Mkuu
Nyani Ngabu, asante kwa maswali yako. Kuhusu la kwanza,Sheria ya Ndoa,1971 haina utaratibu wa Makubaliano ya mgawanyo wa mali kabla au baada ya ndoa.Mgawanyo hufanywa kisheria Mahakamani baada ya kuvunjwa ka ndoa. Isipokuwa, kifungu cha 58 kinaruhusu Makubaliano baina ya wanandoa katika namna ya kupata,kutunza na kuzitumia mali zinazopatikana wakati wa ndoa.
Kuhusu la pili, ndoa hubatilishwa. Mambo kadhaa yanaweza kuifanya Mahakama,baada ya kupokea Maombi toka kwa mmoja wa wanandoa, kubatilisha ndoa. Kwanza,pale ambapo mmoja wa wanandoa hakuwa na umri wa kufunga ndoa na ridhaa ya wazazi haikutolewa kwa kipindi hicho. Pili, kama mwanandoa,wakati ndoa ikifungwa,alikuwa akishambuliwa na kichaa au kifafa.Tatu, kama mwanandoa anakataa kujamiiana kwa makusudi. Na kadhalika.Jisomee kifungu cha 39 cha Sheria ya Ndoa,1971.
Kuhusu swali la tatu, muda wa kubatilisha hutegemeana na sababu ya kuomba kubatilisha.Kwa mfano, kama sababu ni kuwa mwanandoa mmoja alikuwa hana umri wa kufunga ndoa na ridhaa ya wazazi haikuwepo,maombi ya kubatilishwa lazima yawe kabla ya mwanandoa huyo kutimiza umri wa miaka 18.Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 98 (1) (b) cha Sheria ya Ndoa