Shemeji yangu amekataa! Abadani, Mwanangu hapimwi DNA ikibidi ndoa ivunjike tu

Nina watoto mapacha wale mapacha wasiofanana
Mimi ni mweusi kabisa Ile wanaitwa black beauty, baba mtu akicheka gizani utaona meno tu lakin katika wale mapacha wawili mmoja ni mweupe Sana na mwingine ni mweusi Sana,
Hii imekaaje? Rangi sio inshu Kuna Mambo ya ukoo,
Kuna kipindi flan flan Mr alianzaga my question lakin lilipofika kwa baba mkwe akamwita na kumlazimisha aniombe radhi, kwani alipokua anamuona Yule mweupe ndivyo alivyokuwa Bibi yake mzaa baba yake
So kabla ya yote angalieni asili kwanza
 
Hivi km mtu akipima blood group ukakuta mtoto ana blood group tofauti na wazazi wake,je baba atakua na chake hapo!??
 
Mkuu uhangaike na mtoto si wako? Biblia inakataa kubebe geneology isiyoyako.

Ndio maana wazee wanajiua mwishoni baada ya kujua mtoto aliye mhangaikia hakuwa wake na Mama alificha.

Ukumbuke Kiroho iko hivi. Mtoto kama si wako ukamlea kwa kudanganywa ni wako. Hata kama unampenda kivipi siku atakayogundua Baba yake wa Damu sio wewe na ni mwingine atakushangaza na wala usilaum ni Nature.
Na hio siku ipo na inakuja tu, kuna siku mama yake atamwambia kuwa wewe si baba yake mzazi.
 
Okay sawa Mwanamke kagomesha.
Finally brother Ako anaamua nini ?
Yeye kama mwanaume, kulea mtoto wa mshikaji kama Baba mlezi au Kufanya nn...

Bro Ako kapigwa
Sema nini Rasterman mpelekee hii kutoka Katika Biblia Takatifu.

1 Pet 3:7
Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.
 
Hata ningekua mimi ningegoma kama ni kweli sijachepuka. Kuna vitu sio rangi tu ambavyo mtoto anaweza chukua kwa wazazi. Nyie mmekazania rangi rangi kama kafuata kwa bibi mzaa babu yake shangazi.
Kama hujachepuka huwezi kuwa mkali kwenye ishu ya DNA sababu unajiamini. 🤣🤣🤣
 
Huyo mtoto jibu liko wazi kabisa si wa huyo baba, Uthibitisho wa nin tena, Wasijisumbue sana.
Huwa mnapenda sana hio kauli ya kama huniamini tuachane ili kuficha ouvu wenu flani. DNA unpimwa na kuachana tunaachana vile vile 😀😀😀
 
Wakuu tumefika mwisho. Tumekuwa watabe kushauri kwenye mahusiano ya wengine huku mtandaoni lakini huku field Mke wa Brother(rafiki yangu wa longtime) ametushinda.

Ni hivi Mwaka Jana Mke wa Huyu Best Yangu alijifungua mtoto wa kiume. Tulifurahi kupata mtoto wapili na sisi kama ndugu na jamaa wa karibu sana ukizingatia yeye jamaa alinisaidi sana kusoma enzi hizo kipesa na kimawazo basi tulimfanyia Tafrija ndogo ya kupata mtoto.

Siku chache baadae furaha ya jamaa iliingia shubiri kila alipokuwa akifatilia ukuaji wa mtoto.

Yaani mtoto amekuwa na sura na mwonekano tofauti na Baba na Mama yake.

Yaani Mshikaji ni Mweusi na Mke wake maji ya kunde lakini Mtoto ni Mweupe.

Kwa sayansi ndogo tuliyo nayo kama baba mweusi na Mama maji ya kunde sio rahisi kupata mtoto mweupe. Pengine angepata rangi ya kunde kama Mama yake au Mweusi kabisa kama Baba yake.

lakini Baba ni msomi hawezi kufanya maamuzu based on just feelings. Ameamua kushauriana na mkewe kuwa wakampime DNSA maana jamaa roho inakataa kumpenda mwanaye kati kati ya mashaka.

Mke amekataa kata kata kuwa Mwanaye hapimwi DNA ikibidi hata ndoa ivunjike.

Ana dai kama hamwamini mke wake basi bora waaachane.

Mimi na Braza tume baki mdomo wazi juu ya msimamo wa Mwanamama huyu.

Tulitegemea angekubali ili kumwondolea hofu mumewe na upendo uzidi kutamalaki. Hali imekuwa tofauti.
Wewe umeoa? Mnapendaga kuingilia mambo ya watu ya nini? Lione lilivyokomaa! Mwanaume unakuwa kama binti? Wacha hizo mwamba jali business zako! Nimeupenda msimamo wa huyu binti! Hakuna kurudi nyuma!
 
Wakuu tumefika mwisho. Tumekuwa watabe kushauri kwenye mahusiano ya wengine huku mtandaoni lakini huku field Mke wa Brother(rafiki yangu wa longtime) ametushinda.

Ni hivi Mwaka Jana Mke wa Huyu Best Yangu alijifungua mtoto wa kiume. Tulifurahi kupata mtoto wapili na sisi kama ndugu na jamaa wa karibu sana ukizingatia yeye jamaa alinisaidi sana kusoma enzi hizo kipesa na kimawazo basi tulimfanyia Tafrija ndogo ya kupata mtoto.

Siku chache baadae furaha ya jamaa iliingia shubiri kila alipokuwa akifatilia ukuaji wa mtoto.

Yaani mtoto amekuwa na sura na mwonekano tofauti na Baba na Mama yake.

Yaani Mshikaji ni Mweusi na Mke wake maji ya kunde lakini Mtoto ni Mweupe.

Kwa sayansi ndogo tuliyo nayo kama baba mweusi na Mama maji ya kunde sio rahisi kupata mtoto mweupe. Pengine angepata rangi ya kunde kama Mama yake au Mweusi kabisa kama Baba yake.

lakini Baba ni msomi hawezi kufanya maamuzu based on just feelings. Ameamua kushauriana na mkewe kuwa wakampime DNSA maana jamaa roho inakataa kumpenda mwanaye kati kati ya mashaka.

Mke amekataa kata kata kuwa Mwanaye hapimwi DNA ikibidi hata ndoa ivunjike.

Ana dai kama hamwamini mke wake basi bora waaachane.

Mimi na Braza tume baki mdomo wazi juu ya msimamo wa Mwanamama huyu.

Tulitegemea angekubali ili kumwondolea hofu mumewe na upendo uzidi kutamalaki. Hali imekuwa tofauti.
Hii rahisi sana. Kinachohitajika ni vinasaba vya mtoto na aba. Baba amchukue achukue vinasaba vyake na mtoto apeleke kupima. Kwani lazima mama aambiwe? Vinasaba vya mama havihitajiki katika kupima DNA ya baba na mtoto. Vinasaba vya mama vinahitajika tu kuthibtisha kama huyo maa ni mama wa mtoto kweli. Saa sioni niny mnahangaika na huyo mama vipi. Chukuwa mwanao nenda mkapimwe DNA, kwisha. Au mnaogopa huyo mama atawakunja!
 
Rangi ya mtoto haitoshi tu kumshuku, mimi mwenyewe chocolate, mke wangu mweusi ila binti wetu cheupeee!!! Lakini muonekano wa uso wa binti tunafanana balaa belua.
Chukueni nywele ya huyo mtoto kisiri mkapime ili kuondoa mashaka.
 
Wakuu tumefika mwisho. Tumekuwa watabe kushauri kwenye mahusiano ya wengine huku mtandaoni lakini huku field Mke wa Brother(rafiki yangu wa longtime) ametushinda.

Ni hivi Mwaka Jana Mke wa Huyu Best Yangu alijifungua mtoto wa kiume. Tulifurahi kupata mtoto wapili na sisi kama ndugu na jamaa wa karibu sana ukizingatia yeye jamaa alinisaidi sana kusoma enzi hizo kipesa na kimawazo basi tulimfanyia Tafrija ndogo ya kupata mtoto.

Siku chache baadae furaha ya jamaa iliingia shubiri kila alipokuwa akifatilia ukuaji wa mtoto.

Yaani mtoto amekuwa na sura na mwonekano tofauti na Baba na Mama yake.

Yaani Mshikaji ni Mweusi na Mke wake maji ya kunde lakini Mtoto ni Mweupe.

Kwa sayansi ndogo tuliyo nayo kama baba mweusi na Mama maji ya kunde sio rahisi kupata mtoto mweupe. Pengine angepata rangi ya kunde kama Mama yake au Mweusi kabisa kama Baba yake.

lakini Baba ni msomi hawezi kufanya maamuzu based on just feelings. Ameamua kushauriana na mkewe kuwa wakampime DNSA maana jamaa roho inakataa kumpenda mwanaye kati kati ya mashaka.

Mke amekataa kata kata kuwa Mwanaye hapimwi DNA ikibidi hata ndoa ivunjike.

Ana dai kama hamwamini mke wake basi bora waaachane.

Mimi na Braza tume baki mdomo wazi juu ya msimamo wa Mwanamama huyu.

Tulitegemea angekubali ili kumwondolea hofu mumewe na upendo uzidi kutamalaki. Hali imekuwa tofauti.
Kitanda hakizai haramu. Jamaa amemegewa
 
Mwanamke anazingua kukataaa lakini na nyie Muachee ukengeee sasa mtoto kuwa mweupe ndo mkampime DNA[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] acheni ujingaa labda mseme hafanani suraa na wazazi...!!
 
Back
Top Bottom