KANYEGELO
JF-Expert Member
- Nov 12, 2019
- 2,238
- 4,885
Naomba msaada wa kisheria nahitaji kufanya divorce ni muda wa miaka 2 tumetengana na aliyekuwa mke wangu, ambaye nimebahatika kuzaa naye watoto wawili mmoja ana umri wa miaka 8 mwingine 4.
Tunaishi kila mmoja mikoa miwili tofauti yeye yupo Simiyu mimi nipo Mwanza.
Tatizo la kutengana lilitokea tu ghafla mawasiliano kukatika kumbe alipata mwanaume mwingine kwa siri.
Nimemtolea mahari na nimefunga naye ndoa ya serikali. Nimemwambia kistarabu tu tugawane watoto yeye achukue wa kike na mimi nichukue wa kiume, anakataa.
Nimejaribu kumwambia twende mahakamani kwa ajili ya kutengua ndoa. Nalo hataki. Sasa na mimi umri unaenda. Nataka kuoa sasa mwanamke mwingine.
Na ikiwezekana pia nikae na watoto wangu niwalee mwenyewe maana watoto hawampendi kabisa mama yao japo yeye anawalazimisha kukaa nao. Maana muda mwingi anatumia kukaa na hawala yake kuliko watoto.
Likizo huwa naenda kuwachukua watoto! Watoto wanafurahia sana. Yaani huwa naona kabisa watoto kuna message huwa wananipa juu ya mama yao ila nashindwa la kufanya.
Je, nitumie njia gani ili nipeleke ombi mahakama ya mwanzo kwa ajili ya kutengua ndoa ili kila mtu aangalie ustaarabu wake?
Maana nafikiria kumvizia nimshike ugoni naona kama nitamdhalilisha japo huyo mume wake anakuja mara kwa mara hapo nyumbani na kulala.