Sheikh Ponda: Sheria ni kinga ya Haki za Binadamu, si chombo vya kutesa Wananchi

Sheikh Ponda: Sheria ni kinga ya Haki za Binadamu, si chombo vya kutesa Wananchi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Akizungumza mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda amesema kwamba amejiunga na Chama hicho kwa lengo la kuongeza wigo wa maeneo ambayo anaweza kupigania haki na utawala wa Sheria hususani Katiba Mpya.

Amesema kwamba Taifa linatakiwa kuongozwa kwa misingi ya Sheria, lakini anadai kwamba zipo Sheria zimekuwa zikitumiwa kukandamiza Watu.

"Taifa letu linastahili kuongozwa kwa misingi ya sheria, ambapo kila mtu bila kujali cheo chake, dini yake, au kabila lake yuko chini ya sheria.Sheria inapaswa kuwa kinga ya haki za binadamu sio chombo cha kuwatesa wananchi," amesema Sheikh Ponda.

Anaongeza "Tumeshuhudia jinsi sheria kama ile ya Kupambana na Ugaidi ikitumika vibaya kuwalenga wale wanaopinga dhuluma. Tumeshuhudia wananchi wakipigwa na vyombo vya dola kwa sababu ya kulinda kura zao zisiibiwe."
 
Unajua, kiongozi wa dini anapokemea uovu wa ccm anahusishwa na kujiingiza kwenye siasa, watafunga watu wengi kiasi kwamba magereza hayatatosha
 
Back
Top Bottom