Sheikh wa Mkoa Mwanza (Kuhusu Mjadala wa Bandari): Walaaniwe wote wenye nia ovu na Rais Samia

Mzee Wangu namjua na kumuheshimu sana na najua kuwa amelewa sifa za heshima anayopewa kwenye ngazi tofauti. Ila kwa hili amekurupuka sana au amekosa u shauri ningeomba asikie sana na awe wa mwisho kufungua mdomo wake Ili akidhi Sauti ya waislamu wote anao wasemea
 
Ikiwa ni sheikh wa mkoa ina maanisha ni kutoka BAKWATA na BAKWATA ni tawi la CCM kama ilivyo UWC ama UVCCM, sasa unataraji sheikh aseme nini zaidi ya kusifia na kusupport.

Ukimuuliza huyo sheikh mkataba unahusu nini hana hata moja analolijua. Anachofanya yeye ni kutimiza ada kama mwanchama kufuata maelekezo toka juu.
 
Tamko la mtu asie kuwa na akili hata kidogo ndio tamko gani Hilo lilolenga kuisema dini ya KIKRISTO yani huyu shehe kadhihirisha namba udini ulivyomkaa kwenye mishipa yake ya damu,kaongea pumba tupu sijui hata huwa anaambia nini waumini wake zaidi ya kuwapotosha

THIS IS BULLSHIT
 
Wanalipwa kisirisiri.
Hapo bado hajazungumza mkubwa wao Zuberi, huyo ndio atakuja kumaliza kabisa na lafudhi ya kiarabu feki kama mshihiri aliefilisika kwa kumwaga misifa ya mkataba wa bandari ambao hata haujui unaongelea nini.

Jinsi wanavyomdhihaki Mungu kwa njaa zao usishangae hata wakatoa aya ya uongo kuwa DP World iliandikwa kwenye Quran.
 
Huyu anatembelea vieite ulinzi na mshahara mrefu vyote vya serikali.
 
Hawa wanasahau kuwa Hata mangungo Alikua Ana Dini mana ukanda Wa Pwani Ilikua tayari umeshapokea Dini zilizokuja na majahazi Tangu Karne ya 12 . Hata Hivyo mangungo hakuuza Ardhi ya Zanzibar Kwa sababu Ilikua Ina utawala wake. Na mangungo hakuona Mbele kuwa wale Wageni wangekua na athari kiasi Gani Kwa vizazi Mbele yake.

Kwa mkataba Huu Wa DPW Hata usalama Wa nchi Utakua na wakati mgumu sana sana sana. Ni kweli Hawa Jamaa watagawa pesa nyingi sana Kwa watu Kwa sababu Wana agenda ya miaka mingi Mbele .

Ni kweli mashehe na Waislam ni rahisi sana kutumika na kuligawa taifa na Hata kuliingiza kwenye vurugu na ugaidi Mkubwa Zaidi ambao haujawahi kutokea Kwa sababu kubwa kuwa Hawa Waarabu kupitia Dini wanakujaga mara ZOTE na pesa na misaada mikubwa ya kujenga misikiti Kila MAHALI. Kujenga Nyumba za ibada Kwa Waarabu ni thawabu kubwa sana na Serikali zao zinaebdeshwa kidini . Magaidi hua wanaandaliwa na Matajiri Wa Kiarabu kushirikiana na Nchi za Magharibi hasa Marekani.
Hata Hao Dubai wanajua kuwa Mwenyezi MUNGU hakuruhusu Mwanamke kuwa Sultani na kuongoza nchi. Waarabu wanajua wazi kuwa Kipindi hiki Chini ya mwavuli Wa Demokrasia feki ya CCM iliyoruhusu nchi kugawanyika Kwa manufaa ya Wachache ,ndicho kipindi Cha kurejesha Utawala Wa kisultani na koloni lao.

Mfano Ikitokea vita Kati ya Tanzania na Msumbiji au Rwanda nini kitatokea ?
Nadhani wakubwa Wa vyombo Vya Dola hawana habari na hili Kwa sababu vita Kwa nafasi zao haviwagusi wanaweza wakajificha HUKO Dubai na familia zao lakini . Tabú kubwa itabaki Kwa wapiganaji Wa Chini na familia zao.
Ikitokea vitaka Kati ya Tanzania na Msumbiji au Malawi au Rwanda ni wazi kuwa DPW watanunuliwa na upande wenye fedha nyingi ikiwemo upande unaosaidiwa na Marekani na nchi za kibepari.
DPW watazorotesha usalama Wa nchi na kutoa Siri Kwa adui Kwa urahisi sana. Vita za Mataifa na Ukoloni mambo Leo unaongozwa na Nguvu ya kipesa . MWENYE pesa za Kununua mamluki ndiye anayeshinda .
Nchi imeuzwa Kwa mkataba Huu. CCM miaka yote inatumia Dini na ukabila kudhoifisha umoja Wa watanzania dhidi ya udhaifu wao.
Kama hawajui ni Kwamba bandari ni suala la Muungano lakini wameanza na bandari ya DSM Kisha Zanzibar itafuata Kwa mgongo Wa Nyuma. Watapandikiza Kibaraka wao kule na miaka michache ijayo bandari ya Zanzibar itauzwa kutokana na ukweli kuwa mizigo yote itaishia DSM Toka Dubai.
Zanzibar itabidi iuzwe Kwa sababu BIDHAA nyingi watazifuata DSM Badala ya Dubai. Hapo watakwepa vipi kuiuza bandari ya Zanzibar.


Tanzania kiusalama haifungamani na China Wala Marekani lakini Kwa mkataba Huu Tanzania italazimishwa kufungamana na Marekani .
Bandaria kiusalama ni kiungo kikubwa sana wakati Wa uvamizi. Wakoloni walivamia bara la Afrika kupitia majahazi.

Usalama Wa nchi Hii Utakua mdogo sana .

Wazungu wanataka Madini yetu ya kuzalisha Betri Kwa wingi sana .
Wazungu wanataka Urenium, Wazungu wanataka dhahabu ,Wazungu wanataka malaa ya mawe Kwa Sasa , Wazungu wanataka mafuta yatakayopitia Tanga kutoka Uganda.

Mana Samia ameshindwa kuisimamia uchumi Wa nchi Hii Kwa asilimia mia moja . Haiwezekani uchumi Wa nchi Hii yenye rasilimali nyingi na watu wengi ushindwe kuimarika mpaka aje mgeni Kununua nchi . Hapana.
Mwarabu atakaa pale Bandarini Kwa mwaka mmoja tuu atapata pesa za Kununua vifaa vyote Vya kisasa Kwa pesa atakazovuna pale Bandarini.

Rais Kwa mamlaka aliyopewa ameshindwa kuamuru Bandari ifungwe kamera Kila Kona na Taarifa za mizigo yate na makontena yanayoingia yatumwe ofisini kwake . ?

Mashehe Badala ya kuishauri Serikali irekebishe vifungu vinavyokinzana na Kariba na uhuru Wa nchi yetu wao wanahangaika na wakosoaji na Udini wanaouanzisha wao Kwa manufaa ya MTU mmoja na familia yake?
Hii nchi SIO ya kifalme kuwa Labda Sisi wote ni Kama Watoto Wa Rais . No. Hii ni nchi ya kidemokrasia ,Rais anachaguliwa baada ya Kuomba kura . Anapobainika kuwa aliomba kura Kwa malengo yake basi anatolewa madarakani Kwa kampeni kubwa au Kwa maandamano makubwa . Hafai kama halindi nchi na rasilimali za Nchi na usalama Wa nchi dhidi ya adui Wa NJE?

Hii nchi haikuwa na usalama Mkubwa dhidi ya maadui Wa Nje kimchezo mchezo . Wazee Wetu walijitesa Kwa kukataa kununuliwa na kuiuza nchi Ili kulinda uhuru Wetu na utaifa Wetu , Amani yetu na umoja Wetu. Tungeweza kuwa kama Kongo .
Kongo waliuza nchi Yao Kwa Ufaransa wao wakabaki na magitaa ya kucheza rumba. Sasa Sisi leo tunauza nchi yetu Kwa Waarabu ,tutabaki na Simba na Yanga . Na makanisa feki na manabii feki na misikiti itakayojazana na waumini wasio na Elimu ya kujitawala Wala kuutawala uchumi Wa kimataifa na rasilimali zetu. Taifa la wachuuzi Wa BIDHAA kutoka Nje. Wanyama Sasa watabebwa kwenye Meli na SIO ndege Tena. Miaka mia ijayo hapatakuwa na nchi moja ya Tanzania . Nchi itagawanyika vipande vipande , waafrika weusi watauana Kwa unafiki Wa kuwapigania matajiri Wa Kizungu na Kiarabu kama kule Sudani.
Watakaopata wakati mgumu ni Watoto Wa maskini watakaoajiriwa kwenye Majeshi. Hawatalala usingizi kwenye majumba Yao WAKIWA wameacha Sílaha kwenye maghala . Askari Watakwenda majumbani na Bunduki zao kama kule Kongo.
Hapata kuwa na nchi huru Bali ni pango la wezi.
Tumeuzwa Kwa sababu ya kushindwa kwake.

. Wawaulize WanaCCM Kule Zanzibar na Wazanizibara weusi WALIOKO Zanzibar ni Kwa Nini wapotayari muda wote KUFANYA Mapinduzi alimradi wasitawaliwe Tena na Hao Wageni na masalia yao?
 
 
Hii ungemperekea Sheikh inbox kabisa ili ajielimishe.
Nakuunga mkono
 
Kuna mambo 'interesting' na sijui kama watu wanayaona

Waraka wa Shura sikumbuki kama Mo aliuleta hapa kwasababu ulikuwa na ''Facts'
Huu wa Sheikh wa Bakwata ambayo Mo anaipinga kwa maneno na maandiko kauleta - ' Fanatic'

Sheikh Mohamed Said atachukua upande kama hoja ina 'fit narrative' yake.

Wabunge walimshambulia Mbowe kwasababu hawakuwa na hoja za kutetea mswada.
Mjadala wa Bunge ukazama kwa Mbowe na si Mkataba (Tulia A) uliopelekwa Bungeni.
Mbowe akaziba Ombwe la hoja kwasababu Wabunge wengine hata kuelewa kimendikwa nini sina hakika

Hoja yao dhidi ya Mbowe ni kutahadharisha, wakachukua maneno ya Utanganyika na Uzanzibar wakayafanya agenda. Wabunge hawasemi kuhusu Utanganyika na Uzanzibar unaonezwa kwa chuki na ACT Wazalendo ya akina Jussa, Duni na Othman Masoud

Wanamtuhumu Mbowe eti kwa kugusa muungano, lakini Wabunge hao hao hawasemi lolote wakati Jussa, Duni Haji na Masoud Othman wakitaka mamlaka kamili kwa maana moja, kuvunja muungano.

Upotoshaji umetumika kusema Wananchi hawataki uwekezaji. Hakuna anayekataa uwekezaji, Wananchi wanahoji maudhui (contents) za mkataba ambazo hatma yake itakuwa kama ile ya umeme wa Dowans.
Ndege za ATC haziruki kwasababu ya mikataba mibovu ya huko nyuma. Ubaya wa kuhoji upo wapi!

Na Ombwe la kujibu hoja limepelekea kuchomeka hoja ya udini. Watu wanaoshadidia hoja hii hawajibu hoja za maudhui ya mkataba, wamekomalia fulani ni mwislam na wawekezaji ni Waarabu.

Hivi Netgroup ya Mkapa, Dowans na Richmond za Kikwete zilikuwa za Waarabu!
JNHPP ya JPM si ya Waarabu, SGR si inajengwa na Edogan wa Turkiye anayelinda maslahi ya Waislam duniani kuliko Waarabu. Je, lini tuliacha kusema ya Mkapa, JK na JPM?

Suala zima ni upungufu wa hoja za kujibu na wanaposhindwa kujibu wanakimbilia Vihoja vya Mbowe na Udini.
 
Oyaa sheikh ubwabwa huu ndio msimamo wake "Hivyo basi, kama sheikh wenu wa Mkoa, natoa wito kwa kila mwislam popote alipo katika Mkoa huu, afunge kwa siku 3 na katika kila swala ya Ijumaa kuanzia Ijumaa hii ya tarehe 7 Julai 2023 misikiti YOTE 700 ya Mkoa wa Mwanza isome dua ya kunuti kuwalaani WATU WOTE wenye nia ovu na Rais Samia"
 
Ndugu hawa jamaa ikija hoja ya udini yuko tayari atunge uongo ili aonekane ana haki.
Mfuatilie huyu mzee uongo anaomwaga daliy humu.
Kutwa kucha kuongelea wapigania uhuru. Muulize kuhusu John Okelo atakuambia hamjui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…