Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Bahati mbaya Mohamed hatafuata ushauri wako kwa sababu yeye anaangalia kila kitu kwa msingi ya kutetea dini yake na wafuasi wenzake wa dini hiyo dhidi ya udhalimu wa wakristu na dini yao. Wakati wakristu kama Lissu waliwatetea kwa sauti kubwa masheikh waliokuwa mahabusu na walikemea yaliyotokea Kibiti, Mohamed hajawahi kunyanyua sauti yake pale wakristu kama Lissu, Mbowe na wengine walipokuwa wanapitia wakati mgumu. Kwake yeye utu unapimwa kwa misingi ya Umma. Inasikitisha lakini haishangazi kumuona akipigia debe ya hoja kuwa Rais wa sasa anapingwa kwa sababu ya dini yake au/na uzawa ( lakini sio jinsia yake maana hata yeye ana tatizo na hilo) wake.Mohamed Said salam sheikh
Naanza kwa tahadhari kwamba unapoleta jambo ni vema ukajiridhisha na uthabiti wake.
Bandiko kutoka kwa Sheikh Hassan halibebi uzito sana isipokuwa kwa kuletwa nawe kwa umaarufu wako
Chukua tahadhari ili usinasibishwe na 'mzigo' kwavile tu umesimama karibu nayo
Sheikh Said, sidhani kama Sheikh Hassan kafanya 'homework yake' vizuri na ikiwa ni hivyo kuna tatizo .
Kwanza, Hassan anasema hoja ilianza kwamba bandari za Tanganyika zinauzwa.
Ni kweli kwasababu Zanzibar imesema bandari zake hazihusiki hivyo zilizobaki ni za Tanganyika.
Neno bandari zimeuzwa linaweza kuwa na ' semantic '. Hivyo Sheikh Hassan aelewe bandari zilihusu Tanganyika
Pili, kwamba MoU imesainiwa na Wazanzibar wawili, ni Ukweli na sahihi zipo. Kwaninia Wazanzibar wanatajwa? Jibu ni kwamba wizara husika si suala la muungano lakini kubwa zaidi ni kuondolewa kwa bandari za Zanzibar.
Ni Wazanzibar wanaolalamika mambo ya muungano kuongezwa, sasa wanaposaini yasiyowahusu inatia shaka.
Lakini pia wapo wataalamu wanahoji, sahihi ya Mwanasheria mkuu ipo wapi?
Tatu, Mh Mbowe alizungumza kwa kuchagua maneno yake kwa umakini mkubwa sana.
Kwa mtu aliyesikiliza video hakuna mahali alileta taharuki zaidi ya kutahadharisha kile alichokiona na kinachoweza kutafsiriwa kinyume na hali ilivyo. Ile video ukiisikiliza utabaini nia ovu ya wanaojaribu kuipotosha, sina hakika sheikh Said na Sheik Hassan wameiona na kuidurusu kwa kina na utulivu video hiyo!
Tatu, hoja ya bandari haikuanza na bandari za Tanganyika bali MoU iliyovuja kutoka serikalini na ambayo haikuwa katika ratiba za Bunge kwa mujibu wa Wataalam. Kuvuja huko na yale yaliyomo kumeibua hisia na mjadala mkali ukihusisha wanasheria, wanasiasa na hata viongozi wa dini zote akiwemo Sheikh Ponda.
Kwamba walizungumza ni viongozi wa Kikristo, hilo si kweli kwani wapo wa dini zote na wana haki kama Raia wengine. Sheikh Hassan akitazama mijadala kwa jicho la dini hatakosa hoja hata siku moja kwasababu Tanzania ina dini mbali mbali na Rais wake wana haki ya kushiriki mijadala bila kutumia dini zao.
Nne,Kwamba viongozi wa Kikristo walikuwa kimya wakati wa utawala wa JPM, hii ni hoja yenye ukweli nusu.
Ukweli uliokamilika ni kwamba viongozi wa dini zote akiwemo sheikh Hassan walikaa kimya wakati uovu ukitendwa, watu kupigwa risasi au kuokotwa katika viroba.
Hivyo, kukaa kimya halikuwa suala la dini moja, lilikuwa la viongozi wote na hapa umma ulifikia mahali kutilia shaka uadilifu na uongofu wa viongozi wa dini pale wanaposhangilia na kuombea viongozi dua hata za biashara za madini na ujenzi wa madaraja bila kujali utu na uhai wa Raia wao. Sheikh Hassan anakumbuka vizuri hili
Tano, kwamba hoja haijaangaliwa kiuchumi si kweli. Sheikh Hassan anataka kuaminisha umma kwamba tatizo ni mkataba wa uchumi. Ukiwasiliza watu wote wakiwemo Wabunge hakuna anayepinga uwekezaji, watu wanapinga kilichomo ndani ya mkataba ambacho viongozi wa serikali wanapaswa kutetea kwa hoja.
Sheikh Hassan atakumbuka Bunge letu lilijadili kauli ya Mbowe zaidi badala ya Mkataba au basi hoja za kiuchumi.
Tulitarajia Sheikh Hassan aanze kusota vidole kwa Bunge kuliko kushambulia watoa maoni kwa imani zao.
Sita, Bunge la JMT lina watu wa aina na imani zote. Bunge limepitisha Mswada bila kuangalia kingine, na hivyo Sheikh Hassan amekuwa na jicho chongo la kutoona Wabunge walioko ni akina nani.
Saba, kwamba Rais SSH anashambuliwa kwa udini ni hoja dhaifu . Sheikh atueleze ni Rais gani alipata ''immunity' ya kutoshambuliwa ? Urais ni taasisi inayobeba sera na maono ya Taifa.
Ni jambo la ajabu sana kama Rais awaye atapewa ufaulu tu kwa kuangalia jinsia, asili au dini.
Hilo halikuwepo na wenye fikra ongofu hawalifikirii hata kidogo.
Nane, inaonekana Sheikh Hassan alichukizwa na neno Tanganyika. Neno hilo linasemwa kila siku kule Zanzibar tena kwa indhara, kashfa na matusi, leo likitumiwa na Watanganyika linakuwa tusi! Sheikh Hassan na jicho chongo.
Tisa, kwavile Sheikh Hassan ameeleza kuna faida za kiuchumi, ni yeye mwenye dhima ya kueleza faida hizo ni zipi.
Kutuhumu wanaotoa maoni tofauti na matarajio yake wakati hana alichoweka mezani si jambo sahihi.
Kumi, hoja ya Sheikh Hassan inajengwa katika misingi ya udini badala ya uhalisia. Sheikh arudi na kupita video ya Mbowe, apitie mkataba na malalamiko ya wananchi wakiwemo viongozi wote wa dini, arejee katika mkataba na kufafanua vifungu vinavyolalamikiwa na aeleze faida za uchumi. Bila hayo andiko lake lina sura tofauti
Ni kwa msingi huo tunamshauri tena Mohamed Said kuwa mwangalifu wakati wa 'kubeba mizigo' , mingine inachuruzika shombo na hivyo kuichukiza kanzu yake nadhifu achilia mbali jicho la makumi na mamia ya Wapendwa wanaomtazama kwa mahaba, mfano na wivu mkubwa!
Mag3 Fundi Mchundo JokaKuu Pascal Mayalla
Profesa Lipumba ni mmoja wa wasomi wa kwanza waliolalamikia huu mkataba. Jopo la TLS lililopitia huu mkataba lilijumuisha waislamu. Profesa Shivji ni msomi mwingine muislamu aliyeukosoa huu mkataba. Hao wote hawaoni anawaona wakina Anna, Tundu, Freeman, John na wamisheni wengine. Hajiulizi kwa nini huu mkataba hautetewi at full throttle na wanasheria wabobezi wa serikali na viongozi wengine?
Humu ndani hakuna Rais aliyepita ambae hajawahi kukosolewa. Wakati wa JPM watu kutoka dini zote walikuwa wakimkosoa. Sikusikia hata siku moja akitetewa kuwa wanaomkosoa wanafanya hivyo kwa sababu wana chuki na wamisheni.
Mohamed anachezea kiberiti petrol station bila kujali kuwa mlipuko wake utatuathiri wote pamoja na yeye. Msingi wa nchi yetu ni secularism na jamii yetu imeishi kwa upendo na ushirikiano bila kujali dini zetu. Mohamed na wenzake wasiruhusiwe kutuharibia nchi yetu.
Amandla....
Nguruvi3 Mag3 JokaKuu