ukipenda. Mimi kilichonishitua ni vikao na mikutano kufunguliwa kwa sala bila kujali dini nyingine kwasababu tu watu wa dini nyingine ni wachache au hawapo kabisa kwenye mkutano ule.
 
Kujenga msikiti na madrasa zitazosomesha Qur'aan na Sunnah ni bora mara elfu kuliko kujenga shule.
Ndo maana waislamu wanashindwa hata kutoa zaka na sakata, hawana kipato hawana ajira ni vibarua tu wanaovaa yebo na mitumba. Kama huamini nenda kwenye msikiti wa ijumaa halafu angalia viatu vyao pale mlangoni, binafsi natamani kulia. Waumini wana ndala na yebo imetoboka kwenye kisigino
 
Lakini Waislamu ndio matajiri wakubwa hapa nchini sijui nao wamependelewa na nani, na pia kwenye makampuni yao asilimia 90 ya wanaoajiriwa ni Waislamu nadhani ungeanzia huko kwanza mkuu.
Taasisi na ofisi za umma ni mali ya dini zote na zinaendeshwa na kodi za watu wa dini zote, kukaliwa na watu wa dini moja sio afya. Achana na hao matajiri binafsi kama Mengi, Mo, Bakhera
 
Poa.
 
Kama Bakwata haitaacha kuwa chombo cha kisiasa waislamu watakuwa wasindikizaji milele kwenye taifa lao. Hali ya waislam inatisha sana, kuna taasisi za umma zinafungua mikutano yao kwa sala kwakuwa wengi ni dini moja tu.
Wamechelewa mnooo hapo dawa ni juhudi binafs kwa familia za kiislam kuendeleza watoto wao kwa Ilm dunia
 
BAKWATA wana shule zaidi ya 60,Kati ya hizo 32 ni vyuo vya dini.30 ni secondary,,wasomi wengi wa kiislamu waliomaliza BAKWATA,wako nje nchi na wanafasi nzuri za kazi,na wengine ni wafanyabiashara maarufu.
Hahaha eti wasomi wa "ILIMU DUNIA AU FIRDAUS?[emoji3][emoji3] Unajua maana ya msomi?
 
Wewe labda mgeni Tanzania,BAKWATA wana shule nyingi tu,na ni nzuri,wapo wasomi wengi wamemaliza huko.Shule karibia 30 na vyuo vya dini zaidi 32.Na ndani ya BAKWATA wapo wasomi wengi tu.
Shule 60 ndio nyingi? Wakati idadi hiyo ya shule Ni Sawa n'a za wakristo ktk mkoa mmoja tu?
 
Hawa masheikh nao ni wachumia tumbo tu, hawana tofauti na wanasiasa.
 
Hebu ACHA UONGO ndani ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan, eti Mwanafunzi wa dhehebu moja la kikristo hawezi kusoma katika chuo cha dhehebu lingine???

Umelitoa wapi hili?
Kusalimiana kwenu tu kuko tofauti kuna Bwana Yesu asifiwe na Tumsifu Yesu kiristo.Ndio wataka kuniambia hamna utofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…