Mkuu nadhani bado hujaelewa hoja yangu na kama umeielwa basi umeilewa nusu.
Kwanza, ndoa ni mkataba lakini sio mkataba wa kudumu na kumbuka kwamba kila aina ya ndoa (ndoa ya kimila, kikristo au kiislamu) ina masharti yake na namna ya kuivunja. Ninachojaribu kusema ni kwamba kuwepo na sheria itakayo harmonize ndoa zote ili kusiwe na mkwamo pindi mwanaume anashindwa kuishi na mke. Kwa kuwa mume ndiye atakuwa anasaini na ku renew mkataba, pindi mke akikengeuka hakuna haja ya kwenda mahakamani. Simply unasubiri mkataba (mfano wa miaka mitatu, mitano, etc) una expire kisha una terminate contract kwa kuto renew mkataba mpya. Huhitaji kupoteza muda na pesa kwenda mahakamani kujieleza au kupeleka mashahidi. Tupo pamoja?
Pili, sitaki ndoa zifike mahakamani.....mashataka yanapoteza muda na pesa.....nataka ndoa iishie mikononi mwa mume (anayesaiani mkataba). Hivi wachezaji wa mpira wasipoongezewa mkataba huwa wanakimbilia mahakamani? La hasha! Timu isipokuongezea mkataba unatafuta timu nyingine au unastaafu (ikiwa umri umeenda).
Tatu, nimetoa pendekezo hili kwa sababu sheria ya ndoa ya Tanzania haisemi ukomo wa ndoa ni kila baada ya miaka mingapi. Haisemi chochote kuhusu ukomo wa ndoa. Serikali itakapoanza kutumia sheria ya ndoa ya mkataba hapa nchini lazima itataja muda wa mkataba (mfano miaka mitatu. mitano, kumi, etc).