Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Kwa mfano mme anaoa mke mwingine kisiri,ilhali alifunga ndoa ya mke mmoja.Mke wa kwanza akigundua anaweza kwenda mahakamani kumshitaki mme ili amlipe fidia? i mean ma milioni ya pesa

Yes inawezekana, hilo ni kosa la madai kwa huku kwetu. Kwa wengine criminal case mfano waarabu.
 
Nina ndugu yangu ana matatizo sana na ndoa yake, naomba mawasiliano yako ili tuone utamsaidiaje kiushauri.
Nilitaka kutuma PM ila naona umekuwa banned.
 
aisherjs,

Kwanza kabisa unapaswa kufahamu kuwa ukomo wa ndoa hutokea endapo:-

  • Mwanandoa mmojawapo amefariki.
  • Talaka ambayo imetolewa na Mahakama pekee pale inapojiridhisha kwamba kuna sababu ya msingi kufanya hivyo.
Mahakama peke yake ndiyo ina mamlaka ya kutoa amri ya kutengana au talaka na sababu zinazopelekea au kuishawishi mahakama kuvunja ndoa ni pamoja na:-
  • Uzinzi kati ya wanandoa
  • Ukatili kati ya wanandoa au watoto wa ndoa
  • Dharau au kupuuza kulikokidhiri dhidi ya mwenzi
  • Kumtelekeza mwenzi kwa zaidi ya miaka mitatu
  • Pale mwenzi anapofungwa kifungo cha maisha au kwa kipindi kisicho pungua miaka miaka mitano
  • Ikiwa mwenzi ameugua ugonjwa wa akili na imedhibitishwa na daktari kwamba hakuna uwezekano wa kupona.
  • Kubadili dini baada ya ndoa kufungwa pale wanandoa wote walikuwa wakifuata imani ya dini moja.
Kuhusu swala la mgawanyo wa mali kwa wanandoa, mali yoyote ambayo imepatikana wakati wa uhai wa ndoa na kwa nguvu au mchango wa pamoja wa wanandoa.

Iwapo mali iliyopatikana na mwanandoa mmoja wapo kabla ya ndoa au kwa nguvu zake mwenyewe lakini imeboresha/imetunzwa na mwanandoa mwingine mali hiyo itatambulika kama mali ya ndoa.

Lakini kama kuna mali yoyote ambayo mwanandoa mmoja amempa mwanandoa mwenzake kama zawadi, mali hiyo itakuwa ya yule aliyepewa pekee.
 
You are very right. Hata katika kitabu cha malaki imeandikwa Mungu anachukia kuachana. ukiona unaachana tu ujue Mungu anachukia kitendo unachokifanya. na kama ukiachana basi usioe au kuolewa tena hadi mmoja wenu afariki kifo kiwatenganishe. bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILI
 
Kuna grounds za talaka lakin hiyo ya kujiamulia sio sheria labda kuna makubaliano Kati ya wanandoa Soo kama kuna Mali walizochuma wote watagawana lakin sio zile za mtu binafsi.
 
mke wangu alitoroka kuna sheria yoyote inayo niamuru kutenda tendo la ndoa naye maana kesi yetu ya talaka ipo mahakamani
 
Kutenda tendo la ndoa? Kama shauri lipo mahakamani usubiri uamuzi Wa talaka. Sheria haimlazimishi kukupa unyumba. Ingawa kutopewa unyumba yaweza kuwa sababu ya talaka.
 
mke wangu alitoroka kuna sheria yoyote inayo niamuru kutenda tendo la ndoa naye maana kesi yetu ya talaka ipo mahakamani
kama upo naye kwenye "separation" kisheria, ukimlazimisha utakuwa umembaka na unaweza kwenda jela miaka si chini ya 30. ila kama amekubali yeye mwenyewe kwamba umfanye, its not a problem sir. separation kisheria huwa inatolewa ili wanandoa waliokuwa wamekorofishana wapunguze hasira (wacool temper). hiyo inakuwa miaka 3. kama amri ya separation kama hiyo imetolewa, usithubutu kumlazimisha, anakuwa ni mwanamke sawa tu na wengine ambao haujawaoa.
 
Sasa Mke Wangu Ananilazmisha Kutenda Tendo Paspo Ridhaa Yangu Na Amefungua Kesi Ya Kumtelekeza Kisa Simpi Unyumba Lakini Mahitaji Yote Nampa Huku Kes Yetu Ya Talaka Ipo Mahakamani
 
mwombe tu mungu,muweze kurudiana na mwenzio muendeleze familia neno talaka si zuri kimaisha
 
Habari wana forum
Naombeni mnisaidie kisheria ukitaka kumwacha Mke inakubidi umfanyie nini na nini au ni utaratibu upi unatumika kisheria na sio kidini
Aksanteni
 
Habari wana forum naombeni mnisaidie kisheria ukitaka kumwacha Mke inakubidi umfanyie NN na NN au ni utaratibu upi unatumika kisheria na sio ki dini Aksanteni

Lakini pia ungeweza kuomba ushauri wa namna ya kutoachana (kuboresha mahusiano yenu) ili msuluhishwe mkalea watoto pamoja kama mnao, hii itawaondolea watoto wenu maisha ya upweke
 
Nenda kwa wazee kwanza ukapate ushauri nasaha ndiyo urudi humu baada ya miezi 6 ili tukushauri vizuri
 
Kama ni MUNGU wa kweli ndiye aliyewaunganisha, nakushauri umshukuru MUNGU huyo na kumtukuza. Kwani, MUNGU ni MWEMA na tendo la kukuunganisha na kuwa na Mke mwema ni UPENDO MKUU.

Kama wewe ni wa upande mwingine, yaani wa giza, basi pole sana. Huko kwa wenye kutawaliwa na dhambi pia tamaaa za mwili isiyo kuwa na kibali toka kwa BWANA MUNGU tunda lake ni mauti " mshahara wa dhambi ni mauti"
 
Back
Top Bottom