Sheria ya Mashirika ya Dini kuomba msamaha wa kodi waagizapo vifaa ndio hasira ya TEC wanataka waingize vitu bure bila kodi

Haya tumekusikia tilalila tupeni sasa miili ya vijana wetu tukazike na kumaliza misiba wakati tunafakati somo lako jipya
 
Ukitaka kujua udikteta wa TEC fanya reseach. Mapadri 80% hawakubaliani na maamuzi yao.
Bado hujasema, utasema sana. Ni hivi, hakikisha unaweka ushahidi wa wapi kura 31m zimetokea. Tukiingia barabarani 912 uhakikishe na ushahidi wa ule upuuzi uliowafanya muue wananchi wengi vile. Tukienda ICC huko mtanyoosha maelezo.
 
Mpaka mseme.... kwa nini mmeua watu 30,000++, je polepole yuko wapi.. Mjibu kwanza hili...
 
Nakuona chinjachinja katika Ubora wako.
Roma ikisema imesema mwambieni mama yenu aache kuua watanganyika damu za watanganyika zitamlilia mpaka, endelea kusapoti chinjachinjafc.
 
Uchaguzi wa juzi katika jimbo la tandahimba mkoani mtwara matokeo yametangazwa na mkuu wa mkoa kanali Patrick sawala na tandahimba watu wameuana sana jumapili iliyofuata padri alihubiri Kuwa chanzo cha vurugu zile ni serikali
 
..wewe unaongelea kodi, vipi hospitali km Bugando unaweza pima thamani ya mchango wake toka imenzishwa na hiyo kodi unayosema vinalingana? msamaha wa kodi wanaoomba ni kwa ajili ya vitu gani..vya starehe au kusaidia wananchi?
Hakuna mwananchi yoyote maskini anayetibiwa bure katika mahospital yote ya taasisi zote za kidini ambayo yanakamua kodi zetu...Tena gharama za hapo Bugando hospital utasema uko India.Raia wengi masikini hawapati matibabu ya maana kwenye hizo hospital.
 
Mjinga asiyetaka kukubali ukweli ndio anaweza kuona hivi..hospital ya bugando haijaanza jana imekuwepo miaka na miaka na inafanya kile kile kama jana km leo na kesho..mzigo inaobeba serikali haiwezi kubeba, neno bure ni mtizamo, dawa ya sh. 10,000 ikitolewa kwa sh. 2,000 kwangu hiyo dawa ni bure sababu hizo 2,000 ni gharama za usafiri na mchango kwa watoa huduma.
 
Rudisheni maiti zetu tukazike
 
Niishie hapa tu, maana ni dhahiri kuwa hii takataka uliandika ukiwa unatooooo==!
 
Kwahiyo wako tayari kwa lolote ili wapenye kwenye uongozi wa juu wanchi, sio kwamba wanahurumia sana watanzania walio uawawa, wanasaka utawala kwa nguvu zote, ila nacho ona Raisi mkatoliki au Muislamu ulishapita nawakati tuangalie uandilifu na uwezo.
Kama ndivyo huyu aliyepo ana huo “uandilifu” na uwezo?
 

Kutetea hili la gharama za huduma za taasisi mbali mbali za kidini(Mahospitali) pamoja na kupata misamaha ya kodi mbali mbali plus ruzuku inaonesha ts either ni mnufaika wa moja kwa moja au umepofushwa na hisia zako za kidini...kwa taarifa kidogo tu kwako hizo dawa zote unazouziwa huko hospitalini kwa gharama ya shilingi 2000 kwa dose...Bei halisi ya outer box yenye vidonge 100 bei yake ni chini ya shilingi 1000...sasa kwa taasisi ambayo haina kodi na inapata ruzuku serikalini ya uendeshaji kwann wasiuze shilingi 500 kwa dose??...Wizi mtupu na tunajua hilo na uenda ujui unachotetea
 
Vichekesho!! RC ndiyo dhehebu linalojimudu kuliko yote nchi hii upande wa kiuchumi.

Issue ingekuwa hiyo ni viongozi wa dini zote wasingeshobokea wanasiasa ukizingatia BAKWATA walishachomoza hadi kwenye reports za CAG kwa kutumika kupitishia semi trailers halafu yakasajiriwa kwa majina ya watu.
 
Mkuu mbona ulikuwa fresh tu ,nini kimekuoelekea uamue kuwa kupe kibwege hivi?
 
Hivi unadhani Roman Catholic ni kama kabisa za Mwamposa eti?

Watu wanakufanya hela Dunia nzima then waje kulialia na Kodi ya gari , seriously?
 
Tuje kwenye vipimo kutoka katika hizo hospital zetu za taasisi mbali mbali za kidini unazotetea zinasaidia wananchi Wizi na dhulma tu wananchi bila kujali ni muumini wao au laa...hakuna mwananchi wa kawaida anaweza afford CT SCAN....bei ndogo kabisa ya ct scan haipungui 150k....
Hospital nyingi zinatumia low to mid range CT scan ambazo most of them ni refurb.
assuming wamenunua mpya...market price ni less than 200m,Life span yake ni 10 to 15 years...hata kama kila siku wakihudumia wagonjwa wawili kwa hizo machine,wagonjwa 60 kwa mwezi,wagonjwa 720 kwa mwaka mzima assuming imefanya kazi for only 10years ...itakuwa imehudumia wagonjwa 7200...wakati ilihitaji wagonjwa chini ya 1500 kurudisha gharama za kila kitu...Je unadhani kuna sababu ya kuwakosesha huduma hiyo muhimu katika matibabu ya kisasa Watanzania masikini iwapo lengo ni kutoa huduma na sio biashara??
 
..wewe unaongelea kodi, vipi hospitali km Bugando unaweza pima thamani ya mchango wake toka imenzishwa na hiyo kodi unayosema vinalingana? msamaha wa kodi wanaoomba ni kwa ajili ya vitu gani..vya starehe au kusaidia wananchi?
Achana na Mujahidina huyu
 
TEC haiagizi tende na nyama ya ngamia
 
Mmetoka kuua watu sana Mnapambana na dini na Mnataka kupandikiza udini ilo halitawezekana Na ndo dalili za Dola kuanguka Tupo tunaawaangalia Uzuri wa GenZ sio wa dini GenZ dini wapi na wapi mnataka kufanya watu wote wapumbavu never wajibikeni janja Janja za miaka hiyo haiwezi kuwasandia nendeni kwa wananchi wana adhabu yenu ni suala la mda tu Mmesababishia mauji ya watoto wadogo kisa kudai haki zao kikatiba Shame on you Mnateka, mnaua, ufisadi, rushwa unyonyaji dharau. Wanaopinga haya kwamba ndo wabaya sio? Nyie kweli mko dunia yenu Ila muuaji anapofiwa Ulia machozi halisi sio bandia
 
Nguvu gani huyo team fulani kwamba waweke huyo na Polepole nani ana nguvu kwenye chama na serikali ni unafiki tu tunajua sema twende tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…