Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Talaka ipi wakati hawakufunga ndoa?
Hivi wewe unajua maana ya ndoa?? Kwako ndoa ni mpaka kanisani tu au?? Mtu akifungia Bomani kwako sio ndoa?? Mtu akifungiwa ndoa ya mkeka kwako sio ndoa?? Mtu akilipa mahari akapewa mke na wazazi wa mke kwako sio ndoa?? Kama ukiweza kuyajibu hayo maswali vyema, nadhani utajua kuwa; Anatakiwa akampe talaka.

Ushauri:
Kama sijachelewa na ukawa hujaenda hapa baraza la kata;
Fanya hivi; Nenda pale, msikilize atakacho kisema. Ukiisha msikiliza waambie baraza kuwa, humpi talaka bali unamfukuza atoke kwako.

Waambie kuwa, unampa ruhusa kuolewa na huo mchepuko wake na unaomba kiongozi mmoja mwongozane hadi kwako huyo kicheche akachukue kila kilicho chake ila watoto asiwaguse utawalea mwenyewe.

Tangu leo ukimkuta unajua sio mkeo tena bali ni mke wa mtu. Ukimpa talaka ataomba mgawane mali ili akale na huyo mchepuo wake.
 
mangatara,
Wapi nimesema ndoa ya bomani au ya mkeka si ndoa? Kwani ndoa ni utashi wa mtu au ni kitu kilichokuwa defined kisheria?

Sheria inatambua ndoa za aina 4 tu, za kidini, za kimila, za kiserikali (bomani) au presumption of marriage. Sasa niambie yeye kufunga nae ndoa ipi kati ya hizo nne?! Pia rejea post yangu namba 7 na 8 kwa ufafanuzi zaidi.
 
I got rid of mine miaka 10 iliyopita, usimruhusu mtu akuharibia amani na furaha yako, muda uliompa unatosha, mpe talaka, mwache aende zake uanze upya, mwenzio ndio nilichofanya, and now i am happy again

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapi nimesema ndoa ya bomani au ya mkeka si ndoa? Kwani ndoa ni utashi wa mtu au ni kitu kilichokuwa defined kisheria?
Sheria inatambua ndoa za aina 4 tu, za kidini, za kimila, za kiserikali (bomani) au presumption of marriage. Sasa niambie yeye kufunga nae ndoa ipi kati ya hizo nne?! Pia rejea post yangu namba 7 na 8 kwa ufafanuzi zaidi.
Kafunga ya kimila.
 
Kaka pole we nenda baraza la ndoa la kata ,utaulizwa maswali baada ya hapo mtajaziwa fomu kuwa suluhu mmeshindwa kufikia ...watapendekeza mwende mahakama ya mwanzo , mkifika kule mpe taraka yake wewe jikite namna ya kulea watoto ...USIFANYE KOSA LA KUONESHA KUWA BADO UNAMPENDA UTAKOSEA

MI MWENZIO NILIKUWA NATATIZO KM LAKO LAKINI NILITOA TARAKA MAISHA YAMEENDELEA WW BADO NI KIJANA SANA USIJIKATIE TAMAA KIAC HICHO

MAISHA YAPO UTAPATA MTU AMBAYE NI SAHIHI ATAKUOENDA MPK UTASHANGAA KUBALI KUFUNGUA UKURASA MWINGINE

Sent using i phone x
 
Sheria inasema baada ya miezi 6 Kama sikosei tayari Ni mke.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna sheria ya hivyo ya ndoa ni uwongo mtupu soma sheria ya ndoa ya mwaka 1970, ndio utajua usipende mamabo ya kuambiwa

Mahakama inatambua ndoa kwa vithibitisho maaalumu km cheti cha ndoa ,hati ya kimila , cheti ya kanisa cha kubariki ndoa .....lkn sio kusema tu kwa mdomo eti tumeishi miezi 6 ni uwongo

Hayo yanaitwa mahusiano na sio ndoa

Sent using i phone x
 
Kafunga ya kimila.
Mila ya nani? Kwa kifungu kipi cha sheria, kiweke hapa. Pre-requisites ili iwe ndoa ni:

1.) Lazima wahusika wote wawe wanafahamu kwamba kinachoendelea hapo ni ndoa, sio unamuita mtu kwenye birthday party kumbe ndio unamfungisha ndoa bila yeye kujua, hata kama ni ndoa ya kimila, lazima wote wawe fully aware kwamba tunafunga ndoa ya kimila, na mashahidi lazima wawepo na wajue kwamba wanachoshuhudia ni ndoa na si mahari au ubatizo au birthday au engagement au kingine chochote. Na wahusikanwote lazima wawe timamu wa akili, wasiwe wameleweshwa au ni mataahira wa akili, wawe timamu kwa kila hali, namuhimu sana wasiwe wamelazimishwa kwa namna yoyote ile, iwe kwa blackmail au vitisho vya namna yoyote ile, kinyume cha hapo ni hiyo ndoa ni NULL & VOID.

2.) Ndoa iwe ya kimila, ya Kanisani au ya msikitini ni lazima pawe na mfungishaji ndoa ambae anatambulika kuwa na mamlaka ya sect. hiyo kufungisha ndoa, kama ni ya kimila basi awe mzee wa kimila na ajue kwamba anafungisha ndoa na si kupokea mahari, kwa kanisani awe padri halali na ajue kwamba anafungisha ndoa, kwa msikitini awe ni sheikh halali na ajue kwa anafungisha ndoa.

Sasa hapo kwenye mahari kuwa ndoa ya kimila sijui ni muujiza upi unataka kuutumia, kwamba MC ndio mzee wa kimila anaefungisha ndoa au ni nani? Kwamba mtu anaenda kutoa mahari ili aweze kufunga ndoa aliyoipanga (iwe ya kimila, kanisani, msikitini) ghafla anakuja kuambiwa ameshafunga ndoa tayati hivyo hiyo ndoa nyingine ya kimila / kanisani / msikitini haina haja tena, kwahiyo hii imeshakiuka sharti la kwanza kwamba wahusika lazima wajue kwamba wanafunga ndoa na si vinginevyo.
Hivi mnavyorahisisha haya mambo hivi huwa mnajazanaga upumbavu wapi?

Na kama ndoa si ya Kimila, si ya Kanisani na si ya msikitini basi inayobaki ni 'assumption of marriage' tu, na hii ndio impossible kabisa kudhibitisha its impossible, soma post no. 7.
 
Sijaelewa hapo sheria unataka ikusaidie nini hapo...., haya mambo ya roho mtu kama amekuchoka kuendelea kungangania ni kukaribisha mfaidhaiko na stress za bure..., wakati wazee wa zamani wanasema mpende anayekupenda asiyekupenda achana nae ulikuwa wapi ?
 
Majirani kama waliwstambua kama mke na mume yatosha ila inakuwa presumed tu ili kila upande upate mgao kwenye mali mliyochuma kama IPO na matunzo ya watoto kama wapo.sheria ya ndoa 1971 kifungu 160.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo sheria imeshapitwa na wakati. Hivi nikiishi na mwanamke kwa muda wa miezi 6 na majirani wakatutambua kama mume na mke hiyo inatambulika kwamba ni 'Presumption of marriage'?. Sheria iliyopo inforce currently inatamka wazi kwamba mkiishi kama mume na mke kwa muda wa miaka miwili chini ya paa moja.

Kwahiyo udhibitishe kwamba mliishi kwa miaka miwili, dhibitisha kwamba mliishi chini ya paa moja, na dhibitisha kwamba mliishi kama mume na mke, hayo ndio matakwa ya sheria ya sasa.
 
Mfano,ukiishi miezi 6 na bint wawatu mnamka pamoja hizo siku, serikali/kisheria tunatambua ni mkeo,ukilipa Mali kama jamaa bila kwenda kanisani pia tayari nimkeo..vifungu utavikuta hukohuko ,kwahyo kaa mkao wakula ili usijishangae siku

Sent using Jamii Forums mobile app
Weka kifungu cha hiyo sheria. Au weka link, tusiandikie mate wakati wino upo, ndoa si utashi wa mtu bali ni kitu chenye definition kisheria.
 
Back
Top Bottom