Sheria yetu ya uchaguzi, inaruhusu mgombea uraisi kugombea bila kuwa na wadhamini wa ndani ya chama chake?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Naomba wanasheria na wadau wengine wa mambo ya uchaguzi watusaidie kutupa ufafanuzi juu ya hiili.

Pia, nini maana na wajibu wa kisheria wa wanaoitwa wadhamini ili tuone implication yake katika sheria na zoezi zima la uchaguzi wa Raisi.

Na je, kisheria, kuna uhusiano gani kati ya sheria ya uchaguzi na uteuzi wa wagombea ndani ya vyama?

Yaani sheria ya vyama vya siasa inaelekeza nini kuhusu wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika nchi au sheria ya vyama vya siasa iko kimya juu ya taratibu za uteuzi wa wagombea katika vyama vya siasa?

Na ikitokea, sheria ya vyama vya siasa na sheria ya uchaguzi, zinkinzanqi katika swala zima la uhalali wa mgombea, sheria ipi inasimama?

Mwisho, mgombea wa uraisi ambae hana wadhamini, anaweza kupingwa mahakamani?

Karibu wadau tupeane elimu juu ya hili.
 
Inategemea na huyo mgombea anatokea chama kipi. Kama ni nje ya CCM lazima awe na wadhamini ila ndani ya CCM wadhamini sio lazima.
 
Inategemea na huyo mgombea anatokea chama kipi. Kama ni nje ya CCM lazima awe na wadhamini ila ndani ya CCM wadhamini sio lazima.
Hapana!
Magufuli alikuwa na Wadhamini!
Lowasa kabla ya Kukatwa Jina alikuwa na Wadhamini!
Kikwete alikuwa na Wadhamini!
Mkapa alikuwa na Wadhamiini!
Salim ahmed alikuwa na Wadhamini!
 
Tume bado haijatoa fomu bwashee punguzeni papara

CCM ina utamaduni wake 🐼
Kwa utamaduni wetu sisi wana CCM tumeamua kwa kauli moja mgombea wetu ni Daktari, hatuna mgombea mwingine zaidi yake. Kama wewe sio Daktari kaa mbali, usije ukajuta baadae.
 
Hapana!
Magufuli alikuwa na Wadhamini!
Lowasa kabla ya Kukatwa Jina alikuwa na Wadhamini!
Kikwete alikuwa na Wadhamini!
Mkapa alikuwa na Wadhamiini!
Salim ahmed alikuwa na Wadhamini!
MIla na desturi huwa zinabadilika kadri ya mahitaji ya nyakati. Huenda kwa mara ya kwanza chama fulani kitakuwa na mgombea asiye na wadhamini au tuseme ameamua kujidhamini mwenyewe japo sijui kama inakubalika.
 
Mila na desturi Haibadiliki Bila Kuwa na Taarifa ya mabadiliko Kwa wadau..
Hakuna Kikundi watu wala jamii fulani inayojipa Uhalali wa kubadili Mila na Desturi bila kutoa taarifa kwa Jamii itakayoiishi mila Hizo
 
Kama taasisi imeingiliwa na wahuni,tena wahuni wazee. What do you expect ?
 
Uhalali wa mgombea unaanzia ndani ya chama chake au unaanza kuangaliwa na sheria ya uchaguzi pale anapojitokeza kuchukua form ya uchaguzi?
Tume haina taarifa kama kuna mgombea wa chama chochote. Atakayeenda kuchukua na kurudisha fomu ndio ataambatanisha na majina ya wadhamini. So wadhamini wanaweza kupatikana ndani ya siku mbili tu nchi nzima. Hata Kikwete 1995 alichukua fomu na kukusanya saini za wadhamini nchi nzima ndani ya siku moja tu!
 
Kitendo tu cha Rostam kuwepo kwenye dira tegemea udhamini upo 100%.
 
Wadhamini Ndani ya Nchi nzima Kwa siku moja? πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”

Nchi yenye Watu Milion 60..Ukubwa unaozidi 40milion Kilomita square..
Chi yenye Mikoa 26 ?
Is it factual Correct??
 
Wadhamini Ndani ya Nchi nzima Kwa siku moja? πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”

Nchi yenye Watu Milion 60..Ukubwa unaozidi 40milion Kilomita square..
Chi yenye Mikoa 26 ?
Is it factual Correct??
Basi ndio maswali tuliyojiuliza sana tuliokuwepo 1995.
Nyerere alimwita ghafla Kikwete achukue fomu baada ya kujitokeza Prof. Kighoma Malima. Ndani ya siku moja eti JK alichukua fomu, akazunguka mikoa 10 kupata wadhamini na kesho yake akarejesha fomu. Maswali yako hayakupata majibu baada ya Prof. Malima kuhoji hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…