Shemeji yangu kanogewa kukaa kwangu. Kamaliza chuo 2020 lakini haondoki, nifanyeje?

Shemeji yangu kanogewa kukaa kwangu. Kamaliza chuo 2020 lakini haondoki, nifanyeje?

Wewe mwenyewe roho mbaya inakusumbua

Nyie nyie mkiwaona walemavu barabarani mnawapiga mateke, mna roho mbaya sawa wewe na mtoa mada

Mashoga…
Mbona umepaniki mkuu, jamaa angekuwa na roho mbaya angemruhusu huyo shemeji yake akae kwake miaka zaidi ya 6?
Yaani huoni tatizo kwa mwanaune mzima mwenye nguvu ambaye unafaa kuwa na familia kukaa kwa mtu miaka sita unalishwa kama mtoto mdogo?

Nimesha kwambia kuwa kukaa kwa mtu ili kuweka mambo yako sawa sio vibaya ila unatakiwa ujipe muda ujipange ingia kitaa tafuta mishe zozote kama mtoto wa kiume utafute hela ndani ya mwaka mmoja utakuwa umesha kusanya kiasi fulani cha kuanzia maisha yako uwapishe watu waishi kwa uhuru kwenye nyumba yao.
Shemeji yake kumpa makazi na chakula cha bure ni hisani tosha kabisa.

Waafrika wengi ni masikini kwa sababu ya kuendekeza upumbavu wa aina hii.
 
Mkuu naona umenisema Mimi kabisa, hapa umaskini lana mbaya sana tujitahidi kujenga uchumi vinzul.Nimehishi kwa shemeji 4 year, hila shemeji ni mwema sana hata dada yangu hakutaka niishi kwake hila shem halinipambania now sijisifu nipo vinzul mala x 10 zahidi yao hila wema ni akiba na hii thread himenikubusha ngoja niwa bless weekend na wajomba.
Aah kweli shemeji alipambana apewe maua yake, inaonekana ulikua PAPAYA sana kama saivi uko vizuri mara 10 na mwandiko ndio huu, hmm!
 
⊘ 𝘛𝘩𝘪𝘴 𝘮𝘦𝘴𝘴𝘢𝘨𝘦 𝘰𝘯𝘭𝘺 𝘢𝘱𝘱𝘦𝘢r𝘴 𝘵𝘰 𝘱𝘦𝘰𝘱𝘭𝘦 𝘸𝘩𝘰 𝘣𝘢𝘵𝘩.
 
Tena hao wanaofanya kazi bank ni rahisi sana kumshika mkono mtu kama huyo, hapo bank unaweza hata kumfanyia mpango akawa msafishaji huku anasikilizia ajira juu kwa juu

Inaweza ikatokea bank inataka wafanya kaz aka aply yeye wa karibu kwanza

Au akamsaidia kumtafutia mkopo kwa jina lake aende akajitafute

Mtoa mada ana roho mbaya sanaa, mchawi tu
Hilo suala la benki nimetolea mfano sijamaanisha kuwa huyo jamaa ni mfanya kazi wa benk.
Kwanza una uhakika gani kama huyo jamaa na shemeji yake wamesomea fani moja?
Je kama jamaa amesomea ualimu alafu shemeji yake amesomea udokta?
Ya kwamba amchukue amuingize kwenye sekta ya ualimu hali ya kuwa amesomea udaktari?
Alafu suala la kumshughulikia sio razima kitendo cha kumpa chakula na makazi ya bure ni hisani tosha kabisa kwa mtu mwenye akili.
 
Kuna mwanangu mmoja alimuliza mwanao sasa unataka kufanya nini!maana shule kidogo ni changamoto
Ndiyo akamjibu,baba yake anataka awe content creator au msanii 😄

Ova
Kwamba content creator na wasanii ndo wanadharaulika hv 😂
 
Shemeji yangu sasa kanogewa kwangu, amemaliza chuo 2020, bado anasema anasikilizia mchongo.

Shemeji Anashindia TV, kupiga stori na mdada wa kazi na vijiweni

Namuambia ajifunze ufundi anasema yeye anasema muda wake maalumu utafika
Ondoka wewe, unatuletea ufala hapa.
 
Hilo suala la benki nimetolea mfano sijamaanisha kuwa huyo jamaa ni mfanya kazi wa benk.
Kwanza una uhakika gani kama huyo jamaa na shemeji yake wamesomea fani moja?
Je kama jamaa amesomea ualimu alafu shemeji yake amesomea udokta?
Ya kwamba amchukue amuingize kwenye sekta ya ualimu hali ya kuwa amesomea udaktari?
Alafu suala la kumshughulikia sio razima kitendo cha kumpa chakula na makazi ya bure ni hisani tosha kabisa kwa mtu mwenye akili.
Angekuwa mwanamke huu uzi asingeleta angemtaka amle na ampe mtaji afungue biashara kwa vile mwanaume anakuja kumtangaza

Mnashindwa hata kuifadhiana wanaume mnaleta mambo ya kike
 
Mbona umepaniki mkuu, jamaa angekuwa na roho mbaya angemruhusu huyo shemeji yake akae kwake miaka zaidi ya 6?
Yaani huoni tatizo kwa mwanaune mzima mwenye nguvu ambaye unafaa kuwa na familia kukaa kwa mtu miaka sita unalishwa kama mtoto mdogo?

Nimesha kwambia kuwa kukaa kwa mtu ili kuweka mambo yako sawa sio vibaya ila unatakiwa ujipe muda ujipange ingia kitaa tafuta mishe zozote kama mtoto wa kiume utafute hela ndani ya mwaka mmoja utakuwa umesha kusanya kiasi fulani cha kuanzia maisha yako uwapishe watu waishi kwa uhuru kwenye nyumba yao.
Shemeji yake kumpa makazi na chakula cha bure ni hisani tosha kabisa.

Waafrika wengi ni masikini kwa sababu ya kuendekeza upumbavu wa aina hii.
Sasa napanic vip? Sasa siwez kupanic lazima muambiwe ukweli
 
Waleeni watoto wenu kikamanda gentleman 😄

Ova
kwenye malezi ya vijana wangu sinaga mzaha gentleman,

anakula mitama na makonzi ya maana sana akichelewa kwenda shamba, shule au kwenye ibada 🐒
 
😄 🤣

Ova
sure,
yaani sinaga masikhara hata kidogo gentleman,

yaani hata shemeji yangu au uncle wangu sijui alete upuuzi kwenye nilichoagiza na kuamua as head of family, akienda kinyume jioni sitamkuta, atakua kaishasepa kwao na hawez kurudi ispokua mimi nimeomba aje home kuna kazi ya nguvu ya kufanya au nasafiri kwa muda mrefu akae na dada yake,

but sitolarate nonsense hata sekunde moja 🐒
 
Hii nimeiona FB kupitia link imenileta hadi huku..
Nimejisikia vibaya sana Jamaa alivosimangwa kisa kuishi pale kwa miaka sita..

mleta mada hadi anaitoa huku manake ndani ya nafs anaumia jamaa akila chakula chake.

Sidhani kama jamaa kapenda hiyo hali n kwa kuwa amekosa Ramani.. Huyo ni mwanaume mwezio Ebu kaa nae mulize angependa kufanya kitu gani na umsapoti ila sio kumkandia hvi.. Huenda ufundi hapendi mulize anapenda nn..

Kuna sehem niliwah kukaa kwa shem miaka ya 2010-2016.. jamaa alikuwa anafoka sana na vyakula anaficha..
Jamaa alistafu Akapewa kiunuo mgongo kama 120M akaiingiza kwenye Kilimo cha mahindi Akavuna akapeleka kwa BILIONEA WA MKAKO aliyekuwa ananunua mahindi kwa Bei juu..Akatapeliwa akarud kulima mchicha na akawa ananiomba Hela ya mbolea ya kumwaga kwenye mchicha.

NB. Tuishi na wezentu vizuri kesho yetu n Fumbo...Mtu yyt anayezungumzia mambo ya Ownership (Nyumban kwangu,Chakula changu)..
Brother maisha yanabadilika
 
Kuna umasikini na fikra za kimasikini, hizi ni dalili za mawazo ya kimaskini

Kwanini watu wana mitazamo HASI kiasi hiki? Mtu kukaa kwako ni jambo moja lakini kuichukulia hali hiyo kwa mtazamo wa chuki na hasi ni jambo lingine. I

Zungumza naye kama mwenzio, mpe ushauri kwa upendo bila kuwa na mtazamo hasi

Maisha ni mafupi, lakini yamejaa utele mwingi ukichagua njia sahihi.

Chochote ufanyacho ACHANA NA CHUKI, kamwe haitakusaidia badala yake itakutafuna maisha yako yote
 
Unashindwaje mtumia shemeji yako kwa faida?
Hiyo ni "Cheap Labour" unashindwa itumia, job true true.
 
Back
Top Bottom