Kati yako wewe na yeye nani anaejua zaidi? Yeye na wenzie ndio waliokuwa mstari wa mbele kupigania wanachokijua huku wameshikana mikono, unaweza vipi kumpinga mwalimu wako wewe shabiki tu.
Yaliyomfika huko alikokuwa kwa miaka tisa yamemfunza asirudie kushindana na mwenye nguvu zaidi yake, kama kuipigania "Zanzibar yao" hiyo Zanzibar yao walipewa na nani? au waliinunua wapi? na kwanini wao kuipigania "Zanzibar yao" kusababishe waumie wengine ambao hawahusiki?
Ile Zanzibar ninayoijua mimi ni ya wote, hakuna mwenye Zanzibar yake pale, ule waliofanya ulikuwa ni ulevi tu wa ubinafsi na mihemko uliowasababishia matatizo, sasa mwenzako anakiri alikosea, wewe bado unataka umrudishe alikotoka wakati akiteseka kule wewe ulikuwa nyumbani na familia yako unakunywa chai na vitumbua.