Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Kwa hiyo kama kuna viashiria vya ufisadi tusiseme mpaka vitokee? Mfano usiseme kuwa ikulu inahusija na ufisadi wa escrow mpaka mnikuru Gurumo atakapopasua jipu! Hivi sisi waTZ tuko sayari ipi?

Ukisema kuna viashiria vya ufisadi na ukavionesha hivyo viashiria sidhani kama utakuwa umevunja sheria kwa sababu tayari una ushahidi wa madai yako.

Mkuu kwani hiyo sheria wewe umeielewa vipi?
 
Wanaokubali waseme ndiyoo,,wasikubali wasema hapanaa. CCM banaa
 
Uchotwaji wa fedha za umma kiholela, mauaji ya albino, ujangili na utaifishaji wanyama pori na rasilimali zetu, unyanyasaji wa raia unaofanywa na polisi, ongezeko la kodi kwa walala hoi kwa 100% na msamaha wa kodi kwa wawekezaji toka nje, kupanda kwa gharama za simu, kushuka kwa mafuta na nauli kubaki palepale, n.k
vyote hivi havikuchukuliwa hatua ya dharura na serikali ila tu dharura inatolewa kuwalinda majoka wachache wanaotegemea kugombea nyadhifa mbalimbali nchini. Kweli! Mh jk ww sio mfano wa kuigwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Serikali za nchi za Ki-Afrika zinabana sana Media na mitandao kwa sababu zinaogopa kutolewa siri zao Mitandaoni. Serikali kama ni kweli ikiamuwa kupitisha hiyo sheria itakuwa Serikali inaogopa Ukweli wa Media na mitandao ya internet itakuwa Serikali haitendi haki na uhuru wa Mitandao na Media.
 
Tatizo february anafikiri tanzania ni ya mamake,yaani anaamua atakavyo,unamtumia mtoto wa sheikh yahya kuwadanganya watanzania eti rais lazima awe kijana tena awe na majina ya kikristo na kislamu , sasa sisi watanzania hatulitaki jitu kama hili, kwanza elimu yake yenyewe tia maji tia maji hana mchango wowote kwa watanzania zaidi ya kuwafanya waishi maisha magumu na MB 8 zake. namna hii anawaamsha hadi waliolala tunaanza kuzidisha mapenzi kwa lowasa hata kama ana skendo lakini atleast anamchango kwa mwananchi wa hali ya chini tofaut na february ambaye kazi yake kutafuta masikini kupiga nao picha na kuwahadaa watz wasio na uweredi. TANZANIA BILA FEBRUARY INAWEZEKANA
 
Mnakipenda sana chama cha mapinduzi,mnalalamika nini? Na bado-mkiambiwa chama hiki hakifai hamuelewi.2015 tubadilishe chama kingine,ccm imezeeka.wakati wake umekwisha.

POINT, mi ndo mana mtu akisema mabadiliko yanaweza kuletwa na wana ccm hua nacheka sana, kwa mtindo upi ccm imechoka jaman tukubali tukatae hiki chama kinahitaji kukaa upinzani mwaka huu ili kikajiulize kimekosea wapi na vipi kijirekebishe hawa watu wameshalewa madaraka jamani ndo mana kuna wanasiasa wazuri tu ndani ya ccm lakini sababu chama chenyewe kimeoza basi hata hawawachache wazuri wanaonekana nao hamna kitu, Januari Makamba katika hili japo unajiita mteteze wa umma haujatutendea haki!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mi sijui wanataka kuipeleka wapi nchi hii.Uhuru wa vyombo vya habari kubanwa kiasi hiki ni kumnyima mtanzania haki ya kupata habari za ndani ya nchi yake.Hata hivyo ni kumfanya mtanzania kupoteza hamu ya kusikiliza media za ndani au kusoma magazeti ya kitanzania kwani atajua fika hakuna habari za kuvutia na za kweli.
Hivi ninyi mnaotaka kupitisha mswaada huu hamjui kuwa baada ya kumaliza uongozi wenu mtakosa habari kama mnavyowanyia watanzania ambao hawapo madarakani?Haya mnayajua sana hebu angalieni kwa umakini jambo hilo
 
Mbona mawaziri wanadanganya bungeni hawashtakiwi?
 
Na kwa nini uwe muongo bora wakupige na kupelekwa selo jifunze kuleta habari za ukweli
Mtu wa kwanza kukumbwa na habari hii
Atakuwa
Yericko nyerere
Tusubiri mtasikia
 
Hizo kasoro waambiwe wabunge waelewa waziwasilishe marekebisho zilizokaa vizuri ziendelee.Zinazokiuka haki tuzipinge hata mahakamani.
 
Sheria hii n ishara ya anguko la ccm, zikipita na zikatekelezwa ipasavyo hasira za bubu wataziona!
 
FEBRUARY kaona jamiiforums itamfanya akose urais.kwa mawazo yake anadhani watanzania wanamfahamu kama wanavyomfahamu lowasa,kwa hili amebugi na ndio mwanzo wa kuwafanya watu wazidishe imani kwa lowasa. yeye akae na waganga wake washauriane njia nyingine lakini kwa hii tutamdharau sana,mtoto mdogo anakuwa na sheria za kikoloni utafikiri zee la miaka 152. makamba hatukupi urais ng'o hata ufanyeje
 
Ill motives behind the bill! If we will get the honest president come this October general election, he or she will have huge task of putting everything into proper way. Otherwise we are in trouble and turmoil is inevitable.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Siamini kama wabunge wote wana uelewa mpana juu ya matumizi ya mtandao. Naamini wapo wabunge wasiojua hata namna ya kufungua account hapa Jf, Fb, Twitter na ktk mitandao mingine, ila utashangaa nao watapiga kura ya ndio. Kaaazi kweli kweli:biggrin:
 
malengo ni mapana kuliko tunavyohisi Kafulila na Slaa na wapinzani wengine wanaopata taarifa za siri zenye kashfa kama za escrow watapatia wapi habari kama hizo wakati udhibiti wa mawasiliano unaelekea utaruhusu udukuzi katika vifaa vyote vya mawasiliano vya kielektronic...? Mtumishi gani wa serikali atakuwa na ubavu wa kuvujisha habari zinazoelekea kuwa za kashfa kwa serikali..?
 
wao waweke sheria zao,sisi tutazivunja tu,nasema barazani kweupee.ngoja niweke bajeti,nanunua laptop maalum,natengeneza kitambulisho maalum,naenda kusajili simcard malum,nanunua modem maalum,nafungua account maalum,na ID nyengine maalum kwa ajili ya kuwalipua mafisadi,na hivyo vitu sivitumii kwa matumizi mengine yoyote zaidi ya hiyo ID maalum,na wala sitaitumia hiyo ID nikiwa na vifaa vyangu vya kawaida.Mumenisikia nyie sijui TRA sijui TCRA sijui nini!mtatafuta kerubi hadi musinzie kwene keyboard,you'll meet with ghosts,na wewe mod wakikuomba IP yangu wape tu,wala usiumize kichwa,tena wape huku umebanwa na kicheko,nyambaf!wanatutafuta kidijitali,tutajificha kianalojia,tuone kipi ni more secure.
 
Back
Top Bottom