Kama inavyojieleza
Mfano upo kwenye ndoa na mke wako lakini kutokana na masuala mbalimbali ya kimaisha hasa ajira mnaishi mbalimbali kwa muda mrefu na mwisho kuwa na migogoro ya hapa na pale
Baadae mwanamke anaamua kuolewa tena kimya kimya kule alipo bila wewe mume wake kumpa talaka au kuvunja ndoa kwa namna yoyote ile.
Je likitokea jambo kama hili hapo sheria inasemaje kuhusu ndoa hiyo.??
Hapa kuna maswali machache:
1. Je ndoa ilifungwa kimila au kiserikali? Kwa maana ya kwamba mna vyeti vya ndoa? Au Kama ni kimila, ulilipa mahari na kufuata hatua zote za kimila kuhalalisha ndoa yako?
2. Kuna sheria na moyo wa mtu, mpaka mwanamke ameamua kuolewa, tena bila wewe kujua, je unadhani hata kama sheria iko upande wako, vipi mahusiano halisi ya kimapenzi bado yatakuwepo?
Ningekuwa wewe, nisingetafuta kumrudisha. Utaumia mwenyewe maana sisi wanaume tuna kinyaa moja matata sana ukiachilia wivu. Yaani kumkaza mwanamke unayefahamu amewahi kukusaliti na kuishi unyumba na mtu mwingine.
Hapo unajitafutia jinai, ikitokea amekubali kurudi inaweza kutokea siku mkavurugana mmoja wenu akamuua mwenzake bure.
Wanawake wapo wengi mnoo, tafuta mwingine, endelea na maisha. Kwanza wewe ndo mwenye makosa, unawezaje kuishi mbali na mke muda mrefu kiasi cha kumfanya ajihisi upweke wakati mpo nchi moja?
Kama tulivyo na ugwadu, ndivyo wanawake nao pia wana ugwadu, alafu yao imechanganyika na uhitaji wa uhakika wa maisha. Ku feel kuwa safe and protected. Kuhudumiwa kihisia sasa mpaka hapo, jua umemkosea huyo mwanamke. Muache aendelee na maisha.