Kwanza mengi ya haya mabaraza ya kata hufanya kazi zisizozao kwa kuingilia hata mamlaka ya kugawa mali baada ya dissolution of the marriage.
Mselewa Please assist, kuna mtu alikuwa na kesi, ya dissolution ya marriage, mume ndie aliomba ndoa ivunjwe na kweli mke akaridhia kwani mwanaume alikuwa amemtelekeza na watoto kwa muda wa miaka mitatu bila chochote.
Wakati kesi imepangwa kusikilizwa sijui kuna kitu inaitwa FPTC Hakimu akamwambia yule mama kwa kuwa hana wakili aende akaongee na Wakili wa mumewe amueleze maana ya FPTC alipofika kule wakili akatake advantage akamwambia mama wamalize suala nje ya mahakama kwa makubaliano, kweli mama akaingia king. akasaini yale makubaliano ambayo pamoja na mambo mengine yalijumuisha amri ya kuvunja ndoa, mama kupewa gharama za matunzo kwa muda wote aliotelekezwa na baba akakabidhiwa watoto, ila katika hayo makubaliano hakukuwa na amri ya kugawa mali za wanandoa ambao walichuma pamoja.
Je huyu mama anaweza fungua kesi ili aombe mgawanyo wa mali walizochuma pamoja?