Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Nashukuru kwa majibu yako. Lakini nina swali jingine kama hutajali, nalo ni: hivi kabla ya watu kufunga ndoa, huwa kuna utaratibu wa kuomba na kupewa 'marriage license' inayowapa hao wanandoa watarajiwa rukhsa na uhalali wa kufunga ndoa?

Nauliza tu hivyo kwa sababu kuna nchi zingine ambazo mtu huwezi tu kwenda kufunga ndoa halali bila kupata hiyo leseni ya ndoa.

Tanzania tunao huo utaratibu?

Hakuna huo utaratibu Mkuu Nyani Ngabu.Labda masharti au sifa anazopaswa kuwa nazo anayetaka kufunga ndoa zaweza kutafsirika kama ndiyo leseni yenyewe. Lakini,kwasasa makanisa mbalimbali yana taratibu mbalimbali za ndani kuelekea kufunga ndoa.Pia,zaweza kutafsirika kama leseni. Lakini,kisheria hakuna Mkuu
 
Last edited by a moderator:
Kaka Petro E. Mselewa ...nimetengana na mwenzi wangu toka ndoa ya kiKristo sababu kubwa ni hatukuwa na furaha wala amani katika miaka yetu mi3 ya ndoa, na sasa ni miaka mi3 tangu tutengane (sio legal separation nikiwa na maana hatukutengana mahakani). Tuna mtoto mmoja wa miaka mi5 na katika miaka yote hiyo mi3 tuliyotengana nimekuwa nikimsupport yeye na mtoto fully. Juhudi za kutupatisha (ndugu na marifiki, si mabaraza) hazijafanikiwa, na hakuna dalili yoyote ya kurudiana. Sasa kimefika kipindi 'I need to move on', namaanisha tudivorce. Je, nahitaji kufuata procedure zote hizo kuanzia kwenye mabaraza kabla ya kwenda mahakamani? Je, nina nafasi ya kuwin custody ya mtoto (full au shared ili mradi niishi naye, ana miaka mi5)?

Mkuu Riwa, kwakuwa taratibu hizo zote zilikuwa ni za kijamii na sasa unataka kufuata taratibu za kisheria, kuanzia Baraza la Usuluhishi wa Ndoa hakuepukiki.Hii ni kwakuwa kifungu cha 101 cha Sheria ya Ndoa kinalazimisha hatua hiyo kabla ya Maombi ya Talaka Mahakamani.

Kuhusu kupewa mtoto,itategemea na hoja za kisheria na kijamii utakazozijenga Mkuu. Lakini,yawezekana kupewa mtoto kwa ajili ya kuishi naye
 
Last edited by a moderator:
Hongera saana kwa fursa hii, nina swali moja la faster

1. Je, ndugu/rafiki/mtu yeyote anaweza kumkamata ugoni mke asie wake?
 
Hongera saana kwa fursa hii, nina swali moja la faster

1. Je, ndugu/rafiki/mtu yeyote anaweza kumkamata ugoni mke asie wake?

Anaweza Mkuu.Kikubwa ni kumkabidhi mwenye mke ushahidi wa kukamata mgoni huyo. Lakini,hawezi kushtaki
 
Wakili kaka msomi mimi nina viswali vyangu kadhaa...

Je, hiyo sheria ya ndoa inazungumziaje mambo ya pre-nup na post-nup?

Je, hiyo sheria ya ndoa inaruhusu ubatilishwaji wa ndoa?

Kama inaruhusu, ni mazingira au hali gani ndo zaweza kusababisha ndoa kubatilishwa?

Na ni kwa baada ya muda gani, baada ya ndoa kufungwa, ndo inaweza kubatilishwa?

Labda kwa kujibu swali lako kuhusu pre nuptials na post nuptials naomba nikuhakikishie kuwa zinakubalika Tanzania (ingawa sheria haiko wazi sana katika hili hasa kifungu cha 58). Hapo nilipohighlight panatoa posibility ya kuamua ni mali zipi ziwe za ndoa na zipi zisiwe za ndoa. Uamuzi huu (kwa mtazamo wangu) waweza kufanywa kabla ya ndoa na hata baada ya ndoa isipokuwa tu uamuzi huu lazima uzingatie vigezo vilivyowekwa na sheria katika kifungu cha 59. Kfungu cha 59 kinaongelea ushirikishwaji na ruhusa (consent) ya mwenza katika kutoa zawadi ya mali au mauzo.

Nakiambatanisha kifungu chote:
58. Subject to the provisions of section 59 and to any agreement to the contrary that the parties may make, a marriage shall not operate to change the ownership of any property to which either the husband or the wife may be entitled or to prevent either the husband or the wife from acquiring, holding and disposing of any property.

Hapo nilip
 
Vipi masuala ya alienation of affection, sheria ya ndoa inayazungumziaje hayo? Mwanamke au mwanamme anaweza akamshitaki mwizi wa penzi lake?
 
Kaka mimi nina swali,je ni kweli kwamba mume anaweza kumbaka mke wake wa ndoa?na je endapo mke ana nia ya kushtaki,hili ni kosa la kisheria?ntashkuru sana
 
Kaka mimi nina swali,je ni kweli kwamba mume anaweza kumbaka mke wake wa ndoa?na je endapo mke ana nia ya kushtaki,hili ni kosa la kisheria?ntashkuru sana

Mkuu LINDAIKEJI,niwie radhi kwakuwa sitaweza kujibu swali lako.Hili si sehemu ya Sheria ya Ndoa.Ni masuala ya ubakaji ambayo yapo katika sheria nyingine za nchi hii. Anzisha uzi na tutakuja huko kukusaidia. Asante
 
Last edited by a moderator:
Na kuongezea ilo swali linajibu pia swali alilokuwa ameulizia nameless girl

Mkuu Nyani Ngabu, asante kwa maswali yako. Kuhusu la kwanza,Sheria ya Ndoa,1971 haina utaratibu wa Makubaliano ya mgawanyo wa mali kabla au baada ya ndoa.Mgawanyo hufanywa kisheria Mahakamani baada ya kuvunjwa ka ndoa. Isipokuwa, kifungu cha 58 kinaruhusu Makubaliano baina ya wanandoa katika namna ya kupata,kutunza na kuzitumia mali zinazopatikana wakati wa ndoa.

Kuhusu la pili, ndoa hubatilishwa. Mambo kadhaa yanaweza kuifanya Mahakama,baada ya kupokea Maombi toka kwa mmoja wa wanandoa, kubatilisha ndoa. Kwanza,pale ambapo mmoja wa wanandoa hakuwa na umri wa kufunga ndoa na ridhaa ya wazazi haikutolewa kwa kipindi hicho. Pili, kama mwanandoa,wakati ndoa ikifungwa,alikuwa akishambuliwa na kichaa au kifafa.Tatu, kama mwanandoa anakataa kujamiiana kwa makusudi. Na kadhalika.Jisomee kifungu cha 39 cha Sheria ya Ndoa,1971.

Kuhusu swali la tatu, muda wa kubatilisha hutegemeana na sababu ya kuomba kubatilisha.Kwa mfano, kama sababu ni kuwa mwanandoa mmoja alikuwa hana umri wa kufunga ndoa na ridhaa ya wazazi haikuwepo,maombi ya kubatilishwa lazima yawe kabla ya mwanandoa huyo kutimiza umri wa miaka 18.Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 98 (1) (b) cha Sheria ya Ndoa
 
Je kama mtu na mewe wamefunga ndoa, halafu baada ya kufunga ndoa kumbe mwanaume afanyi kazi (yaani hasimamishi) na wameendelea kwa muda kama wa miaka mitatu...je mwanamke anaweza kuomba talaka?
 
Kumsaidia kidogo ni kwamba hayo makosa ya ubakaji hayako kwenye sheria hii inayozungumziwa ya ndoa bali yako kwenye makosa ya jina.
Mfano katika sheria mpya ya Sexual Offences Special Provisions Act (SOSPA)ambayo ilileta mabadiliko mbali mbali katika sheria mama ya makosa ya jinai (Penal Code) haikutoja na jibu kamili kwenye kifungu 130(2) cha Sheria ya Makosa ya Jinai kuhusu ubakaji wale walio kwenye ndoa halali. Kifungu 130(2) (a) cha Sheria ya Makosa ya Jinai kinaongela tu makosa ya kubaka kwa mke na mme wametengana kisheria. Kwa hiyo mwanamke ambaye ameolewa kisheria na bado yuko kwenye ndoa hawezi kuhesabiwa amebakwa kama amekubali au hajakubali (wife who is still married cannot be raped whether or not she has consented to having intercourse with her husband or she has been forced to have sex in circumstances amounting to rape) na hiyo inakuwa suported na mila na dini zinazoamini hivyo. Kama nilivyosema mpaka hapo kama wametengana kisheria (legally separated). Na kama wako wote hayo yatakuwa ni makosa ya shambulio (assault). Ila kama alivyosema kaka yangu msomi ilo swali peleke kwenye thred nyingine inayozungumzia makosa ya jinai

Mkuu LINDAIKEJI,niwie radhi kwakuwa sitaweza kujibu swali lako.Hili si sehemu ya Sheria ya Ndoa.Ni masuala ya ubakaji ambayo yapo katika sheria nyingine za nchi hii. Anzisha uzi na tutakuja huko kukusaidia. Asante
 
Mh. Kuna kesi moja ya dada yangu ambayo mume alitelekeza familia ya watoto wawili akaenda kuishi kwingine na kimada. Mume yule akaenda mahakamani kufungua kesi ya talaka ili aweze kuoa yule kimada. Alifungua kesi 3 na zote talaka hakupata, Ya kwanza alitumia hati ya usuluhishi imepitwa na wakati, ya pili hakuhudhuria kesi ikafutwa, ya tatu akaomba restoration baada ya miaka kama mitatu kupita. Suprisingly, eti hakimu akakubali restoration!!!! (najua 90 days ndiyo utaratibu). Hata hivyo mdai hakufika mahakamani huku mdaiwa akiwa anahudhuria for 3 good years. Mwishowe ikafutwa tena. Sasa mdai ameamua kugeukia kanisani akiomba ndoa ibatilishwe!! Huko nako najua itagonga mwamba!!! Sasa kisheria mdai anaweza tena kurudi mahakama ya serikali kufungua tena kesi ya nne? Je kwa kuwa mdai alitelekeza familia bila sababu i.e he is not clean before the law) je anaweza kufungua kesi ya madai ya talaka? Je kati ya mke na mume huyu ni nani mwenye haki ya kufungua kesi ya talaka?
 
Je kama mtu na mewe wamefunga ndoa, halafu baada ya kufunga ndoa kumbe mwanaume afanyi kazi (yaani hasimamishi) na wameendelea kwa muda kama wa miaka mitatu...je mwanamke anaweza kuomba talaka?

Ndiyo Mkuu SOCIOLOGISTTZ.Lakini,mwanamke atapaswa kuieleza Mahakama ni kwanini alichelewa kuleta shauri kwa muda wote huo wa tatizo. Kutosimamisha ni moja ya sababu za kubatilisha ndoa chini ya Sheria ya Ndoa ninayoizungumzia hapa. Asante.
 
Last edited by a moderator:
Swali ilo lilikuwa limejibiwa uko nyuma kuhusu kubatilisha ndoa na sababu iliyotajwa ni kuhusu kutokuwa na uwezo kujamiana (incapable of consumating it or impotence) na inapatikana kwenye Sheria ya Ndoa ya 1971 kifungu 39(a)(i)

Je kama mtu na mewe wamefunga ndoa, halafu baada ya kufunga ndoa kumbe mwanaume afanyi kazi (yaani hasimamishi) na wameendelea kwa muda kama wa miaka mitatu...je mwanamke anaweza kuomba talaka?
 
Ndiyo Mkuu SOCIOLOGISTTZ.Lakini,mwanamke atapaswa kuieleza Mahakama ni kwanini alichelewa kuleta shauri kwa muda wote huo wa tatizo. Kutosimamisha ni moja ya sababu za kubatilisha ndoa chini ya Sheria ya Ndoa ninayoizungumzia hapa. Asante.
kama ndiyo hivyo mbona wanamsakama Dr. Slaa kwamba kapora mke wa mtu kumbe sheria ziko wazi namna hii? Nawaomba MACCM yajifunze sheria hii ili wasiendelee kudhalilisha watu wenye matatizo ya kutokusimamisha. Au unaweza kuniambia kuna kosa lolote mtu anaweza kutenda kwa kumdhalilisha mtu asiyesimamisha?

Back
Top Bottom