Sheria ya Pasu Kwa Pasu ifutwe Kwa Hoja zifuatazo

Kuna Tatizo na Huu Uzi.
Kuna Tatizo na Huu Uzi.

WiZARA YA AFYA pamoja NA Wizara ya USTAWI WA JAMII

Jamani msifungie macho mambo kama haya.
 
Kuna Tatizo na Huu Uzi.
Kuna Tatizo na Huu Uzi.

WiZARA YA AFYA pamoja NA Wizara ya USTAWI WA JAMII

Jamani msifungie macho mambo kama haya.
Haya yote kasababisha yule tapeli mke wa Dokta mwaka, watu wataacha kuoa sasa
 
Sheria ya ndoa muda mwingine imekuwa ikitumiwa vibaya na watoa haki na kuwapa kibri wanawake. Siku hizi wanawake hawaoni shida kusema " km vipi tuachane tugawane mali pasu kwa pasu". Udhaifu wa sheria hii ni pamoja na kupendelea wanawake. Hivi inakuwaje haki inatakiwa itendeke baina ya pande mbili alafu hapohapo sheria hiyo inampa mmoja haki kabla ya haki kuwa haki kwa wote. Kwa lugha nyingine ktk kugawana mali hakuna haki kwa wote bali haki kwa mmoja na kinachobakia ndio haki kwa mwingine. Hii inamaana " ladies first". Walahi wanawake watazidi kula jasho la waume zao kwa sheria hizi, na ndio maana wanadai talaka Kila siku sababu wanajua Kuna HAKI inawasubiri.
 
Sijasoma bandiko lote ila mawazo yako yanatupa tabu sana ktk kuchangia michango hasa ya akina mama wanaokaa nyumbani na kulea familia

Unaweza kudhani kuwa ulezi wa familia ni kitu kidogo lakini kimantiki ni kazi kubwa sana uwepo wake tu inatosha kumpa amani mtafutaji mkuu na kumhamasisha kutafuta zaidi

Pia wanawake wengine michango yao sio tangiable wao huwa kama motivation factor ambapo bila wao hao watafutaji wakuu wasingepata motisha ya kutafuta zaidi

Ishu ipo kwenye kutambua na kuchanganua michango ya wenzetu akina mama hasa wa nyumbani
 
Tena ni mchango mkubwa sana
 
Hata wanaume wametumia madaraka yao vibaya kunyanyasa wanawake na hata kutelekeza familia na kukacha majukumu yao. Hivyo siyo sahihi kudhani kwamba tatizo kwenye ndoa ni wanawake peke yao. Sheria kutumika vibaya hili lipo, na binafsi siwezi kupinga, lakini matukio mengi na mifano ambayo mnaileta hapa ni ile ambayo mmeiangalia kwenye mitandao hasahasa kwenye nchi za Marekani na Ulaya. Tena nako mambo hayatokei kama ambavyo mnalazimisha tuyaone......
 
kasome case ya bi Hawa vs mume wake
 
Bora ndoa zifutwe tu,maana inakoelekea watu wataangalia mali na sio mapenzi
 
wanawake wenyewe tegemezi;
hunipikii
hunifulii
huna chochote unachozalisha
halafu unakuja na story za pasu kwa pasu! Inauma sana
 
Sasa hapa Robert ndo tutakutana kwenye point ya kwamba na wanawake wapewe fursa kwenye kazi, michakariko ya maendeleo. Kuna mwanaume anakwambia mwanamke atafute mali ya kazi gani wakati mumewe anamuhudumia, the same time mnasema wakiachana kila mtu aondoke na alichokitafuta. Hapo kuna haki?

Watu wanakwambia wanawake wanaofanya kazi ni wajeuri, so mwanamke anatakiwa akae tu nyumbani alee watoto, ikatokea wameachana huyu mwanamke ataondoka na nini ilhali ametumia muda wake kukaa nyumbani? Ni kweli sheria ya mwanamke kupewa mali pasu kwa pasu na haswa kama kaikuta sio sawa ila pia kumkandamiza na kumwambia akae nyumbani asifanye kazi ila mwanaume ana uhuru wa kumwacha mtupu hapo ndo kwenye shida.
 
Ndio iko hivyo, wanawake wengi wanaona ni jambo rahisi , eti upate 50/50, hilo halipo na halitakaa litokee. Wengi wanaangukia pua. Ni vyema wanawake na sisi tumiliki mali zetu au mali za pamoja tusisubirie huruma za mahakama.
 
Mwanamke anayejitambua hawezi kukaa nyumbani tu hata siku moja bila kuongeza kipato cha familia.
 
Mbona hujaweka hiyo sheria ya pasu kwa pasu tuione? Bila ushahidi ni hadithi tu umeandika hapa.
 
Umenena vyema! Japo umefanya makosa kuwaambia ukweli. Ungewaacha waendelee kuamini hizi porojo zao.
Kuna jirani yangu aliachana na mme wake, alimkuta jamaa na nyumba, kaambulia milion 11 tu. Tena yeye alichangia kidogo kwenye finishing
 
Wewe unaongea tu, mshahara wa mwanamke wanakwambia ni wake, ila wako ni wa familia, hata akiumwa yeye, wewe ndio umtibie, ukimuuliza pesa zako unapeleka wapi, hasemi, mambo ya ajabu
Huyo anafanya kazi ili iweje? Mama zetu walikuwa wanachangia ustawi wa familia, sembuse kipindi hiki cha uchumi wa kati.
 
Lakini mali inabaki ya mmiliki. Anamhusisha tu kama anataka kuuza etc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…