High Vampire
JF-Expert Member
- Nov 17, 2012
- 2,915
- 2,134
Mkuu High Vampire,kwenye ndoa hakuna mali ya mtoto/watoto. Kuna aina mbili za mali: mali binafsi ya mwanandoa na mali ya pamoja ya wanandoa. Hivyobasi,ni busara kuepuka varangati juu ya mali kwa kuweka mali katika mifumo/aina hizo zinazotambulika kisheria.
umekaa na mwanamke miaka miwili bila kumlipia mahali baadae akafariki sheria itasemaje hapo
Mkuu sana Petro,je inawezekana kwa watu waliokuwa kwenye ndoa mmoja wao kudai mali fulani aliyoipata kama nyumba ni mali yake binafsi kama hakuingia mkataba huo na mwenzake kabla?
jf kisima cha maarifa. Asante mleta mada kwa mada nzuri.
je unaposema mali za pamoja/mali binafsi... ni nini kinahitajika au kinaprove kuwa hizi ni za pamoja au za binafsi? hasa kwa zile zilizochumwa baada ya ndoa.
Mali binafsi ndani ya ndoa haitanguliwi na mkataba. Hutanguliwa na taarifa kwa mwenza wako na namna ya upatikanaji wa mali husika. Kikubwa ni kuweka mambo yenu wazi kama wanandoa. Mali binafsi zinaruhusiwa katika ndoa Mkuu Masonjo
Mkuu sana jMali, kwanza Amri ya Talaka haibebi maelekezo mengineyo kama hayajaombwa kimahakama.Pili, mali binafsi huruhusiwa kwa wanandoa.Ni wajibu wako kutunza nyaraka za kuthibitisha kuwa mali fulani ni zako pekee.Kinyume na hapo,itahesabiwa kama ni mali ya ndoa/machumo na itagwanywa inavyopasa.
Kulingana na sheria hiyo tafsiri ya ndoa ni nini
Je waweza kukaa/ishi na mwanamke/mwanaume kwa muda gani itatafsirika kuwa ndoa?
Haya masuala ya void and voidable marriages yakoje?
Void marriage ni ndoa ambazo ni batili mfano, wanandoa kutofikia umri wa kuingia kwenye ndoa au ndoa za jinsia moja.
Voidable marriage ni ndoa ambazo zinatambulika kisheria ila mmoja kati ya wanandoa hao anaweza kuitengua ndoa mfano kukosa consent kipindi cha ndoa, magonjwa kama HIV/AIDS ama kushindwa kuconstumate.
Ngoja mkuu mwenye siredi apite, natumai atakupa na vifungu.
Good job mates!! Umeeleweka uzuri tu.
Void marriage ni ndoa ambazo ni batili mfano, wanandoa kutofikia umri wa kuingia kwenye ndoa au ndoa za jinsia moja.
Voidable marriage ni ndoa ambazo zinatambulika kisheria ila mmoja kati ya wanandoa hao anaweza kuitengua ndoa mfano kukosa consent kipindi cha ndoa, magonjwa kama HIV/AIDS ama kushindwa kuconstumate.
Ngoja mkuu mwenye siredi apite, natumai atakupa na vifungu.
Wakili kaka msomi mimi nina viswali vyangu kadhaa...
Je, hiyo sheria ya ndoa inazungumziaje mambo ya pre-nup na post-nup?
Je, hiyo sheria ya ndoa inaruhusu ubatilishwaji wa ndoa?
Kama inaruhusu, ni mazingira au hali gani ndo zaweza kusababisha ndoa kubatilishwa?
Na ni kwa baada ya muda gani, baada ya ndoa kufungwa, ndo inaweza kubatilishwa?
Mkuu Nyani Ngabu, asante kwa maswali yako. Kuhusu la kwanza,Sheria ya Ndoa,1971 haina utaratibu wa Makubaliano ya mgawanyo wa mali kabla au baada ya ndoa.Mgawanyo hufanywa kisheria Mahakamani baada ya kuvunjwa ka ndoa. Isipokuwa, kifungu cha 58 kinaruhusu Makubaliano baina ya wanandoa katika namna ya kupata,kutunza na kuzitumia mali zinazopatikana wakati wa ndoa.
Kuhusu la pili, ndoa hubatilishwa. Mambo kadhaa yanaweza kuifanya Mahakama,baada ya kupokea Maombi toka kwa mmoja wa wanandoa, kubatilisha ndoa. Kwanza,pale ambapo mmoja wa wanandoa hakuwa na umri wa kufunga ndoa na ridhaa ya wazazi haikutolewa kwa kipindi hicho. Pili, kama mwanandoa,wakati ndoa ikifungwa,alikuwa akishambuliwa na kichaa au kifafa.Tatu, kama mwanandoa anakataa kujamiiana kwa makusudi. Na kadhalika.Jisomee kifungu cha 39 cha Sheria ya Ndoa,1971.
Kuhusu swali la tatu, muda wa kubatilisha hutegemeana na sababu ya kuomba kubatilisha.Kwa mfano, kama sababu ni kuwa mwanandoa mmoja alikuwa hana umri wa kufunga ndoa na ridhaa ya wazazi haikuwepo,maombi ya kubatilishwa lazima yawe kabla ya mwanandoa huyo kutimiza umri wa miaka 18.Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 98 (1) (b) cha Sheria ya Ndoa