Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Mkuu, heshima mbele kwa ufutaji huu wa tongo tongo.

Ama baada ya adabu hiyo, mimi nijikite katika muundo, uhalali na upatikanaji (kwa maana ya anuani kamili) ya mabaraza ya usuluhishi kama yanavyotamkwa katika sheria hiyo ya ndoa.

In practical terms: Baraza la Usuluhishi ni nini? (Nina idea linafanya nini kutokana na jina lake), linaundwaje? (How is it formed & what is the composition), linapatikana wapi? Yana Ofisi? (Physical location, nikienda wapi naweza ku-log malalamiko yangu), ratiba zake za kazi (Je, ni Juma tatu hadi ijumaa ama lina msimu wa vikao vyake kama mabaraza ya madiwani?), nini gharama za shauri langu kusikilizwa nao? (How much cost would I incur to have my case deliberated upon), Uhalali wake? (Je lina msajili ama usajili? Nisije nikapata huduma zao ila kufika mahakamani huduma yao ishindwe kutambulika)

Mkuu, niwie radhi, nimeuliza kama vile nataka kwenda kuwaona kesho asubuhi. Utakapojibu, tafadhali jielekeze kwamba muhitaji huduma ya baraza amefunga ndoa ya mke mmoja ya kikristo.
Asante.
 
Samahani mkuu; dada yangu yupo kwenye ndoa, mwaka wa tatu sasa na hawajabahatika kupata mtoto.. Tatizo lililopo ni kwamba dada Hana tena mapenzi na mumewe, je hiyo nayo inaweza kuwa sababu ya kuombea talaka? Ndoa ni ya kiislam
Kupoteza mapenzi si sababu ya kuvunja ndoa kisheria. Sababu zinazoainishwa ni uasherati/uzinzi,mateso na kutelekeza. Kwa ndugu zangu waislam,mwanamke aweza kuvunja ndoa kwa sababu hiyo kwa namna ya kujihurui. Lakini,kimahakama lazima kuwe na sababu nilizozitaja
 
Mkuu, heshima mbele kwa ufutaji huu wa tongo tongo.

Ama baada ya adabu hiyo, mimi nijikite katika muundo, uhalali na upatikanaji (kwa maana ya anuani kamili) ya mabaraza ya usuluhishi kama yanavyotamkwa katika sheria hiyo ya ndoa.

In practical terms: Baraza la Usuluhishi ni nini? (Nina idea linafanya nini kutokana na jina lake), linaundwaje? (How is it formed & what is the composition), linapatikana wapi? Yana Ofisi? (Physical location, nikienda wapi naweza ku-log malalamiko yangu), ratiba zake za kazi (Je, ni Juma tatu hadi ijumaa ama lina msimu wa vikao vyake kama mabaraza ya madiwani?), nini gharama za shauri langu kusikilizwa nao? (How much cost would I incur to have my case deliberated upon), Uhalali wake? (Je lina msajili ama usajili? Nisije nikapata huduma zao ila kufika mahakamani huduma yao ishindwe kutambulika)

Mkuu, niwie radhi, nimeuliza kama vile nataka kwenda kuwaona kesho asubuhi. Utakapojibu, tafadhali jielekeze kwamba muhitaji huduma ya baraza amefunga ndoa ya mke mmoja ya kikristo.
Asante.

Mkuu,Mabaraza ya Usuluhishi hutofautiana kutokana na aina ya ndoa. Kuna ya kidini,kimila na kiserikali. Hivyo,taratibu na ufanyaji wake kazi hutegemea dini,mila au serikali husika. Makanisa,kwa mfano,huwa na Mabaraza yao na yenye taratibu zao. Waislamu hutumia hasa Mabaraza yaliyo Ofisi za BAKWATA.
 
Mali binafsi ndani ya ndoa haitanguliwi na mkataba. Hutanguliwa na taarifa kwa mwenza wako na namna ya upatikanaji wa mali husika. Kikubwa ni kuweka mambo yenu wazi kama wanandoa. Mali binafsi zinaruhusiwa katika ndoa Mkuu Masonjo
Je kama mume ndo ulikuwa unapambana mke hana kazi kakaa nyumbani tu je kwa huyo inafaa kugawana?au inaposemekana kuchuma wote ni kwamba mke anatoa mchango wake kiuchumi kulifanikisha jambo
 
Mkuu,nasikitika kusema kuwa swali hili nilishalijibu humu. Lakini,hata kama mke anakuwa mama wa nyumbani,atapata mgawo wake kadiri mahakama itakavyoona inafaa
 
Endapo nimeishi na mume wangu kwa takribani miaka mitano na katika kipindi hicho ndani ya miaka mitatu hatujakutana kimwili na mume sababu kubwa ikiwa ni yeye japo hasemi kama ana tatizo ama la naweza kuachana nae!?
 
Je ikitokea umemfumania mke/mume je mgoni kisheria anatakiw akulipe fidia y kukuumiza?na je km mgoni aliongopewa kwmb mke/mme hajaoelewa/oa anaweza kushinda kesi ya madai hayo?
 
Mkuu Invisible tafadhali ifanye thread hii sticky ili iwe rahisi kupeana elimu
Je ikitokea umemfumania mke/mume je mgoni kisheria anatakiw akulipe fidia y kukuumiza?na je km mgoni aliongopewa kwmb mke/mme hajaoelewa/oa anaweza kushinda kesi ya madai hayo?
 
Je ikitokea umemfumania mke/mume je mgoni kisheria anatakiw akulipe fidia y kukuumiza?na je km mgoni aliongopewa kwmb mke/mme hajaoelewa/oa anaweza kushinda kesi ya madai hayo?
Mkuu,yote hayo yatategemea ushahidi utakaokuwepo juu ya kosa na madhara uliyoyapata
 
Ninampenz wangu mkristo mimi muislam nataka kumuoa hii imekaaje kisheria?
 
Ikitokea ke/me amemchoka mwenzie bila sbb za msingi anaweza kumuacha? Je anaeachwa anaweza kushtaki kulazmisha mahusiano na akashinda ikawalazimu kuishi ktk mazingira ya kuchokana?
 
Hiyo ni rahisi kwakuwa mtakuwa na chaguo la kuamua. Kwanza,mwaweza wote kuwa kwenye dini moja kwa mmoja wenu kubadili. Halafu,mnafunga ndoa ya dini husika. Pili,mwaweza kufunga ndoa ya kiserikali kama si ya mke mmoja basi ni ya wake wengi. Tambua kuwa,ndoa ya kiislam ni ndoa ya wake wengi kwa uasili wake
 
Mkuu,tenganisha kuachana na kuvunja ndoa. Kuachana kwaweza kufanyika kienyeji. Lakini,ndoa huvunjwa mahakamani kwa taratibu zilizopo.
 
Wana-JF,

Karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.

Asanteni na karibuni!
Kwanini irithi huandikwa na baba wa familia na sio mama?
 
Hiyo ni rahisi kwakuwa mtakuwa na chaguo la kuamua. Kwanza,mwaweza wote kuwa kwenye dini moja kwa mmoja wenu kubadili. Halafu,mnafunga ndoa ya dini husika. Pili,mwaweza kufunga ndoa ya kiserikali kama si ya mke mmoja basi ni ya wake wengi. Tambua kuwa,ndoa ya kiislam ni ndoa ya wake wengi kwa uasili wake
Thnx
 
Back
Top Bottom