Sawa mi mtoto sina amani nae nataka niujue ukweli ila si expect response ya ukali. Always response ya aina hio inaashiria kutojiamini ambako kunakuwa backed up na vitabia flani vya kishetani ambavyo mwanamke anavyo ikiwa ni pamoja na uchepukaji.
Wanawake huwa naamini wanaelewaga mimba ni ya nani toka awali ila swala la kuikabidhi ataangalia sehemu ambapo anahisi mtoto wake atalelewa kwa amani.
Kigezo kikubwa mwanamke anachoangalia ni kuwa je, mtoto huyo baba yake ana hela. Ikiwa baba mwenye uwezo kamkataa kibabe basi jua atasakiziwa asiye na uwezo alimradi tu anajua mtoto atasitirika. Ishu inakuja ambapo huyu baba wa kusakiziwa amekuwa makini zaidi kufuatilia mimba na akahisi kapigwa.