Mila ya nani? Kwa kifungu kipi cha sheria, kiweke hapa. Pre-requisites ili iwe ndoa ni:
1.) Lazima wahusika wote wawe wanafahamu kwamba kinachoendelea hapo ni ndoa, sio unamuita mtu kwenye birthday party kumbe ndio unamfungisha ndoa bila yeye kujua, hata kama ni ndoa ya kimila, lazima wote wawe fully aware kwamba tunafunga ndoa ya kimila, na mashahidi lazima wawepo na wajue kwamba wanachoshuhudia ni ndoa na si mahari au ubatizo au birthday au engagement au kingine chochote. Na wahusikanwote lazima wawe timamu wa akili, wasiwe wameleweshwa au ni mataahira wa akili, wawe timamu kwa kila hali, namuhimu sana wasiwe wamelazimishwa kwa namna yoyote ile, iwe kwa blackmail au vitisho vya namna yoyote ile, kinyume cha hapo ni hiyo ndoa ni NULL & VOID.
2.) Ndoa iwe ya kimila, ya Kanisani au ya msikitini ni lazima pawe na mfungishaji ndoa ambae anatambulika kuwa na mamlaka ya sect. hiyo kufungisha ndoa, kama ni ya kimila basi awe mzee wa kimila na ajue kwamba anafungisha ndoa na si kupokea mahari, kwa kanisani awe padri halali na ajue kwamba anafungisha ndoa, kwa msikitini awe ni sheikh halali na ajue kwa anafungisha ndoa.
Sasa hapo kwenye mahari kuwa ndoa ya kimila sijui ni muujiza upi unataka kuutumia, kwamba MC ndio mzee wa kimila anaefungisha ndoa au ni nani? Kwamba mtu anaenda kutoa mahari ili aweze kufunga ndoa aliyoipanga (iwe ya kimila, kanisani, msikitini) ghafla anakuja kuambiwa ameshafunga ndoa tayati hivyo hiyo ndoa nyingine ya kimila / kanisani / msikitini haina haja tena, kwahiyo hii imeshakiuka sharti la kwanza kwamba wahusika lazima wajue kwamba wanafunga ndoa na si vinginevyo.
Hivi mnavyorahisisha haya mambo hivi huwa mnajazanaga upumbavu wapi?
Na kama ndoa si ya Kimila, si ya Kanisani na si ya msikitini basi inayobaki ni 'assumption of marriage' tu, na hii ndio impossible kabisa kudhibitisha its impossible, soma post no. 7.