Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Tundu Lissu aliposema nchi inaongozwa na mafashisti wengi hawakumuelewa,,,,na bado muswada wa habari uko njiani.

Sasa mtaelewa alimaanisha nini.
 
Kwani ni lazima utukane, kukashifu na/au kudhalilisha mtu ili ujumbe ufike?
 
tunaweza jiunga ktk forum za nchi jiran ambazo serikal itakuwa haina mamlaka nazo mfano humu Jf kuna wakenya kibao

Sheria pendekezwa inasema ukifanya kosa kama wewe ni mtanzania mahakama ina mamlaka juu yako
 
Hivi hapo kwenye kifungu cha 16 neno sahihi lilipaswa kuwa ni mfumo wa computer au mfumo wa ki-electronic?

Na mimi sasa nimekaa kama kamati nyuma ya keyboard yangu nikitunga sheria(sheria kandamizi)
kupitia hapa JF.
Soma interpretation maana ya computer system nafkiri utaelewa wana maana gani
 
Mkuu Informer ilikuonyesha hapa hakuna dhamira njema sec;50
Huu ni utawala wa Imla.Haiwezekani mtu mmoja eti Mkurugenzi wa Mashitaka awe muamuzi wa mwisho na kusiwe na hata nafasi ya kukata rufaa.


Wapinzani wakishiriki katika kupitisha hili,nadhani nitajifikiria kama kunahaja ya kupiga kura hapo Oct.2015
Kama marekebisho ya msingi yatakataliwa wawaache wapitishe wenyewe wenye Nchi
(CCM)
maana na amini wako watu makini Bungeni watakaoleta maboreho muhimu na yakujenga ,lakini kwa sababu kuletwa kwa msada huu kiuharaka kuna nia ofu ndani yake yatakataliwa.





Suala jingine lenye kuleta mianya na matumizi mabaya ya utawala.Ni hili la Waziri mwenye dhamana kutengeneza Kanuni.
Kanuni hizi ifike mahali zipitie kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge na Kamati ya Katiba na Sheria na ijadiliwe na waipigie kura za wazi.
Ukumbuke kwamba mkurugenzi wa mashtaka anaingia pale ambapo wewe umeamua kwenda kukubali mbele yake kwamba umekubali kosa sasa rufaa ya nini wakati umemfuata mwenyewe ukasaini mwenyewe kwamba unakubaliana na kosa na adhabu mbele yake?
 
Last edited by a moderator:
Ndiko tulikofika? All Assad na Gadaf walifanya hivyo, lakini hali ya kibinadamu ni ngumu na ya hatari sana,

Uchina na Urusi walijaribu havyo lakini utandaridhi vimewashinda,

Sasa kwetu si watafunga kila wanayemhisi tu bila ushahidi?
Tahadhari kwako unaejifamya mtoto wa nyerere.
Cc mwanadiwani
 
sioni haja ya kua na muswada wenye kurasa nyingi wakati wangeweza kuweka maneno machache kua serikali haitaki wananchi tutumie internet basi sio kuuma uma maneno huku dhamira iko wazi




eti usi tume picha ya mtu Bila permission utampata wapi Messi umwombe permission

hii mijitu iliyitunga huu mswada haifai mbinguni wala duniani
Na wewe acha kutupeleka machaka yako umesoma wapi palipoandikwa hivyo
 
Kuna watu humu wanaifurahia hii sheria bila kujua kwamba, imetengenezwa mahsusi ili kuifungia kama siyo kuifuta kabisa Jamii Forums.

Huu ni mkakati maalum wa kuzuia uhuru wa kupata habari hasa ktk kuelekea uchaguzi mkuu.

Hatma ya hili suala liko mikononi mwa wabunge wazalendo na wapenda maendeleo.

JF live long.......

Sijaona sehemu ilipisema jamii forum itafungwa, ila tu wamiliki wamepewa obligation kadhaa, ambao wanapost humu mambo ya uongo huku wakijua ni ya uongo ndo shida ipo kwao.... Imagine mtu anakuzushia umefariki wewe unalichukuliaje hilo
 
Naona ni mkakati wa kudhibitiana kambi za Urais,siku mtu akipigwa chini akitaka kumwaga mboga sheria imfunge
 
Mimi naona watu wanaongelea mswada huu kwa kutouelewa kwa mfano, kusema waziri anapewa mamlaka ya kutengeneza makosa hii si sahihi bali anapewa mamlaka ya kutangaza miundombinu muhimu, swala la kula njama lipo hata kwenye penal code sasa hivi sasa mbona malalamiko sasahivi na sio tangu wakati huo, na swala la kufanya impesonation hauwezi kufanya kwenye mtu ambaye ha-exist. Ninashauri tuzisome na kuelewa...
 
Ngoja ni fute posts zangu zote JF...ninazoziona za hatarii.....Hawa maCCM wameamua, lkn hii itawafanya wapendwe? au ndio jibu la ile hali tete aliyosema JK kwamba nchi yetu inayo?!! ...CCM inakufa kwa kutapatapa sana itaumiza watu wengi mnoo!!
 
Jamani albino si binadamu? Na sheria ya mauaji si ipo? Sasa itengenezwe sheria gani nyingine?
Ni kweli unachokisema.Nakubaliana na wewe Foxbat.. Lakini kwa upande wangu naona tuongeze kitu cha ziada,cha dharura mahususi tu kuhakikisha hawa binadamu wenzetu nao wanaishi kwa amani at least kama wengine ambao hawana tatatizo la ngozi
 
Ngoja ni fute posts zangu zote JF...ninazoziona za hatarii.....Hawa maCCM wameamua, lkn hii itawafanya wapendwe? au ndio jibu la ile hali tete aliyosema JK kwamba nchi yetu inayo?!! ...CCM inakufa kwa kutapatapa sana itaumiza watu wengi mnoo!!

mkuu usimalize kibando chako bure kwenye taratibu za uendeshaji wa makosa ya jinai kuna kanuni inaitwa noellapoenasinilege,huwezi kushitakiwa kwa kose ulilotenda wakati unatenda halikuwa kosa
 
Sheria mbovu itakayolinda mafisadi na madudu wanayofanya yashindikane kuanikwa HADHARANI means to binds wanyonge wasifahamu ni nini kinaendelea ktk nchi yao hasa ualifu wao wa kifisadi,mikataba ya hovyo na madudu kem kem ya hovyo thanks tz HURU
 
Me nafikiri kabisa hatuwezi kufanya lolote kuzuia hizo sheria.. na kila nchi zina hizo sheria za kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii!

Jf ambacho wanatakiwa kujifunza au kuchukua tahadhari ni kuanza moderatio ya aina yake ambayo haitokuwa na huruma na mtu anaye vunja kanuni makusudi na wasitegemee tena watu mpaka wa report abuse kinacho takiwa ni kukakagua kila kinacho anzishwa kwenye majukwaa na kusiwe na huruma tena!

Kwa hali ilivyo ni lazima sheria za namna hii zije japo zinahitaji marekebisho lakini tusitegemee kwa ukuaji wa technology kusiwepo na sheria za namna hii!

Hakika mkuu, wakati tunalalamika kwa upande mmoja lakini pia upande wa pili ina maslahi. Hata humu JF baadhi ya watu wamechukulia kuwa ni sehemu ya kupost uzushi usio na maana bila kuwa vyanzo vya habari zao, watu wanaweka mada za kupotosha sana tu. Ni wakati sasa watu wawajibike kwa taarifa zao, kama una uhakika na unachoweka huna haja ya kuogopa!!!
 
Sasa ndo ndugu yangu ndio najiuliza hapa ni kitu gani kiongezwe kiweze kusaidia?
 
Mwaka jana mwezi wa 12 wabunge wa bunge la kenya walitwangana makonde bungeni kwa ajili ya sheria kama hii hii., baina ya wapinzani na wale wanaounga mkono serikali

Kimantiki mswada unafanana na ule wa kenya tofauti ni aina ya uwasilishwaji wake lakini malengo yake ni yale yale kudhibiti midomo isipaze sauti macho yasisome ya wapinzani na masikio yasisikie ya wapinzani.

...matumizi ya mtandao ni kama matumizi ya kisu ukitumia kwa ajili ya kukatia nyama ya ng'ombe ndio mahali pake lakini kukitumiya kwa mwanadamu sio mahali pake kifaa ni kile kile matumizi yake ndio yanaleta hukumu ya jinsi kilivyotumika..
 
Ni kweli unachokisema.Nakubaliana na wewe Foxbat.. Lakini kwa upande wangu naona tuongeze kitu cha ziada,cha dharura mahususi tu kuhakikisha hawa binadamu wenzetu nao wanaishi kwa amani at least kama wengine ambao hawana tatatizo la ngozi

Sasa ndo ndugu yangu ndio najiuliza hapa ni kitu gani kiongezwe kiweze kusaidia?
 
Back
Top Bottom