Kindeena
JF-Expert Member
- Sep 27, 2017
- 11,462
- 21,124
Ni ukosefu wa wanasheria makini na waadilifu mkuu. Mwanasheria makini na muadilifu ni yule anayeweza kusimamia taaluma yake hadi mwisho, na unaposhauri ukaona ushauri wako haujasikilizwa, ili kulinda taaluma yako unajiuzulu.
Kama wewe ni mwanasheria, ukimshauri mteja wako jambo analotaka kufanya ni kinyume na sheria akaendelea kulifanya na ukamsaidia, utasema wewe ni mwanasheria muadilifu?
Nimesomea sheria na kufanya kazi Mahakamani, Firm na kwenye Jamii.
Ninaandika nilichokishuhudia toka kwenye Miswada, Bungeni, Serikalini na Mahakamani.