Akili Unazo!
JF-Expert Member
- Feb 18, 2009
- 3,930
- 4,912
Kama mtu na mume wake wameshindwana, wanafanyaje ili kuachana kisheria bila kujali sheria ya dini?
Mfano kama inawezekana kukubalina kwamba "tunaachana", je wafanye nini ili kutarikiana na kila mmoja kubaki huru kisheria?
Je, inaweza kuchukua mda gani mahamani mpaka divorce ikawa final?Ili mahakama ivunje ndoa lazima mmepitia baraza la usuluhishi la ndoa (marriage conciliation board) ikashindikana kusuluhisha ndoa..kutoka kwenye baraza la usuluhishi mtapewa certificate kwamba usuluhishi umefeli kwahyo muende mahamakani.
Mahakama ktk kuvunja ndoa inakuwa inaongozwa na sheria ya ndoa ya Mwaka 1973 japo kuna revised edition ya 2002 ambayo inasema ndoa mpk ivunjwe n lazima iwe imefikia hatua ambayo haiwezi kurekebishika(the marriage has broken down irreperably) kumaanisha mmeenda usuluhishi Wa bodi imeshndkana na mnaweza pewa separation period Kwa muda almost miaka 2 muangalie km mtaweza kusuluhisha. Vyote vikishindikana basi mtafile petition for divorce itasikilizwa then ndoa itavunjwa na kubaki kuangalia mambo mengine kama division of matrimonial asset and custody of the children yani mgawanyo Wa mali na matunzo ya watoto kama wapo.
Bora umetambua kuwa aliepo ni shetani, sasa nasema bora malaika nisiemjuaMkuu nakushauri usivunje ndoa kisa mmeshindwana, ndoa yahitaji uvumilivu na kujuana tabia. Labda kama baada ya kuvunja hutaoa/hutaolewa tena hapo sawa. Ila kama unatarajia kuoa/kuolewa tena vumilia. Namalizia kwa kuwanukuu wahenga HERI SHETANI UNAYEMJUA KULIKO MALAIKA USIYEMFAHAMU. Duniani hakuna aliyekamilika kila mtu ana mapungufu yake.
mzee vipi kwa walio kwapuana na kuanza maisha bila ndoa kanisani wakiachana na kupata wenza wengine huko wakafunga ndoa bado ni wazinifu tu?Mathayo 19:9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
Ha ha ha ha mkuu we nomaBora umetambua kuwa aliepo ni shetani, sasa nasema bora malaika nisiemjua
Siyo kila kinachoitwa ndoa kina baraka na kibali cha Mungu. Tunazoita ndoa nyingi ni machukizo mbele za Mungu,unakuta zimefungwa kibatili,kwa kufoji na kudanganya mambo,nyingi zinafungwa kwa mtazamo wa sherehe na sifa ya kuoa ama kuolewa siyo dhana ya umilele.Jamani si mkumbushane upendo wa awali,msivunje ndoa nyie Mungu hapendi taraka.
Kama msing ulikosewa ni kutubu tu na kuanza upyaS
Siyo kila kinachoitwa ndoa kina baraka na kibali cha Mungu. Tunazoita ndoa nyingi ni machukizo mbele za Mungu,unakuta zimefungwa kibatili,kwa kufoji na kudanganya mambo,nyingi zinafungwa kwa mtazamo wa sherehe na sifa ya kuoa ama kuolewa siyo dhana ya umilele.
Watu wanajiita wapo na ndoa lkn wanaishi kila mmoja na hamsini zake,hawafuati taratibu anazoagiza Mungu,nyingi ni ndoa vyeti,wengi wanafunga harusi si ndoa.
Km hamfuati misingi na hamkufuata misingi aagizayo Mungu hiyo ni chukizo,hivo siyo kila ndoa uihusianishe na maamrisho ya Mungu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, tafadhali hariri swali lako ili nilielewe na kulijibuKwa nn sheria na malezi ya mtoto hutoa hualari wa mtoto baada ya mzazi kuto mazazi kutojili baada ya miezi 24 na ustawi wa jamii hawakubali kiualaka kwenda kupima vina sana msaada plz
Sent using Jamii Forums mobile app