Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Kama muswada wa mambo ya mtandao na habari utapita kama ulivyo, Jamiiforums inaweza kufungiwa au kufanyiwa marekebisho makubwa.Tukae chonjo wanajamiiforums huenda ile slogan yetu ikatoweka.
 
Tatizo kuna watu wanaharibu sana jf kwa mada mbovu mbovu!
 
Mi nawaomba mods wawe makini kwa mada zinazoanzishwa hasa za kisiasa zisizo ushahidi wenye mashiko pia tujuzane forum nyingine tukifungiwa hapa tupate pa kukimbilia
 
Mi nawaomba mods wawe makini kwa mada zinazoanzishwa hasa za kisiasa zisizo ushahidi wenye mashiko pia tujuzane forum nyingine tukifungiwa hapa tupate pa kukimbilia

Mkuu huko pakukimbilia napo hakutabaki salama.
 
JF ikifungiwa basi tutakosa mengi, it has public interest.
Itakuwa "where dare to keep silence"
 
Sheria inasema atakayeandika habari za uongo na uzushi atapata adhabu............. Sasa mnaogopa nini kama mnaandika habari za kweli? Kumbe mlikuwa kazi maalum ya uzushi humu Jf kuchanganya watu? Raia mwema hana hofu na polisi. Kwa hii naunga mkono 100%
 
Vitu vingine avina maana hapa jf wanaingia watu wengi sana ina maana wakichangia jambo watu zaidi ya 100 mtawakamata wote kwa wakati mmoja mkawafungulie mashtaka?
Sheria zingine nikukandamizana lkn najua Mungu atasaidia iko siku kitaingia chama safi kuongoza taifa hili na sheria nyingi zitalekebishwa.
 
Ni ya kidikteta,inayorudisha taifa enzi za ujima,katili na inayopingana kabisa na haki ya kikatiba ya uhuru wa kutafuta na kupata habari
 
Kuna watu humu wanaifurahia hii sheria bila kujua kwamba, imetengenezwa mahsusi ili kuifungia kama siyo kuifuta kabisa Jamii Forums.

Huu ni mkakati maalum wa kuzuia uhuru wa kupata habari hasa ktk kuelekea uchaguzi mkuu.

Hatma ya hili suala liko mikononi mwa wabunge wazalendo na wapenda maendeleo.

JF live long.......
 
Wakuu tuzidi kuwa makini kwa hili ila kiukweli JF ni jukwaa ambalo lina watu wenye heshima japo kuna vijilugha vichafu vya hapa na pale. Humu kuna wataalam wa fani mbalimbali na wengi tumenufaika na mada zao. Cha msingi tuboreshe ili tuweze kuvuna zaidi
 

Kweli kiongozi
 
Ukandamizaji wa
haki za kila siku za binadamu
 
Ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo usikiri udaifu mpendwa
 

Ukifanya mambo ya kipumbavu tutasema bila kufinya macho kwamba wewe ni mpumbavu. Hivi ni tusi kubwa kiasi gani serikali kufyonza sh bilioni 300 na kudanganya wananchi. Hivi mwizi akiingia nyumbani kwako akapora hazina yako unamuitaje, rafiki au mheshimiwa. Mafisadi hawana hadhi ya kupata heshima yoyote, hao wanataka kufunga vinywa vya watu. Hao wanao umbuana na picha za uchi ni vichaa, hakuna nchi inayokosa vichaa. Unafikiri serikali imewa target hao, NO. Targeted guys are those who speak the truth, maana ukweli unawauma sana. Serikali ya ccm haitaki kuusikia ukweli ukizungumzwa na watu wa kawaida. Imagine jinsi serikali ya JK ilivyo vurunda, unategemea nini kama sio kufungia mitandao yenye mawazo chanya. Sitashangaa hizo blogs za matusi ndio zikaachiwa na kushamiri maana wakubwa wengi wako huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…