Sheria ya goli ni kwamba ni lazima mpira uvuke mstari kwa asilimia 100

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Kwa maneno mengine ni kwamba ukichora mstari juu sambamba na ule wa chini halafu uchore mstari mwingine kutoka juu hadi chini perpendicular (nyuzi 90) hapo ulipo mpira, huo mstari wa kutoka juu kuja chini haupaswi kuugusa mpira! Kwa hiyo hata kama mpira umebaki.

Nje kwa milimita 1 Hilo dogo goli kwa kuwa Kuna asilimia kidogo za mpira Bado ziko nje!! Tukirudi kwenye sakata la goli analodai kufunga yanga dhidi ya mamelodi ni kwamba kigezo cha mpira kuvuka mstari kwa asilimia 100 hakikufikiwa! Ilikuwa ni maamuzi mepesi ya VAR yasiyohitaji refarii wa kati kusaidia.

Tukubali timu Bora ya Mamelodi ilistahili kusonga mbele! Underdogs yanga walijitahidi.
 
Sasa lile la Aziz Ki mpira ulivuka mstari kwa asilimia 200, ni halali si halali ?🐒
 
Kwahiyo wewe uliona wapi wamechora hiyo hiyo mistari ili kuonesha kuwa sio goli? Yaani tatu mzuka fc mnaweweseka.
 
Picha zote zinazotumiwa kusema goli ni halali hazijitoshelezi kbs kwa kuwa zinatokea upande mmoja..!

Zilihitajika picha zaidi za kamera inayochukua kutokea juu na kutokea nyuma ya goli.(kumbuka goli la Nzengeli dhidi ya IHEFU,picha kutokea angles tofauti ndio zilionyesha halikuwa bao halali)

Hivyo Refarii angeweza kuamua chochote..!

Hata hivyo, nasubiri mapovu kutokea upande ule kwa haya maoni..!
 
Tumepewa Al Ahly tunawajua wale yaani nusu fainali lazima utopolo mtapigwa nyingi sana na Mamelodi. Saivi mmesahau kujadiliana litimu lenu libovu imepigwa nje ndani na ndio timu pekee iliyofungwa kwa aggregate ya 3-0
 
Ndugu mbumbumbu umeandika goli Lili hitaji maamuzi ya muda mfupi kwakua mpira haukuingia kwa asilimia 100.

Kitu kilicho shangaza ni refa kutumia zaidi ya dk 5 kutoa maamuzi wakati wewe umeandika alichukua muda mfupi.
Hivi katika soccer dk 5 ni muda mfupi Tena ukiongozwa na VAR!!!

Ule mpira ulivuka mstari hazipungui sm 10, hakukua na shaka yoyote na goli, ukitumia libero kitu kinasoma ndani.
 
Uongoooo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tatizo unaendeshwa na mapenzi na sio uhalisia, unajua kuwa matukio yenye utata refarii anashauriwa na nani kwenda kwenye VAR? kasome kanuni za matumizi ya VAR, mwamuzi licha ya kushauriwa bado ndio mwenye maamuzi ya mwisho, sasa kama in ale walioko kwenye VAR, walimwambia kuwa lile sio goli, alikuwa na ulazima gani wa kwenda?
 
Wachezaji wetu ndiyo wa kuwalaumu

Walizubaa sana walitakiwa wamzonge refa sana hasa captain kumshinikiza aende kwenye var
 
Wachezaji wetu ndiyo wa kuwalaumu

Walizubaa sana walitakiwa wamzonge refa sana hasa captain kumshinikiza aende kwenye var
naona umecheka hapo kwa koment yangu, kulikon mkuu?, unalosema ni kwel kabisa captain alitakiwa kumshinikiza refa aende kwenye var, au hata angetoa timu nje kama alivofanyaga ronaldo, kama mbwai iwe mbwai tu, wooiiiiih
 
naona umecheka hapo kwa koment yangu, kulikon mkuu?, unalosema ni kwel kabisa captain alitakiwa kumshinikiza refa aende kwenye var, au hata angetoa timu nje kama alivofanyaga ronaldo, kama mbwai iwe mbwai tu, wooiiiiih
Hapana
Ila hilo swali lako ulilomuuliza huyo kolo limenifurahisha.

Nondo ameonesha udhaifu sana
Mimi naona tulitakuwa tuwe na captain kama diarra ingefaa sana


Tatizo anajua French tu
 
"MASHABIKI WA YANGA NI MAMBWA HAKUNA LOLOTE WANALOJUA KUHUSU KANDANDA ILA MUDA WOTE WANAZOMEA TU UTADHANI MANYANI" - DR LUC EYMAEL 2020
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…