Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Kama mtu na mume wake wameshindwana, wanafanyaje ili kuachana kisheria bila kujali sheria ya dini?
Mfano kama inawezekana kukubalina kwamba "tunaachana", je wafanye nini ili kutarikiana na kila mmoja kubaki huru kisheria?

Private Inestigator anataka kuvunja Ndoa Yake. hahahahaha
 
Ili mahakama ivunje ndoa lazima mmepitia baraza la usuluhishi la ndoa (marriage conciliation board) ikashindikana kusuluhisha ndoa..kutoka kwenye baraza la usuluhishi mtapewa certificate kwamba usuluhishi umefeli kwahyo muende mahamakani.
Mahakama ktk kuvunja ndoa inakuwa inaongozwa na sheria ya ndoa ya Mwaka 1973 japo kuna revised edition ya 2002 ambayo inasema ndoa mpk ivunjwe n lazima iwe imefikia hatua ambayo haiwezi kurekebishika(the marriage has broken down irreperably) kumaanisha mmeenda usuluhishi Wa bodi imeshndkana na mnaweza pewa separation period Kwa muda almost miaka 2 muangalie km mtaweza kusuluhisha. Vyote vikishindikana basi mtafile petition for divorce itasikilizwa then ndoa itavunjwa na kubaki kuangalia mambo mengine kama division of matrimonial asset and custody of the children yani mgawanyo Wa mali na matunzo ya watoto kama wapo.
Je, inaweza kuchukua mda gani mahamani mpaka divorce ikawa final?
 
Vipi kuhusu kuvunja ndoa ambayo haikufungwa na walikwapuana tu,na ukatoa mahari na mmeisi miaka zaid ya mitano.
 
Pamoja na sheria za kuvunja ndoa kuwepo sishauri wana ndoa kuvunja ndoa zao.Ndoa zinahitaji uvumilivu sana.Kuna dhehebu fulani wao wanasema ndoa ni nyumba yenye mlango mmoja tu wa kuingilia,hakuna mlango wa kutoka nje!
 
Jamani si mkumbushane upendo wa awali,msivunje ndoa nyie Mungu hapendi taraka.
 
Watauana kwa ngoma bure. Michepuko imezidi. Bora kila mmoja kivyakevyake.
 
Mkuu nakushauri usivunje ndoa kisa mmeshindwana, ndoa yahitaji uvumilivu na kujuana tabia. Labda kama baada ya kuvunja hutaoa/hutaolewa tena hapo sawa. Ila kama unatarajia kuoa/kuolewa tena vumilia. Namalizia kwa kuwanukuu wahenga HERI SHETANI UNAYEMJUA KULIKO MALAIKA USIYEMFAHAMU. Duniani hakuna aliyekamilika kila mtu ana mapungufu yake.
 
Mkuu nakushauri usivunje ndoa kisa mmeshindwana, ndoa yahitaji uvumilivu na kujuana tabia. Labda kama baada ya kuvunja hutaoa/hutaolewa tena hapo sawa. Ila kama unatarajia kuoa/kuolewa tena vumilia. Namalizia kwa kuwanukuu wahenga HERI SHETANI UNAYEMJUA KULIKO MALAIKA USIYEMFAHAMU. Duniani hakuna aliyekamilika kila mtu ana mapungufu yake.
Bora umetambua kuwa aliepo ni shetani, sasa nasema bora malaika nisiemjua
 
Kazi ya kutoa ushauri ni ngum.Unashauri watu ambao hujui walianzaje mahusiano,, wengine labda aliozeshwa mwanafunzi baada ya kumpa mimba, wengine mwanamke aling'ang'ania ndani sasa ndo kamjua vizuri tabia, mfano kunajamaa alienda kufanya kazi sehem akakutana na mdada akawanae geto kwa miez kama sita gafla wa kwao bint wakamtokea wakaelewana na mahal, jamaa ikabidi aoe, yule dada akawa anamdanganya hana mtoto, siku moja yule dada kaenda kwao akajisahau akaja na kadi ya clinic ya mwanae mkubwa,na alikuwa na watoto wawili nyumbani, ha kumbe alikuwa mkubwa miaka sita kumzidi jamaa, kuanzia hapo ndoa hiyo ikayumba na tayar walikuwa na mtoto mmoja, utaishauri vipi hii ndoa.
 
Mathayo 19:9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
 
Mathayo 19:9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
mzee vipi kwa walio kwapuana na kuanza maisha bila ndoa kanisani wakiachana na kupata wenza wengine huko wakafunga ndoa bado ni wazinifu tu?
 
Nitoe shukrani zangu kwako mtaalam kwa msaada unaotupatia. Nami pia ni mhanga wa matatizo ya ndoa na nahitaji msaada wa haraka. tatizo langu limeanza tangu nimeanza kuishi na mke wangu (sipendi kumwita hivyo) yapata miaka karibu 9 hivi iliyopita japo miaka ya ndoa ni 6. Kwa ufupi mke wangu huyu sipo nae kwa sasa ameshaondoka nyumbani baada ya mvurugano aliousababisha mwenyewe. Kama nilivyosema matatizo yalianza tangu tuanze kuishi pamoja na vyanzo ni wivu wa kupindukia pamoja na kutokuwa na heshima na utii kwangu kama mumewe. Japo niliyaona haya lakini nakiri kukosea kufunga naye ndoa kwa sababu nilimpenda sna na niliamini nitaweza kumbadilisha kwa namna yoyote na pia kwa wakati huo na hata sasa sikuweza kuishi peke yangu kutokana na changamoto za kiafya nilizonazo. Wivu aliokuwa nao ulinikosesha amani kwani nilikuwa nikitoka japo mara chache, lazima nikirudi inakuwa kesi na anataka nimuambie kila sehemu niliyopita. Narudia tena hili lilininyima raha mpaka kutamani nisitoke. Matatizo haya yaliendelea kwa miaka mingi lakini nikiwa mwaminifu kwa %100 kwani kwa muda wote huo sikuwahi hata kumtongoza mwanamke yeyote na hata yeye nilishamwambia tena mbele ya baba yake mzazi wakati tunasuluhishwa. Sasa nasikitika balaa limekuja hivi karibuni ilikuwa mei mosi baada ya kupewa maneno na staff mwenzangu wa kike ambaye tayari nilimuonya kuhusiana na urafiki wao kutokana na rafikiye kumletea mambo ya ofisini tena ya uongo na kutugombanisha. Kilichotokea, alimtuma rafikiye kuchunguza mahusiano na wenzangu kazini akaletewa habari kuwa kuna mwal huwa ananiletea vitafunwa na kunitengea chai pamoja na kuwa nae karibu sana jambo ambalo ni uongo, mwal aliyehusishwa ni katibu wangu nami ni m/kiti wa mahusiano kazini na hili alilijua. hili alilisema mbele ya baba yake pamoja na kumtaja mwl huyo. Kosa lake kubwa zaidi ni kuamini hayo na nasema wazi alinitukana na kuniambia kila aina ya uchafu mpaka kufikia kuniambia nimeathirika. Namshukuru sna Mungu kwa kunipa uvumilivu kwa kutomgusa japo nilikuwa na hasira sana. Na katika maneno aliyokuwa anayatoa alisema anaondoka mi si mumewe tena. Kutokana na mfululizo wa mambo kama haya nami nilishachoka na niliona wazi siwezi kuishi nae zaidi, niliona wazi madhara makubwa mbeleni na hasa usalama wa pande zote. Niliamua hivyo japo nilitegemea akiondoka atajifunza mengi na nikijiridhisha kubadilika ningempokea tena kwani tayari tuna watoto 2. Nilifikisha tatizo langu ofisi ya kata baada ya m/kiti wa kitongoji kushindwa kusaidia kwa wakati, afisa mtendaji alinisihi sna nivumilie aandae baraza lake la usuluhishi waongee nae asipobadilika ndio nichukue maamuzi yangu. Nilikubali tukapanga mazungumzo yawe tar 27. 6 mwaka huu na nikampa taarifa. Kabla ya siku husika alinigeuka na kukataa mazungumzo akitoa sababu zisizo na maana na kabla ya siku tuliyokubaliana aliondoka na watoto na kuchukua vitu vya ndani mpaka kitanda japo nilisikia ameweka kwa jirani na yeye kwenda Arusha na watoto. Sasa kwa alichokifanya ndio kimenipa hasira zaidi sababu ameondoka na mtoto mkubwa ambaye alikuwa akisoma chekechea. Kwa alichofanya nimeamua kuachana naye kabisa kwa sababu nimegundua siwezi kumbadili na hataki kusikiliza hata wazazi wake. Alishaaswa sna kuwa mume halindwi hivyo lakini alianza kuwashutumu wazazi kuwa wananipendelea na aliwahi kuniambia kuwa tuliyoongea kwenye kikao na baba mkwe(upatanishi) ni yetu kwamba hayamhusu. Naomba ushauri wa kisheria nifanyaje niwe huru kuangalia mambo mengine kwa manufaa ya watoto, hapa nimefupisha sna. Nawasilisha kwa msaada.





Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
Jamani si mkumbushane upendo wa awali,msivunje ndoa nyie Mungu hapendi taraka.
Siyo kila kinachoitwa ndoa kina baraka na kibali cha Mungu. Tunazoita ndoa nyingi ni machukizo mbele za Mungu,unakuta zimefungwa kibatili,kwa kufoji na kudanganya mambo,nyingi zinafungwa kwa mtazamo wa sherehe na sifa ya kuoa ama kuolewa siyo dhana ya umilele.

Watu wanajiita wapo na ndoa lkn wanaishi kila mmoja na hamsini zake,hawafuati taratibu anazoagiza Mungu,nyingi ni ndoa vyeti,wengi wanafunga harusi si ndoa.

Km hamfuati misingi na hamkufuata misingi aagizayo Mungu hiyo ni chukizo,hivo siyo kila ndoa uihusianishe na maamrisho ya Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
S
Siyo kila kinachoitwa ndoa kina baraka na kibali cha Mungu. Tunazoita ndoa nyingi ni machukizo mbele za Mungu,unakuta zimefungwa kibatili,kwa kufoji na kudanganya mambo,nyingi zinafungwa kwa mtazamo wa sherehe na sifa ya kuoa ama kuolewa siyo dhana ya umilele.

Watu wanajiita wapo na ndoa lkn wanaishi kila mmoja na hamsini zake,hawafuati taratibu anazoagiza Mungu,nyingi ni ndoa vyeti,wengi wanafunga harusi si ndoa.

Km hamfuati misingi na hamkufuata misingi aagizayo Mungu hiyo ni chukizo,hivo siyo kila ndoa uihusianishe na maamrisho ya Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama msing ulikosewa ni kutubu tu na kuanza upya
 
Kwa nn sheria na malezi ya mtoto hutoa hualari wa mtoto baada ya mzazi kuto mazazi kutojili baada ya miezi 24 na ustawi wa jamii hawakubali kiualaka kwenda kupima vina sana msaada plz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba uliza mume alikopa nyumba tukiwa pamoja na alianza kulipa akisema hii nyumba yetu. pesa nyingi italipa deni tuvumilie maisha. je akitoa talaka mke anahaki yake hapo?
 
Back
Top Bottom