Sheria ya Ardhi inahitaji marekebisho?

Sheria ya Ardhi inahitaji marekebisho?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Inasemekana:

Kwa Sheria ya Tanzania, hakuna mtu anayeweza kumiliki ardhi. Anaweza kupangishwa tu, labda kwa kipindi cha miaka 99.

Kwa Sheria za Tanzania, Rais ndiye "mmiliki" wa ardhi yote nchini. Sijui itakuwaje pale Serikali itakapoitamani ardhi iliyokupangisha! Sijui itakupokonya!

Kwa Sheria za Tanzania, kilichopo chini ya ardhi ni mali ya Serikali. Siku ukigundua kuna almasi kwenye ardhi unayojitia kuimiliki huruhusiwi "kuyavuna" mpaka upate kibali cha mwenye ardhi ambaye ni Serikali. Cha kusikitisha, unaweza usipewe leseni hata kama utakuwa umekidhi vigezo.

Sijui kama hayo ni kweli!

Kama ni kweli, kwa nini muswada usipelekwe bungeni kubadilisha hizo Sheria kandamizi?
 
Unataka umiliki maji, madini, gesi na mafuta?

Haya mambo yanaweza yakaleta machafuko kwa sababu iwapo watu binafsi watamiliki madini wanaweza wakapata utajiri na kufadhili makundi tishio kwa usalama wa Taifa.
 
Rais siyo mmiliki Bali ni msimamizi (Trustee).
Ni kama mmiliki tu.

Kama sikosei, anaweza kubadilisha matumizi ya ardhi hata kama ilishamilikishwa kwa mtu mwingine.
 
What if muhusika akikataa:
1. Kiasi cha fidia kitakachopendekezwa na Serikali?

2. Kufidiwa kwa kuwa hayupo tayari kuliachia eneo lake?
Anaweza kukataa tathmini lakini siyo kuachia eneo.
Tathmini inapingwa mahakamani, kwa kuja na tathmini yako.
 
Ukiwa na Ardhi Omba Kibali cha Kumilki na yaliyo chini ya Ardhi....Ila nakubali hii Sheria Siyo rafiki Kwa wananchi,kwamba Rais wa JMT ndiyo Trustee.
 
Hii Sheria ni nzuri sana. Kwa nchi zetu. ikiruhisiwa mtu binafsi kumiliki ardhi masikini hawatakuwa na ardhi. Matajiri watainunua yote na kujimilikisha.
Maskini hata pata hata kipande pa kutemea mate.
Ni Sheria bora kabisa ibaki hivyo hivyo.
Waulizeni Wakenya.
 
Unataka umiliki maji, madini, gesi na mafuta?

Haya mambo yanaweza yakaleta machafuko kwa sababu iwapo watu binafsi watamiliki madini wanaweza wakapata utajiri na kufadhili makundi tishio kwa usalama wa Taifa.
Sikubaliani na wewe hata kidogo!

Unataka kuniambia watu kama akina Bakhressa, Mo Dewji, Rostam Aziz, na matajiri wengine waliopo Tanzania ni wafadhili wa ugaidi?

Matajiri wakubwa duniani kama akina Elon Musk, Mark Zuckerberg, Warren Buffett, Bill Gates, n.k., wameshawahi kutuhumiwa kufadhili ugaidi? Ukumbuke hao wana hela kuzidi Serikali ya Tanzania.

Hofu ya kuuogopa utajiri imechochewa na mtazamo wa kimaskini! Haina mashiko.
 
Hii sheria ni nzuri sana.

Tanzania ndio maana ni nchi ya amani kwa asilimia kubwa kuliko majirani zake.
 
Hii Sheria ni nzuri sana. Kwa nchi zetu. ikiruhisiwa mtu binafsi kumiliki ardhi masikini hawatakuwa na ardhi. Matajiri watainunua yote na kujimilikisha.
Maskini hata pata hata kipande pa kutemea mate.
Ni Sheria bora kabisa ibaki hivyo hivyo.
Waulizeni Wakenya.
1. Watainunua kutoka kwa nani? Kwani sasa hivi hawawezi kuinunua?

2. Watu gani wanamiliki ardhi kwemye maeneo mazuri (prime areas) nchini kama Mbezi & Masaki Dar, Njiro Arusha, Capri Point Mwanza, n.k.? Waliyapataje hayo maeneo ikiwa hawakuwa wazaliwa wa maeneo hayo?

3. Hiyo Sheria imewasaidiaje Wazaramo wa Dar Es Salaam? Inafahamika kwamba ndilo kabila wenyeji jijini Dar Es Salaam? Ni kweli wangali wanaishi katikati ya jiji? Naamini wawili watatu wenye maeneo mijini hawakosekani, na kama wapo, ni kwa sababu ya ubora wa Sheria au uwezo wa mifuko yao?
 
Rais sio mmiliki wa Ardhi bali ni Msimamizi/Trustee.tumemuaminisha yeye kumkabidhi ardhi kwa niaba ya wananchi.
Kuna sheria zetu ambazo zinaongoza masuala ya ardhi.
1.Sheria ya Ardhi no.4 [1999]
2.Sheria ya Ardhi ya Vijiji no. 4 [1999]

Pamoja na hizo kuna sheria nyingine zinaongoza mambo specific
Mfano kuna sheria ya upimaji n.k Kwa issue yako uliyoi-address (utwaaji)..kuna sheria inayoelekeza hayo mambo:
The land acquistion act, sheria ya utwaaji wa ardhi..
Hivyo Rais hawezi akaamka usingizi akasema anachukua ardhi ya mtu mpaka pale ijiridhishe kuwa inamasrahi mapana kwa jamii au taifa.
Lazima utafidiwa kulingana na thamani ya ardhi yako, usumbufu, maendelezo, mazao n.k..
Kwa ufupi Rais akitaka kuchukua ardhi yako..kuna utaratibu wa kisheria na utalipwa kiwango (Ambacho hakipaswi kukuweka well off or better off)..Hutauza bali utafidiwa.
 
Back
Top Bottom