Shemeji yangu kanogewa kukaa kwangu. Kamaliza chuo 2020 lakini haondoki, nifanyeje?

Na saa ingine hao wanakuwaga mizigo kweli kweli mana unakuta akiamka asubuhi hata kujigusa hajigusi kisa yupo msaidizi wa kazi za ndani.
Na muda mwingi ni kuwalala mahousegirl,yaani mkiondoka wao ndio wanapiga show hadi kwenye masofa ambayo watoto wakitoka shule ndio biscuits zao zinagalagala hapo,🙂‍↕️🙂‍↕️
 
Nilipo achaga kuvuta bangi Nika Anza kuwa mtu mwema mpaka Leo mzee..

Ulicho zungumza sio ubinadamu...unaweza mfanyia ivyo siku moja jamaa akaja fanikiwa kupita wewe na ukaitaji msaada wake remember LIFE IS A CYCLONIC PROCESS.
Siungi mkono ubaya.
Ila kumsaidia shemeji yako au mtu yeyote siyo uhakika atakuja kuwa msaada kwako.
Pengine atakunyanyasa sana ukianguka kiuchumi. Hasa shemeji hao, bora dada au kaka zako.
 
Siungi mkono ubaya.
Ila kumsaidia shemeji yako au mtu yeyote siyo uhakika atakuja kuwa msaada kwako.
Pengine atakunyanyasa sana ukianguka kiuchumi. Hasa shemeji hao, bora dada au kaka zako.

Haina haja ya kuachana na MTU kwa ubaya au kumuita Mzigo .

Mambo yanabadilika sana ktk maisha so MTU anaweza ishi miaka sita bila bila ila akaja ku win ndani ya mwaka Mmoja na akamiliki Kila kitu na kuwa msaada kwako.

Njia ya kuhakikisha shemeji anakuwa busy na maisha ni nzuri ila kumfukuza haijakaa sawa
 
Mambo yote hayo ni njaa na umasikini , unakuwa unamchukia Kila MTU
Samahani mbona kama umekwazika sana?wewe unaona ni sawa kuishi kwa mwenzio miaka 6?yaani mwenzio anaamka asubuhi anaenda kutafuta anarudi jioni wewe upo unaangalia TV kwa miaka 6?unasema umaskini na njaa ndio unaleta chuki,naomba nikuhakikishie hakuna Tajiri anaweza vumilia huu upuuzi....
 
Ushauri mzuri, hafanyi hivyo kumkomoa, anamsaidia na kumfunza kuwajibika, katika kufanya hivyo anaanza kupata faida na kusaidia majukumu ya nyumbani. Lazima ampe wajibu wa kufanya, badala ya kuwa mzigo anakuwa mtu muhimu wa kusaidia majukumu ya familia.
 


Yes nimepitia hizo phase .

Nilichogundua njaa ndo tatizo ila kukaa na MTU miaka sita na una -provide kwake sioni tatizo kabisa



Kuna watu wanawahudumia wanawake na kuwapa Kila kitu Sasa iweje ndugu yangu nishindwe kukaa nae .

Umasikini ni mbaya sana Kila MTU unakuwa unaona yupo kinyume na wewe .

Ukiwa na uchumi mzuri HAYO maneno ya kumuita binadamu meenzako mzigo utaacha

Lack of humanity inachangiwa na umasikini wa fikra , uchumi mpaka tumbo.
 
Miaka 6 ni mingi sana kusikilizia mchongo.
nadhan dogo atakuwa ana bet. Na ndio inampa uvivu na high hopes kuwa siku moja atatusua.

Kuna graduates weng tu sikuhizi wanaendesha bajaji na hawakosi kulaza 20 - 30k faida. Ukitoa mafuta na hela ya boss.
Mwambie aache uvivu na asikae kizembe, miaka inaenda.
 
Miaka 6!Hapo wa kumlaumu mkeo kabla ya shemeji..mimi hapana siwezi kukaa na mdogo wangu miaka sita tangu amalize chuo,angechagua kurudi nyumbani au angeenda kupanga
Hii ni rasilimali hupaswi kuipoteza, mpe majukumu ya kufanya
 

Tena matajir ndio hawatak kabisa watu ambao hawajitumi.

Una nguvu uwezo . Why usipambane?.
Tena usikute hajawah kumpa wazo au business plan shemej yake?.

Kama yuko mjini, amuombe shemej akope . Anunue pikpik ya umeme. (4.5 ml) afanye bolt.

Hawez kosa 40k kwa siku.
Anakuwa anarudisha mdogo mdogo.
 
Nakubaliana na hoja yako 100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…