Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Mkuu, jisomee tena Sheria ya Ndoa na taratibu zake. Waislamu wanayo Mabaraza ya usuluhishi. Na ni lazima kuanzia huko kabla ya kwenda Mahakamani.Sema kwa upande wa ndoa ya Kiislam, Sheria itakayotumika mahakamani ni Sheria ya Kiislam. Kwao hakuna kupitia mabaraza ya usuluhishi.
Nilimaanisha Marriage Reconcilliatory Board. Sikuwa nafahamu km inahusisha na Mabaraza ya KiislamMkuu, jisomee tena Sheria ya Ndoa na taratibu zake. Waislamu wanayo Mabaraza ya usuluhishi. Na ni lazima kuanzia huko kabla ya kwenda Mahakamani.
Law of marriage Act cap.29,1971.ahsante mkuu sasa hiyo sheria ya ndoa ya 1971 haina CAP? hebu naomba full citation mkuu
Watoto wa nje hawana haki ya kurithi labda awagawie kabla hajafa ama awagawie kwenye wosia kama anavyoweza kumgawia mtu yeyote.hivi mme akiwa na watoto wa nje,halafu mimi na yeye tumeoana tukiwa hatuna kitu,then tukafight tukawa matajiri,siku akifa je wanae wa nje wana haki ya kurithi na wanangu wa ndani ya ndoa?
Wana-JF,
Karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.
Asanteni na karibuni!
Ndiyo Mkuu. Ndoa huvunjwa mahakamani kwa utaratibu wa kisheria. Mshauri aanze kufungua shauri la kuvunja ndoa kwanza.Asante sana,
Mimi swali langu ni hili.
Nimeenda kijijini kutafuta mke wa kuoa, nimemkuta mwanamke akiwa anaishi kwao bila mme, niliulizia nikaambiwa wameachana na mme wake miaka mitano iliyopita.
Nilichumbia kwao nikaoa kwa kutoa mahali.
Je! Mume wake wa awali anaweza kuja kushika ugoni kwa kuwa hakutoa talaka?
Kama ametimiza sharti la kuanzia Baraza la Usuluhishi,atasikilizwa upande wake na uamuzi kutolewa.Nina swali, Mwanandoa mmoja akipeleka shauri mahakamani la kutaka talaka na court wakamwita mwenzake na asihudhurie mahakamani zaidi ya mara tatu, Mahakama uchukua hatua gani?
Nenda Baraza la usuruhishi la kata au ustawi wa jamii Wilaya.Usuruhishi ukishindikana mtapewa barua mwende juu,baada ya hapo unaenda mahakamani kuomba divorce decree.Mahakama ikikubali kutoa taraka ,itaamua namna ya kulea watoto,kuwatunza na vipi mgawane Mali.Mgawanyo si lazima nusu kwa nusu mahakama itaamua kulingana na mlivyochangia kuitafuta hyo Mali.Mme wangu ananifukiza kwa sababu zisizo na msingi Mara kwa Mara, ila Mara hii nimeamua kuondoka mana ameanza kunipiga,.kuna Mali tumechuma wote,naanzia wapi ili nipate haki zangu?
Nenda Baraza la usuruhishi la kata au ustawi wa jamii Wilaya.Usuruhishi ukishindikana mtapewa barua mwende juu,baada ya hapo unaenda mahakamani kuomba divorce decree.Mahakama ikikubali kutoa taraka ,itaamua namna ya kulea watoto,kuwatunza na vipi mgawane Mali.Mgawanyo si lazima nusu kwa nusu mahakama itaamua kulingana na mlivyochangia kuitafuta hyo Mali.
Ngoja waje wataalamuNaomba kuuliza.
Nimeishi na mwanamke toka 2000 na tukafunga ndoa mwaka 2007 tumezaa na tuna watoto wawili.
Ila kutokana na tabia zake tulitengana 2015 ili kupeana muda wa kutafakari kwa sababu tulikuwa tumefikia hatua mbaya ila kumbe kulikuwa na mtu aliyekuwa ameingilia ndoa yangu ndo maana tukafikia hali ile.
Tulipotengana kwa muda wakaenda kufunga ndoa ya kwa mkuu wa wilaya na ukumbuke ya kwangu ilikuwa ya kanisani.
Naomba ushauri.
1.Ndoa aliyonayo ni halali?
2.Kisheria nawezaje kupata talaka?
3.je kama kugawana mali tunagawana ipi?ile tuliyokuwa nayo 2015 au tutakayokuwa nayo muda mahakama itakapotoa talaka?
4.Huyo jamaa aliyeingilia ndoa yangu anaweza kuchukuliwa sheria gani?
5.Au naweza kuacha hivyohivyo na mimi nikaenda kufunga ndoa nyingine?
Asante