Sheria ya ndoa ifanyiwe marekebisho kuruhusu ndoa za mkataba

Ingawa unetumia lugha kali kidogo, ila uko sahihi,
Chanzo cha ndoa nyingi kuingia kwenye mafarakano ni kwasababu ya kumuasi Mungu na kuishi kiholela bila kufuata sheria ya ndoa iliyowekwa na Mungu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Mkuu mada hizi zimekuwa nyingi na zinachosha kweli kweli.
 
💯
 
Mikataba kwa ajiri ya nini sasa? Kama haujui unachokwenda kufanya katika ndoa ni vema ujifunze kwanza.

Ndio nyingi zinafeli kutokana na mseto changamoto za kitabia ambazo watu hutoka nazo makwao na kuzipeleka kwa mtu ambaye alimuahidi kuishi nae kwa amani na utulivu wakisaidiana kutafuta maisha.
 
Sasa Mkuu kuna mambo unachanganya.

Kwanza inatakiwa ujue kuwa ndoa zote zinasimamiwa na sheria ya ndoa, iwe ya kiislam, iwe ya kikristu au iwe ya kimila zote hizo zinasimamiwa na sheria ya ndoa.

Pili, ndoa ni mkataba ila ni mkataba ambao haujatoa sehemu ya kuuvunja kwenye mazingira hayo ndipo inatumika mahakama. Sasa kwanini mkataba wa ndoa usiseme wazi kuwa wahusika mume na mke wanaweza kuvunja mkataba wao pakitokea kutokuelewana au hata wakiridhiana wenyewe?.

Zipo sababu nyingi miongoni ni matunda ya ndoa ambapo kuna watoto na mali, hivi vitu sidhani kama umeviwaza. Naona sehemu kubwa unamuwaza mwanaume pekee

Endapo ikiwa hivyo unavyopendekeza basi madhara ni mengi zaidi na ugomvi utaongezeka gasa kwenye kulea watoto na kugawanywa kwa mali, ndoa zikiwa rahisi kuvunjwa basi jua ni udhaifu wa kisheria na utapeli wa kimapenzi ndipo utaposhika hatamu.

Kutaibuka watoto waliotelekezwa, kutaibuka nfoa za msimu zenye lengo la kuvuna mali (udangaji rasmi) kutaibuka na vurugu nyingi sana

Wazo lako ni zuri ila wazo lako halitatui changamoto zilizopo zaidi linaongeza changamoto.

Sheria bora inaangalia sio tu haki za walengwa bali haki ya jamii nzima.
 
WATU WANAOISHI BILA KUOANA WANAISHI VIZURI KULIKO HAWA WA KANISANI AU MSIKINI(TENA BORA HAWA)
NYAKATI ZETU HIZI KUOA NI RISK SANA
 
WATU WANAOISHI BILA KUOANA WANAISHI VIZURI KULIKO HAWA WA KANISANI AU MSIKINI(TENA BORA HAWA)
NYAKATI ZETU HIZI KUOA NI RISK SANA
Umeongea ukweli 100% mkuu. Nimeshuhudia ndoa nyingi watu wanaishi bila kuoana zinakuwa na amani sana; hazina hekaheka kama hizi ndoa za kikristo na kiislamu ambazo wanawake hudhani wamepata tiketi kudumu kuendeleza ngebe kwenye ndoa. Wanaudhi sana ujue hawa viumbe kutoka sayari isiyojulikana.
 
Kumbe hata wewe umeona mkuu? Ndoa nyingi zinavurugwa na wanawake hasa pale wanapokuwa na uhakika wa ndoa ya kudumu. Dawa yao ni ndoa za mikataba tu, hakuna namna nyingine. Hawa viumbe ni wasumbufu sana.
 
Unaokoteza tu mandiko ili kuhalalisha sheria mbovu ya ndoa iliyopo. Ni wapi Mungu aliwaonya au kuwalaani hao waliooa wanawake wengi ktk hayo maandiko ya biblia niliyokuwekea hapo?
Hoja nzuri…
 
Kufuatia kuongezeka matukio ya wanawake kukengeuka kwenye ndoa, nasisitiza serikali ipeleke bungeni muswada wa dharula kuruhusu ndoa za mikataba. Hakuna haja ya kuumizana kichwa na ndoa za kudumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…