Mohamed Said salam sheikh
Naanza kwa tahadhari kwamba unapoleta jambo ni vema ukajiridhisha na uthabiti wake.
Bandiko kutoka kwa Sheikh Hassan halibebi uzito sana isipokuwa kwa kuletwa nawe kwa umaarufu wako
Chukua tahadhari ili usinasibishwe na 'mzigo' kwavile tu umesimama karibu nayo
Sheikh Said, sidhani kama Sheikh Hassan kafanya 'homework yake' vizuri na ikiwa ni hivyo kuna tatizo .
Kwanza, Hassan anasema hoja ilianza kwamba bandari za Tanganyika zinauzwa.
Ni kweli kwasababu Zanzibar imesema bandari zake hazihusiki hivyo zilizobaki ni za Tanganyika.
Neno bandari zimeuzwa linaweza kuwa na ' semantic '. Hivyo Sheikh Hassan aelewe bandari zilihusu Tanganyika
Pili, kwamba MoU imesainiwa na Wazanzibar wawili, ni Ukweli na sahihi zipo. Kwaninia Wazanzibar wanatajwa? Jibu ni kwamba wizara husika si suala la muungano lakini kubwa zaidi ni kuondolewa kwa bandari za Zanzibar.
Ni Wazanzibar wanaolalamika mambo ya muungano kuongezwa, sasa wanaposaini yasiyowahusu inatia shaka.
Lakini pia wapo wataalamu wanahoji, sahihi ya Mwanasheria mkuu ipo wapi?
Tatu, Mh Mbowe alizungumza kwa kuchagua maneno yake kwa umakini mkubwa sana.
Kwa mtu aliyesikiliza video hakuna mahali alileta taharuki zaidi ya kutahadharisha kile alichokiona na kinachoweza kutafsiriwa kinyume na hali ilivyo. Ile video ukiisikiliza utabaini nia ovu ya wanaojaribu kuipotosha, sina hakika sheikh Said na Sheik Hassan wameiona na kuidurusu kwa kina na utulivu video hiyo!
Tatu, hoja ya bandari haikuanza na bandari za Tanganyika bali MoU iliyovuja kutoka serikalini na ambayo haikuwa katika ratiba za Bunge kwa mujibu wa Wataalam. Kuvuja huko na yale yaliyomo kumeibua hisia na mjadala mkali ukihusisha wanasheria, wanasiasa na hata viongozi wa dini zote akiwemo Sheikh Ponda.
Kwamba walizungumza ni viongozi wa Kikristo, hilo si kweli kwani wapo wa dini zote na wana haki kama Raia wengine. Sheikh Hassan akitazama mijadala kwa jicho la dini hatakosa hoja hata siku moja kwasababu Tanzania ina dini mbali mbali na Rais wake wana haki ya kushiriki mijadala bila kutumia dini zao.
Nne,Kwamba viongozi wa Kikristo walikuwa kimya wakati wa utawala wa JPM, hii ni hoja yenye ukweli nusu.
Ukweli uliokamilika ni kwamba viongozi wa dini zote akiwemo sheikh Hassan walikaa kimya wakati uovu ukitendwa, watu kupigwa risasi au kuokotwa katika viroba.
Hivyo, kukaa kimya halikuwa suala la dini moja, lilikuwa la viongozi wote na hapa umma ulifikia mahali kutilia shaka uadilifu na uongofu wa viongozi wa dini pale wanaposhangilia na kuombea viongozi dua hata za biashara za madini na ujenzi wa madaraja bila kujali utu na uhai wa Raia wao. Sheikh Hassan anakumbuka vizuri hili
Tano, kwamba hoja haijaangaliwa kiuchumi si kweli. Sheikh Hassan anataka kuaminisha umma kwamba tatizo ni mkataba wa uchumi. Ukiwasiliza watu wote wakiwemo Wabunge hakuna anayepinga uwekezaji, watu wanapinga kilichomo ndani ya mkataba ambacho viongozi wa serikali wanapaswa kutetea kwa hoja.
Sheikh Hassan atakumbuka Bunge letu lilijadili kauli ya Mbowe zaidi badala ya Mkataba au basi hoja za kiuchumi.
Tulitarajia Sheikh Hassan aanze kusota vidole kwa Bunge kuliko kushambulia watoa maoni kwa imani zao.
Sita, Bunge la JMT lina watu wa aina na imani zote. Bunge limepitisha Mswada bila kuangalia kingine, na hivyo Sheikh Hassan amekuwa na jicho chongo la kutoona Wabunge walioko ni akina nani.
Saba, kwamba Rais SSH anashambuliwa kwa udini ni hoja dhaifu . Sheikh atueleze ni Rais gani alipata ''immunity' ya kutoshambuliwa ? Urais ni taasisi inayobeba sera na maono ya Taifa.
Ni jambo la ajabu sana kama Rais awaye atapewa ufaulu tu kwa kuangalia jinsia, asili au dini.
Hilo halikuwepo na wenye fikra ongofu hawalifikirii hata kidogo.
Nane, inaonekana Sheikh Hassan alichukizwa na neno Tanganyika. Neno hilo linasemwa kila siku kule Zanzibar tena kwa indhara, kashfa na matusi, leo likitumiwa na Watanganyika linakuwa tusi! Sheikh Hassan na jicho chongo.
Tisa, kwavile Sheikh Hassan ameeleza kuna faida za kiuchumi, ni yeye mwenye dhima ya kueleza faida hizo ni zipi.
Kutuhumu wanaotoa maoni tofauti na matarajio yake wakati hana alichoweka mezani si jambo sahihi.
Kumi, hoja ya Sheikh Hassan inajengwa katika misingi ya udini badala ya uhalisia. Sheikh arudi na kupita video ya Mbowe, apitie mkataba na malalamiko ya wananchi wakiwemo viongozi wote wa dini, arejee katika mkataba na kufafanua vifungu vinavyolalamikiwa na aeleze faida za uchumi. Bila hayo andiko lake lina sura tofauti
Ni kwa msingi huo tunamshauri tena
Mohamed Said kuwa mwangalifu wakati wa 'kubeba mizigo' , mingine inachuruzika shombo na hivyo kuichukiza kanzu yake nadhifu achilia mbali jicho la makumi na mamia ya Wapendwa wanaomtazama kwa mahaba, mfano na wivu mkubwa!
Mag3 Fundi Mchundo JokaKuu Pascal Mayalla