Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Mkuu, kwa mfano watu walifunga ndoa kanisani. Kisha mwanamke akaondoka kwa mumewe bila kufuata utaratibu wowote. Baada ya miaka mitatu kwa mfano, bila mawasiliano kabisa, mwanaume akataka kuoa tena. Anatakiwa kufanyeje ili kuvunja ndoa ya awali na kuingia mpya?
 
Mkuu ndoa ya kikristo ni ndoa ya mke mmoja. Mwisho wake kidini ni hadi mmoja wa wanandoa afariki. Kisheria,ndoa hiyo huvunjwa mahakamani. Inapasa kuvunja ndoa moja kabla ya kuingia nyingine. Hapo sababu ni kutelekezwa
 
Mkuu Petro E. Mselewa naomba kujua taratibu za ndoa ya serikali hua zinakuaje na hatua na vigezo vyake (mwanzo mwisho) ?
Mkuu,kwanza kuwe na umri wa ndoa yaani umri wa utu uzima. Pili,kuwe na matangazo ya ndoa kwa siku zisizopungua 21. Tatu,kufunga ndoa kwa Mkuu wa Wilaya. Taratibu nyingine huelezwa kwenye Wilaya husika
 
Shukran mkuu
 
Nimepitia hii thread kuanzia mwanzo hadi mwisho

Maswali mengi yanajirudia hasahasa kwenye upande la suala la kugawana mali bila kusahau suala la dhanio la ndoa ambapo mitaani watu wengi hudanganyana kuishi na mwanamke kwa miezi kadhaa tu inapelekea kuwa ndoa..

Ingependeza sana kabla ya kuuliza swali mtu upitie nyuma kidogo maana wakati uzi huu unaanza majibu yalikuwa marefu na yenye kueleweka..

Ubarikiwe Petro

Pia watu wengi wanavl
 
Mkuu ndoa ya kikristo ni ndoa ya mke mmoja. Mwisho wake kidini ni hadi mmoja wa wanandoa afariki. Kisheria,ndoa hiyo huvunjwa mahakamani. Inapasa kuvunja ndoa moja kabla ya kuingia nyingine. Hapo sababu ni kutelekezwa
Ahsante mkuu. Kwenye mazingira hayo mwanaume anaweza kudai ametelekezwa na mkewe na ikawa basis ya kuvunja ndoa kanisani?
 
Mkuu,nasisitiza tena na tena,ndoa huvunjwa mahakamani tu. Kanisani na misikitini huwa ni hatua tu za kuelekea kuvunja ndoa
 
Nauliza hivi kwa mfano mume wangu amenitamkia nishakuacha lakini tulikuwa tunatoleana maneno ya hapa na pale nikamtamkia kuwa niache basi na yeye akasema haya nishakuacha basi nenda zako kwenu ! Je Talaka hii itakuwa imesihi na kama imesihi atakuwa ameniacha kwa talaka ngapi hapo ? na ipi suluhu yake ?
 
Mkuu,ingawa swali lako ni la kidini zaidi nitajaribu kulijibu. Kadiri nijuavyo,talaka za kiislamu ni kauli ambayo yaweza kuandikwa au kutamkwa. Ni kauli aitoayo mwanaume kuwa hamuhitaji mkewe tena. Kauli husika huesabiwa kwa kadiri itolewapo. Mwisho ni mara tatu. Kwa talaka moja au mbili,mume aweza kumrudia mkewe kabla ya kumaliza eda ya kuachwa. Ikiisha eda au kwa talaka tatu,mume itampasa amuoe tena mkewe. Zingatia kuwa mimi ni mkristo mwenye ufinyu katika uelewa wa uislamu na sharia.
 
Wengi wetu huamini kuwa kupewa talaka na mumeo au mkeo ndio suala limeishia hapo, hakuna hatua inayofuata na kawaida hakuna utaratibu unaotumika kuwaelimisha kwani wengi hasa wanawake huamua kwenda Baraza la Kata kwa ajili ya kuomba mgawanyo wa mali jambo ambalo sio utaratibu hata kidogo.
 
Kwanza mengi ya haya mabaraza ya kata hufanya kazi zisizozao kwa kuingilia hata mamlaka ya kugawa mali baada ya dissolution of the marriage.
Mselewa Please assist, kuna mtu alikuwa na kesi, ya dissolution ya marriage, mume ndie aliomba ndoa ivunjwe na kweli mke akaridhia kwani mwanaume alikuwa amemtelekeza na watoto kwa muda wa miaka mitatu bila chochote.
Wakati kesi imepangwa kusikilizwa sijui kuna kitu inaitwa FPTC Hakimu akamwambia yule mama kwa kuwa hana wakili aende akaongee na Wakili wa mumewe amueleze maana ya FPTC alipofika kule wakili akatake advantage akamwambia mama wamalize suala nje ya mahakama kwa makubaliano, kweli mama akaingia king. akasaini yale makubaliano ambayo pamoja na mambo mengine yalijumuisha amri ya kuvunja ndoa, mama kupewa gharama za matunzo kwa muda wote aliotelekezwa na baba akakabidhiwa watoto, ila katika hayo makubaliano hakukuwa na amri ya kugawa mali za wanandoa ambao walichuma pamoja.
Je huyu mama anaweza fungua kesi ili aombe mgawanyo wa mali walizochuma pamoja?
 
Mkuu,maombi ya mgawanyo wa machumo yaweza kuwasilishwa yakijitegemea. Hivyobasi,kwakuwa ndoa imeshavunjwa,aweza kuomba mgawanyo wa mali kama tu suala la mgawanyo wa mali halikuwepo kwenye shauri ulilolisema. Vinginevyo,aonane na Mawakili awaonyeshe nyaraka zake ili wamsaidie
 
FPTC ni Final Pre-trial Conference. Kimsingi,ni hatua ya kimajadiliano ya kumaliza mgogoro ulio mahakamani
 
Je Ni muhimu Mtu kwa na vyeti vya ndoa zaidi ya kioja..?

Au Niruksa Mtu kuwa na cheti cha ndoa cha Kiserikali na cha Kanisani vyote 2 kwa pamoja...?
 
Haiwezekani kisheria kuwa na cheti zaidi ya kimoja cha ndoa
 
Back
Top Bottom