Sheria inasemaje kwa wabunge wanapohama vyama vyao kipindi hichi?

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
9,722
Reaction score
15,117
Ester Bulaya atimkia CCM, kuchukua fomu kugombea Bunda

Mbunge Kaboyoka: Nimekuja ACT Wazalendo na watu, tutaishangaza dunia Oktoba 2025.

Jee ubunge wao unakoma na posho na stahiki zake zote zinapotea?
 
Bunge limeishavunjwa. Maslahi yao wameishalipwa.
Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limehitimisha rasmi shughuli zake Juni 27, 2025 na Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye pia alilitunuku hotuba ya mwisho. Litavunjwa rasmi Agosti 03 litakapohitimisha ukomo wake kikatiba.
 
Mtu akiahama chama kwa nia ya kugombea uongozi akae kwenye chama husika alichohamia walau mwaka apimwe.Hata makazini kuna probation time bila kujali nafasi yako
 
Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limehitimisha rasmi shughuli zake Juni 27, 2025 na Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye pia alilitunuku hotuba ya mwisho. Litavunjwa rasmi Agosti 03 litakapohitimisha ukomo wake kikatiba.
Hiyo tarehe ndipo Gazeti la Serikali (The Government Gazette) ndipo litakapotangaza rasmi kuvunjwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni kama vile Rais anaweza kusaini leo tarehe 28/6/2025 Muswada kuwa Sheria, lakini Sheria hiyo itaanza kufanya kazi baada ya kutangazwa rasmi kwenye The Government Gazette!
Sijui umenielewa?
 
Kwa hivyo hivi sasa sio wabunge tena? Kama wabunge ni vyama gani?
 
Ndio. Sio wabunge tena. Hili suala la kiutaratibu na kulielewa tu. Angalia hotuba ya Mwamba Magufuli ya tarehe 16/6/2020 ya Kulivunja Bunge. Aliongea hivyo hivyo.
 
Wakasubiri kutunukiwa vyeo vingine baada ya uchaguzi, ubunge wawaachie wanachama waliokitumikia muda mrefu nao wagombee ubunge
 
Bunge limeishavunjwa. Maslahi yao wameishalipwa.
Bunge halijavunjwa kwa.mujibu wa Samia amesitisha shughuli za Bunge kuanzia Tarehe 26/06/2025 Ila Bunge litavunjwa Tarehe 03/08/2025 .
Yaani sijamuelewa huyu samia
 
Una uelewa wowote wa mambo ya kisheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
 
Back
Top Bottom