Ufahamu wa wengi wa ma - shekhe wa kiislamu ambao hushinda kutwa nzima wamevaa majoho na vibaragashia ni mdogo sana...
Mmoja wao ni huyu.
Kwa namna fulani anajaribu kuwa "neutral" Kwa kujitenga na "udini", lakini ameshindwa kufanya hivyo kwani kupitia maandishi yake haya, kajiweka wazi
kuwa anatetea dini na
anamtetea mwislamu mwenzake..
Shekhe
Mohamed Said, fahamu kuwa sisi hatuna shida na dini au uislamu wa huyu mama yenu Rais Samia Suluhu Hassan.
Shida ya Watanganyika ni mkataba wa kutoa bure rasrimali bandari zetu Watanganyika za bahari na maziwa Kwa waarabu ambazo urithi wetu na watoto tuliopewa na Mungu baba...
Na shida yetu nyingine Kwa huyu mama ni U - zanzibari wake na Hilo hakuna kumung'unya maneno...!!
Maswali ni haya na kama una akili hebu yajibu bila kujificha kwenye udini. Na ukiitendea haki nafsi yako, na ukajibu Kwa ufasaha, utapanua ufahamu wako sana na utaelewa kuwa mama na mwislamu mwenzenu katukosea sana Watanganyika...
1. Kwamba, iweje Rais wa JMT, ndugu Samia Suluhu Hassan (Mzanzibari) Kwa kushirikiana na waziri wake wa ujenzi na usafirishaji (ambayo si wizara inayohusika na mambo ya muungano) lakini alimteua waziri Mzanzibari Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mzanzibari) pamoja na Katibu mkuu wa wizara hiyo ambaye naye pia ni (Mzanzibari) wakapanga deal la kuuza bandari za Tanganyika pekee wakiziacha za kwao Zanzibar? Huoni tatizo hapo?
2. Na, Je unajua kwamba mambo ya bandari na bahari ni mambo ya muungano? Iweje Rais wa JMT anafanya jambo kubwa kama hili linalohusu muungano lakini akihusisha upande mmoja tu (Tanganyika) akiacha upande mwingine wa muungano yaani Zanzibar? Je, huku si kuvunja katiba?
3. Na mwisho Unataka Watanganyika wanyamazie jambo Kwa sababu za kijinga za eti kuambiwa wanavunja muungano au kufanya ubaguzi wa kidini?
No way!!
, Watanganyika hatunyamaza kwa hili mpaka huyu mama akilli kuwa amekosea na arekebishe kosa lake Hilo mara moja na ikiwezekana aachie U -Rais wetu waingie wenye akili na maarifa ya kutenda...!!