Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Mkuu High Vampire,kwenye ndoa hakuna mali ya mtoto/watoto. Kuna aina mbili za mali: mali binafsi ya mwanandoa na mali ya pamoja ya wanandoa. Hivyobasi,ni busara kuepuka varangati juu ya mali kwa kuweka mali katika mifumo/aina hizo zinazotambulika kisheria.

nashukuru mkuu ila poa nije nkufate PM
 
Last edited by a moderator:
Mkuu sana Petro,je inawezekana kwa watu waliokuwa kwenye ndoa mmoja wao kudai mali fulani aliyoipata kama nyumba ni mali yake binafsi kama hakuingia mkataba huo na mwenzake kabla?
 
jf kisima cha maarifa. Asante mleta mada kwa mada nzuri.

je unaposema mali za pamoja/mali binafsi... ni nini kinahitajika au kinaprove kuwa hizi ni za pamoja au za binafsi? hasa kwa zile zilizochumwa baada ya ndoa.
 
Mkuu sana Petro,je inawezekana kwa watu waliokuwa kwenye ndoa mmoja wao kudai mali fulani aliyoipata kama nyumba ni mali yake binafsi kama hakuingia mkataba huo na mwenzake kabla?

Mali binafsi ndani ya ndoa haitanguliwi na mkataba. Hutanguliwa na taarifa kwa mwenza wako na namna ya upatikanaji wa mali husika. Kikubwa ni kuweka mambo yenu wazi kama wanandoa. Mali binafsi zinaruhusiwa katika ndoa Mkuu Masonjo
 
Last edited by a moderator:
jf kisima cha maarifa. Asante mleta mada kwa mada nzuri.

je unaposema mali za pamoja/mali binafsi... ni nini kinahitajika au kinaprove kuwa hizi ni za pamoja au za binafsi? hasa kwa zile zilizochumwa baada ya ndoa.

Kwanza, chanzo cha pesa zinazofanikisha kupatikana kwa mali husika.Pili, majina/jina linalojitokeza katika nyaraka za umiliki wa mali hizo. Tatu, makubaliano baina ya wanandoa juu ya aina gani ya mali ambazo wanandoa wanataka wazimiliki. Kimsingi, wanandoa wana nafasi kubwa ya kupanga mambo yao wenyewe. Hakuna haja ya kuwahusisha watu kwa kila kitu kihusucho ndoa-kwa mfano wa mali.
 
Mali binafsi ndani ya ndoa haitanguliwi na mkataba. Hutanguliwa na taarifa kwa mwenza wako na namna ya upatikanaji wa mali husika. Kikubwa ni kuweka mambo yenu wazi kama wanandoa. Mali binafsi zinaruhusiwa katika ndoa Mkuu Masonjo

Aksante sana mkuu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu sana jMali, kwanza Amri ya Talaka haibebi maelekezo mengineyo kama hayajaombwa kimahakama.Pili, mali binafsi huruhusiwa kwa wanandoa.Ni wajibu wako kutunza nyaraka za kuthibitisha kuwa mali fulani ni zako pekee.Kinyume na hapo,itahesabiwa kama ni mali ya ndoa/machumo na itagwanywa inavyopasa.

asante sana
 
Nipo kwenye ndoa mwaka wa tano,Mwanaume anaandika majina yake tu katika mali tulizochuma pamoja na kudai ivyo vitu ni vya watoto wake,je ni haki? hawez nidhulum siku moja?
 
Haya masuala ya void and voidable marriages yakoje?

Void marriage ni ndoa ambazo ni batili mfano, wanandoa kutofikia umri wa kuingia kwenye ndoa au ndoa za jinsia moja.
Voidable marriage ni ndoa ambazo zinatambulika kisheria ila mmoja kati ya wanandoa hao anaweza kuitengua ndoa mfano kukosa consent kipindi cha ndoa, magonjwa kama HIV/AIDS ama kushindwa kuconstumate.
Ngoja mkuu mwenye siredi apite, natumai atakupa na vifungu.
 
Good job mates!! Umeeleweka uzuri tu.
 
Kama wanandoa wanaishi mikoa au nchi tofauti lakini wameamua kutalikiana, baraza la kata linawezaje kuwasuluhisha wakati mmoja wao hata weza kuhudhuria vikao vya usuluhishi?

Endapo wanandoa hawajawahi kuishi pamoja mara baada ya kufunga ndoa na wala hawana mpango huo na ndoa haijawahi kuwa consummated kwa zaidi ya mwaka mmoja toka ndoa ifungwe, hii inaweza kuwa sababu ya kudai talaka?
 
Wakili kaka msomi mimi nina viswali vyangu kadhaa.

Je, hiyo sheria ya ndoa inazungumziaje mambo ya pre-nup na post-nup?

Je, hiyo sheria ya ndoa inaruhusu ubatilishwaji wa ndoa?

Kama inaruhusu, ni mazingira au hali gani ndo zaweza kusababisha ndoa kubatilishwa?

Na ni kwa baada ya muda gani, baada ya ndoa kufungwa, ndo inaweza kubatilishwa?
 
Void marriage ni ndoa ambazo ni batili mfano, wanandoa kutofikia umri wa kuingia kwenye ndoa au ndoa za jinsia moja.
Voidable marriage ni ndoa ambazo zinatambulika kisheria ila mmoja kati ya wanandoa hao anaweza kuitengua ndoa mfano kukosa consent kipindi cha ndoa, magonjwa kama HIV/AIDS ama kushindwa kuconstumate.
Ngoja mkuu mwenye siredi apite, natumai atakupa na vifungu.

Mkuu nameless girl,nakushukuru kwa kuendeleza darasa hili kwa wanajamii wenzetu. Kama ulivyosema, void na voidable hueleweka haraka hivyo ulivyosema. Void Ceremonies zinazungumziwa chini ya kifungu cha 38 cha Sheria ya Ndoa na Voidable Marriages zinazungumziwa chini ya kifungu cha 39 cha Sheria hiyo.

Kifungu cha 38 kinaorodhesha matukio/sababu ambazo hupelekea sherehe/hafla/shughuli fulani ambayo ilitazamwa kuwa ya ndoa kuwa batili. Mfano,mmoja wa wanandoa hao hakuwepo katika tukio lenyewe.Pia, aliyeifungisha hana mamlaka ya kufanya hivyo. Vilevile, wanandoa kuwa katika mahusiano yanayokatazwa (kaka na dada,baba na bintiye nk).

Voidable Marriage huwa halali hadi ibatilishwe. Ni kama mwanandoa kutokuwa na uwezo wa kujamiiana na mwenzake, mwanandoa kutokuwa na umri wa ndoa wakati ndoa ikifungwa n kadhalika. Voidable hubatilishwa na Mahakama baada ya Maombi Maalum kuwasilishwa.
 
Last edited by a moderator:
Wakili kaka msomi mimi nina viswali vyangu kadhaa...

Je, hiyo sheria ya ndoa inazungumziaje mambo ya pre-nup na post-nup?

Je, hiyo sheria ya ndoa inaruhusu ubatilishwaji wa ndoa?

Kama inaruhusu, ni mazingira au hali gani ndo zaweza kusababisha ndoa kubatilishwa?

Na ni kwa baada ya muda gani, baada ya ndoa kufungwa, ndo inaweza kubatilishwa?

Mkuu Nyani Ngabu, asante kwa maswali yako. Kuhusu la kwanza,Sheria ya Ndoa,1971 haina utaratibu wa Makubaliano ya mgawanyo wa mali kabla au baada ya ndoa. Mgawanyo hufanywa kisheria Mahakamani baada ya kuvunjwa ka ndoa. Isipokuwa, kifungu cha 58 kinaruhusu Makubaliano baina ya wanandoa katika namna ya kupata,kutunza na kuzitumia mali zinazopatikana wakati wa ndoa.

Kuhusu la pili, ndoa hubatilishwa. Mambo kadhaa yanaweza kuifanya Mahakama,baada ya kupokea Maombi toka kwa mmoja wa wanandoa, kubatilisha ndoa. Kwanza, pale ambapo mmoja wa wanandoa hakuwa na umri wa kufunga ndoa na ridhaa ya wazazi haikutolewa kwa kipindi hicho. Pili, kama mwanandoa,wakati ndoa ikifungwa,alikuwa akishambuliwa na kichaa au kifafa.Tatu, kama mwanandoa anakataa kujamiiana kwa makusudi. Na kadhalika. Jisomee kifungu cha 39 cha Sheria ya Ndoa,1971.

Kuhusu swali la tatu, muda wa kubatilisha hutegemeana na sababu ya kuomba kubatilisha.Kwa mfano, kama sababu ni kuwa mwanandoa mmoja alikuwa hana umri wa kufunga ndoa na ridhaa ya wazazi haikuwepo, maombi ya kubatilishwa lazima yawe kabla ya mwanandoa huyo kutimiza umri wa miaka 18.Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 98 (1) (b) cha Sheria ya Ndoa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nyani Ngabu, asante kwa maswali yako. Kuhusu la kwanza,Sheria ya Ndoa,1971 haina utaratibu wa Makubaliano ya mgawanyo wa mali kabla au baada ya ndoa.Mgawanyo hufanywa kisheria Mahakamani baada ya kuvunjwa ka ndoa. Isipokuwa, kifungu cha 58 kinaruhusu Makubaliano baina ya wanandoa katika namna ya kupata,kutunza na kuzitumia mali zinazopatikana wakati wa ndoa.

Kuhusu la pili, ndoa hubatilishwa. Mambo kadhaa yanaweza kuifanya Mahakama,baada ya kupokea Maombi toka kwa mmoja wa wanandoa, kubatilisha ndoa. Kwanza,pale ambapo mmoja wa wanandoa hakuwa na umri wa kufunga ndoa na ridhaa ya wazazi haikutolewa kwa kipindi hicho. Pili, kama mwanandoa,wakati ndoa ikifungwa,alikuwa akishambuliwa na kichaa au kifafa.Tatu, kama mwanandoa anakataa kujamiiana kwa makusudi. Na kadhalika.Jisomee kifungu cha 39 cha Sheria ya Ndoa,1971.

Kuhusu swali la tatu, muda wa kubatilisha hutegemeana na sababu ya kuomba kubatilisha.Kwa mfano, kama sababu ni kuwa mwanandoa mmoja alikuwa hana umri wa kufunga ndoa na ridhaa ya wazazi haikuwepo,maombi ya kubatilishwa lazima yawe kabla ya mwanandoa huyo kutimiza umri wa miaka 18.Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 98 (1) (b) cha Sheria ya Ndoa

Nashukuru kwa majibu yako. Lakini nina swali jingine kama hutajali, nalo ni: hivi kabla ya watu kufunga ndoa, huwa kuna utaratibu wa kuomba na kupewa 'marriage license' inayowapa hao wanandoa watarajiwa rukhsa na uhalali wa kufunga ndoa?

Nauliza tu hivyo kwa sababu kuna nchi zingine ambazo mtu huwezi tu kwenda kufunga ndoa halali bila kupata hiyo leseni ya ndoa.

Tanzania tunao huo utaratibu?
 
Kaka Petro E. Mselewa ...nimetengana na mwenzi wangu toka ndoa ya kiKristo sababu kubwa ni hatukuwa na furaha wala amani katika miaka yetu mi3 ya ndoa, na sasa ni miaka mi3 tangu tutengane (sio legal separation nikiwa na maana hatukutengana mahakani). Tuna mtoto mmoja wa miaka mi5 na katika miaka yote hiyo mi3 tuliyotengana nimekuwa nikimsupport yeye na mtoto fully. Juhudi za kutupatisha (ndugu na marifiki, si mabaraza) hazijafanikiwa, na hakuna dalili yoyote ya kurudiana. Sasa kimefika kipindi 'I need to move on', namaanisha tudivorce. Je, nahitaji kufuata procedure zote hizo kuanzia kwenye mabaraza kabla ya kwenda mahakamani? Je, nina nafasi ya kuwin custody ya mtoto (full au shared ili mradi niishi naye, ana miaka mi5)?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom