Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Tundu Lissu aliposema nchi inaongozwa na mafashisti wengi hawakumuelewa,,,,na bado muswada wa habari uko njiani.

Sasa mtaelewa alimaanisha nini.
 
Kwani ni lazima utukane, kukashifu na/au kudhalilisha mtu ili ujumbe ufike?
 
Ingetungwa sheria ya dharura ya kupambana na mauaji ya albino kwanza
.Hyo ndio dharura

Jamani albino si binadamu? Na sheria ya mauaji si ipo? Sasa itengenezwe sheria gani nyingine?
 
tunaweza jiunga ktk forum za nchi jiran ambazo serikal itakuwa haina mamlaka nazo mfano humu Jf kuna wakenya kibao

Sheria pendekezwa inasema ukifanya kosa kama wewe ni mtanzania mahakama ina mamlaka juu yako
 
Hivi hapo kwenye kifungu cha 16 neno sahihi lilipaswa kuwa ni mfumo wa computer au mfumo wa ki-electronic?

Na mimi sasa nimekaa kama kamati nyuma ya keyboard yangu nikitunga sheria(sheria kandamizi)
kupitia hapa JF.
Soma interpretation maana ya computer system nafkiri utaelewa wana maana gani
 
Ukumbuke kwamba mkurugenzi wa mashtaka anaingia pale ambapo wewe umeamua kwenda kukubali mbele yake kwamba umekubali kosa sasa rufaa ya nini wakati umemfuata mwenyewe ukasaini mwenyewe kwamba unakubaliana na kosa na adhabu mbele yake?
 
Last edited by a moderator:
Ndiko tulikofika? All Assad na Gadaf walifanya hivyo, lakini hali ya kibinadamu ni ngumu na ya hatari sana,

Uchina na Urusi walijaribu havyo lakini utandaridhi vimewashinda,

Sasa kwetu si watafunga kila wanayemhisi tu bila ushahidi?
Tahadhari kwako unaejifamya mtoto wa nyerere.
Cc mwanadiwani
 
Na wewe acha kutupeleka machaka yako umesoma wapi palipoandikwa hivyo
 

Sijaona sehemu ilipisema jamii forum itafungwa, ila tu wamiliki wamepewa obligation kadhaa, ambao wanapost humu mambo ya uongo huku wakijua ni ya uongo ndo shida ipo kwao.... Imagine mtu anakuzushia umefariki wewe unalichukuliaje hilo
 
Naona ni mkakati wa kudhibitiana kambi za Urais,siku mtu akipigwa chini akitaka kumwaga mboga sheria imfunge
 
Mimi naona watu wanaongelea mswada huu kwa kutouelewa kwa mfano, kusema waziri anapewa mamlaka ya kutengeneza makosa hii si sahihi bali anapewa mamlaka ya kutangaza miundombinu muhimu, swala la kula njama lipo hata kwenye penal code sasa hivi sasa mbona malalamiko sasahivi na sio tangu wakati huo, na swala la kufanya impesonation hauwezi kufanya kwenye mtu ambaye ha-exist. Ninashauri tuzisome na kuelewa...
 
Ngoja ni fute posts zangu zote JF...ninazoziona za hatarii.....Hawa maCCM wameamua, lkn hii itawafanya wapendwe? au ndio jibu la ile hali tete aliyosema JK kwamba nchi yetu inayo?!! ...CCM inakufa kwa kutapatapa sana itaumiza watu wengi mnoo!!
 
Jamani albino si binadamu? Na sheria ya mauaji si ipo? Sasa itengenezwe sheria gani nyingine?
Ni kweli unachokisema.Nakubaliana na wewe Foxbat.. Lakini kwa upande wangu naona tuongeze kitu cha ziada,cha dharura mahususi tu kuhakikisha hawa binadamu wenzetu nao wanaishi kwa amani at least kama wengine ambao hawana tatatizo la ngozi
 
Ngoja ni fute posts zangu zote JF...ninazoziona za hatarii.....Hawa maCCM wameamua, lkn hii itawafanya wapendwe? au ndio jibu la ile hali tete aliyosema JK kwamba nchi yetu inayo?!! ...CCM inakufa kwa kutapatapa sana itaumiza watu wengi mnoo!!

mkuu usimalize kibando chako bure kwenye taratibu za uendeshaji wa makosa ya jinai kuna kanuni inaitwa noellapoenasinilege,huwezi kushitakiwa kwa kose ulilotenda wakati unatenda halikuwa kosa
 
Sheria mbovu itakayolinda mafisadi na madudu wanayofanya yashindikane kuanikwa HADHARANI means to binds wanyonge wasifahamu ni nini kinaendelea ktk nchi yao hasa ualifu wao wa kifisadi,mikataba ya hovyo na madudu kem kem ya hovyo thanks tz HURU
 

Hakika mkuu, wakati tunalalamika kwa upande mmoja lakini pia upande wa pili ina maslahi. Hata humu JF baadhi ya watu wamechukulia kuwa ni sehemu ya kupost uzushi usio na maana bila kuwa vyanzo vya habari zao, watu wanaweka mada za kupotosha sana tu. Ni wakati sasa watu wawajibike kwa taarifa zao, kama una uhakika na unachoweka huna haja ya kuogopa!!!
 
Sasa ndo ndugu yangu ndio najiuliza hapa ni kitu gani kiongezwe kiweze kusaidia?
 
Mwaka jana mwezi wa 12 wabunge wa bunge la kenya walitwangana makonde bungeni kwa ajili ya sheria kama hii hii., baina ya wapinzani na wale wanaounga mkono serikali

Kimantiki mswada unafanana na ule wa kenya tofauti ni aina ya uwasilishwaji wake lakini malengo yake ni yale yale kudhibiti midomo isipaze sauti macho yasisome ya wapinzani na masikio yasisikie ya wapinzani.

...matumizi ya mtandao ni kama matumizi ya kisu ukitumia kwa ajili ya kukatia nyama ya ng'ombe ndio mahali pake lakini kukitumiya kwa mwanadamu sio mahali pake kifaa ni kile kile matumizi yake ndio yanaleta hukumu ya jinsi kilivyotumika..
 
Ni kweli unachokisema.Nakubaliana na wewe Foxbat.. Lakini kwa upande wangu naona tuongeze kitu cha ziada,cha dharura mahususi tu kuhakikisha hawa binadamu wenzetu nao wanaishi kwa amani at least kama wengine ambao hawana tatatizo la ngozi

Sasa ndo ndugu yangu ndio najiuliza hapa ni kitu gani kiongezwe kiweze kusaidia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…