Sherehe ya Mwaka Mpya ni ya Kikristo, Waislamu tumeivamia tu bila kujua

Sherehe ya Mwaka Mpya ni ya Kikristo, Waislamu tumeivamia tu bila kujua

Labda nikutoe wasi wasi kuwa, sioni kama kuadhimisha mwaka mpya wa kidunia kukiwa na adhari yoyoye kwa waislam; Hii ni sawa tu na kuadhimisha siku ya kuzaliwa CHADEMA, CCM, Siku ya wafanyakazi nk.
Nafikiri Ujikite kwenye mambo ya msingi aliyo yaamrisha Mwenyezi Mungu badala ya kujichosha na hoja ndogo ndogo
Fundisha watu waache, Ushirikina, Wizi, uasharati, Kupunja kwenye Mizani, Kupindisha sheria nk
Wajikite zaidi kwenye Kusaidia wenye mahitaji kama mayatima na wasio na uwezo, Kutenda haki hasa kwa wenye nafasi hiyo nk
Tukubaliane kuwa upo ila muislam safi hapaswi kuusherehekea kwa sababu ya nature na waanzilishi wake
 
Tukubaliane kuwa upo ila muislam safi hapaswi kuusherehekea kwa sababu ya nature na waanzilishi wake
Tatizo kubwa la waislamu ni kutokuwa na Elimu ya Kutosha juu ya Dini yao
Utashangaa, Mtu anahangaika kubishania vitu vidogo vidogo vya Sunna
Huku haoni Uasharati, Ushirikina, Wizi nk kama ni makosa pengine ukubwa wake (dhambi zake) ni mara 100 kuliko ya suna anazo hangaika nazo..
 
Kuna swali niliuliza Yesu alivaa Kobazi au Raba ?

Kingine naona umekosea kujadiliana na Mimi, ukijadiliana na Mimi hakikisha unajua kulinganisha mambo na kutumia vizuri mifano. Mfano wa nguruwe na mchuzi wake ni kitu tofauti na suala hili. Sababu kutumia nguruwe hujatenzwa nguvu ila mwaka umeingia katika mfumo kutokana na mazingira tunayoishi wala siyo dhambi kutumia mwaka huu, ila kusherehekea ni jambo lisilo faa katika mwaka wa Kiislamu na usio wa kiislamu.
Hebu twende kwa Hoja.

Unasema siyo dhambi kutumia mwaka huu...

Kama mwaka unautumia, Dhambi iko wapi kuusherehekea?

Kusherehekea Kitu unachokitumia inakuwaje dhambi????
 
Nini maana kuelimika ? Kuingia kanisani na vimini au vimodo au kuamini utatu na kuungama kwa mwanadamu mwenzako ? Au kuelimika ni kuchanganyika jinsia mbili tofauti kwenye ibada ? Kuelimika ni nini hasa ?
Kumbe kuchanganya jinsia mbili ni kitu kibaya?

Huko Kwenye daladala/sokoni etc... nyie wavaa kobazi huwa hamchanganyi jinsia?
 
Labda nikutoe wasi wasi kuwa, sioni kama kuadhimisha mwaka mpya wa kidunia kukiwa na adhari yoyoye kwa waislam; Hii ni sawa tu na kuadhimisha siku ya kuzaliwa CHADEMA, CCM, Siku ya wafanyakazi nk.
Nafikiri Ujikite kwenye mambo ya msingi aliyo yaamrisha Mwenyezi Mungu badala ya kujichosha na hoja ndogo ndogo
Fundisha watu waache, Ushirikina, Wizi, uasharati, Kupunja kwenye Mizani, Kupindisha sheria nk
Wajikite zaidi kwenye Kusaidia wenye mahitaji kama mayatima na wasio na uwezo, Kutenda haki hasa kwa wenye nafasi hiyo nk
Sio mwaka wa kidunia.
Ni mwaka ulioanzishwa na Wakristo chini ya Papa Gregory XIII
 
Hebu twende kwa Hoja.

Unasema siyo dhambi kutumia mwaka huu...

Kama mwaka unautumia, Dhambi iko wapi kuusherehekea?

Kusherehekea Kitu unachokitumia inakuwaje dhambi????
Soma maelezo niliyo kupa yako wazi sana. Kwenu nyinyi kusherehekea mwaka mpya ni ibada au siyo ibada ? Kama ni ibada wapi ibada hii mmeipata ? Je Yesu alisherehekea kupinduka kwa mwaka ?

Kusherehekea ni dhambi sababu hakuna waio tutangulia wailifanya jambo hili si mitume wala si manabii. Mola wetu ameweka usiku na mchana ili watu wapate kuhesabu na kujua hesabu na idadi ya miaka na si kusherehekea.

Kwahiyo suala la sisi Waislamu kutumia mwaka usio wa Kiislamu upo nje ya uwezo wetu sababu tumekuta tayari jambo hilo lipo ila kwa nchi ambazo zinajitawala zenyewe yaani za Kiislamu unazingatiwa mwaka wa kiislamu. Kwahiyo hili linaingia katika mlango huo wala haliathiri dini maadamu tunajua mwaka wetu wa Kiislamu ukoje, siku inadalika saa ngapi haidhuru.
 
Unamshukuru Alah kuuona mwaka mpya wa Kikristo ulioanzishwa na Papa Gregory wa kanisa Katoliki.

Safi sana

Namshukuru Allah kwa mafanikio aliyonipa mwaka uliopita na sio namshuru Allah kwa kubadilika mwaka.-- soma vizuri pont yangu. Hata pia huwa namshukuru kwa mafanikio mwaka mpya wa kiisilamu unapoingia.
 
Sasa kama si asili katika Dini Si Mliache?

Kwa nini mnalitumia mpaka kwenye ratiba zenu za msikitini jambo ambalo si asili ya uislam?
Tunalitumia sababu lipo nje ya uwezo wetu kutokana na mfumo wa nchi jinsi ilivyo. Unaelekea ninacho kiongelea ?

Ndiyo maana katika kuliacha tunafanya yale ambayo yapo ndani ya uwezo na Hilo linaingia katika mlango wa dharura, na dharura hukadiriwa kwa makadirio yake.
 
Hii kalenda tunayotumia,Gregorian Calendar ilikuja baada ya Julian Calendar, zote zina uhusiano na Issa ndio maana utakuta maneno kama AD au BC yote yanamrefer Nabii Issa.

Sasa sisi Waislam imekuwaje hatulijui hili au kufuata mkumbo? au ndio dunia inaongozwa na mfumo Kristo?
Kalenda ni Kama elimu,Haina dini,haijalishi nani kagundua,hata Gregory hakusukumwa na ukiristo kutengeneza hiyo kalenda, Qur'an 17:12,10:6,29:14,2:260 inatambua kwamba tunatumia jua na mwezi kupima nyakati
 
Kumbe kuchanganya jinsia mbili ni kitu kibaya?

Huko Kwenye daladala/sokoni etc... nyie wavaa kobazi huwa hamchanganyi jinsia?
Uislamu umekamilika sana, unauliza maswali mepesi sana. Huko kwenye madaladala ni katika mlango wa dharura na mlango katika dini upo.

Lakini suala la kiibada si jambo la dharura, Yesu alifanya vipi ibada au mafundisho ya kufanya ibada zenu mmeyapata wapi ?

Lakini nashangaa wewe huoni ubaya wa kuchanganyika jinsia mbili tofauti akili zako ndogo sana kijana au hufikirii. Jamii imeharibika na kuwa hivi katika sababu kubwa ni kuruhusu michanganyiko hiyo.
 
Waislam wana kalenda yao hujawahi kusikia mwezi wa shaaban, rajab, ramadan

Au hujawahi kusikia mwaka mpya wa kichina

Wahindi,wayahudi wote wana kalenda zao kutokana na tamaduni zao

Lakini kalenda tunayotumia sasa ya kikristo ya papa Gregorian ndo ya kisasa na imemeza kalenda nyingine zote
Hii kalenda ya Gregory inahusiana nini na ukiristo!?
 
Ukitaka kuona jinsi hawa wafuasi wa mudy wana uwezo mdogo kiakili, nenda kwenye hiyo wanaita mihadhara yao. Mazungumzo yao ni kama uitishwe mkutano wa watoto
1998 jeshi la polisi liliua waislam mwembechai,baada ya padre kulalamika yesu anatikanwa,mihadhara hiyo kanisani na serikalini palikua hapalaliki hapaliki
 
Back
Top Bottom