Shetani hana rafiki: Israel yatimua Majenerali wake sababu ya October 7, 2023

Uchambuzi mzuri. Mtu ambaye hakutimiza wajibu, anawajibishwa. Hata hapa TZ aliyesababisha ghasia zilizojitokeza mwezi Oktoba anabidi awajibike. Aliyemdangaya Rais kwamba hakuna mwananchi atakayeandamana awajibishwe; pia, la muhimu zaidi, aliyeagiza raia wauawe awajibishwe vilivyo.
 
Wasingeenda wachapa Iran namna ile. Israel ilipata sababu ya kuwachakaza Hamas na ndugu zake. Kwa sasa unawasikia tena?

Wamemaliza kazi. Bado maeneo madogo tu.
 

Dogo kuna mambo mengi hujui. Hii si sawa na kuvuta shisha au kula ubwabwa kwa ndizi
 


JamiiForums
International Forum
Hongera IDF kwa kuwapeleka mputa mputa Hezbollah huko Lebanon
Thread starterEcholima1 Start dateYesterday at 9:19 AM Tagshezbollah in lebanon
Jump to new
Subscribe

•••
Echolima1
Echolima1
JF-Expert Member
Yesterday at 9:19 AM
New
Add bookmark
#1
Msemaji wa IDF atangaza rasmi:

IDF imemwangamiza Haitham Ali Tabatabai, Mkuu wa utawala wa shirika la kigaidi la Hezbollah.

Msemaji wa IDF atangaza kwamba leo, Novemba 23, 2025, IDF, ikiongozwa na vitengo vya Ujasusi wa Kijeshi na kupitia Jeshi la Anga, ilishambulia eneo la Beirut na kumuongamiza gaidi Haitham Ali Tabatabai, Mkuu wa utawala katika kundi la kigaidi la Hezbollah.

Tatabai alikuwa mkongwe na mhudumu mkuu katika shirika la kigaidi. Alijiunga na safu zake miaka ya 1980 na tangu wakati huo alishikilia safu ya nafasi za juu, ikiwa ni pamoja na kamanda wa Kikosi cha Radwan na mkuu wa shughuli za Hezbollah nchini Syria. Katika nafasi yake nchini Syria, aliimarisha uimarishaji wa Hezbollah nchini.

Wakati wa vita, aliteuliwa kuwa mkuu wa mfumo wa shughuli za shirika, na katika nafasi hii alikuwa na jukumu la kuimarisha picha ya uendeshaji na kujenga uwezo wa shirika. Wakati wa Operesheni "Mishale ya Kaskazini (“Northern Arrows”,)
baada ya uongozi mwingi wa kijeshi kuangamizwa, alihudumu kama kamanda wa kweli anayesimamia mapigano dhidi ya Israeli.

Mwishoni mwa Operesheni "Mishale ya Kaskazini", (Northern Arrow)Tabatabai aliteuliwa kuwa Mkuu wa utawala wa Hezbollah, na katika jukumu hili aliongoza ujenzi mpya wa shirika hilo. Tabatabai aliongoza vitengo vingi vya Hezbollah na alifanya kazi kwa bidii ili kurejesha utayari wao wa vita na Israeli.
Huyu ni mkuu wa tatu wa maafisa wakuu wa Hezbollah ambaye Israeli imemwangamiza tangu Oct 07,2023

Wa kwanza alikuwa Fuad Shukr aliangamizwa Julai 30, 2024

Wa pili alikuwa Ibrahim Aqil aliangamizwa Septemba 29, 2024

Wa tatu Haitham Ali Tabatabai ambaye aliangamizwa jana Novemba 23, 2025
 
Wasingeenda wachapa Iran namna ile. Israel ilipata sababu ya kuwachakaza Hamas na ndugu zake. Kwa sasa unawasikia tena?

Wamemaliza kazi. Bado maeneo madogo tu.
Nawasikia ndio, Hamas bado ipo na inazidi recruit sababu uhuru wao haujapatikana so usidhani itaondoka leo wala kesho. Na hata mkiua wote wataunda chama kingine na kuendeleza pale pale walipoishia Hamas na Qaseem Brigade
 
October 7 imeisaidia Israel kuharibu maadui zake wote
 
Ulitegemea nini sasa. Unafikir watu walioserious na nchi zao wanavumilia kosa kama nyie sio
 
Huo ndiyo uwajibikaji! Unafikiri haya Mauaji yaliyotokea kuanzia okt 29 ingekuwa huko CDF,IGP,DTISS,Kamishina wa Uhamiaji wangekuwa kazini?
 
Nawasikia ndio, Hamas bado ipo na inazidi recruit sababu uhuru wao haujapatikana so usidhani itaondoka leo wala kesho. Na hata mkiua wote wataunda chama kingine na kuendeleza pale pale walipoishia Hamas na Qaseem Brigade

Mkiua tena? 🤣 Israel au mimi? Wanachofanya ni kulipiza watu wao wanapouawa. Ni jino kwa jino. So Hamas wakiunda nao wanaunda. Ni vuta n'kuvute. Hakuna kulia.
 
Kipi sikijui? Taja basi usikimbie mada

October 7 imekuwa siku ambayo iliwapa sababu kubwa Israel kuwafanyia kazi maadui zake. Walipata sababu kubwa ya kugalagaza watu waliokuwa wapo kwenye target Hamas, Hezbollah na Iran.
 
October 7 imekuwa siku ambayo iliwapa sababu kubwa Israel kuwafanyia kazi maadui zake. Walipata sababu kubwa ya kugalagaza watu waliokuwa wapo kwenye target Hamas, Hezbollah na Iran.
Kwamba kabla ya oktoba 7 Israel haikuwahi shambulia Iran, Hezbollah na Hamas? Upo serious kweli? Israel haiihitaji sababu ili ishambulie imefanya sana ugaidi huko westbank ingawa hakuna hao maadui zake uliowataja.
 
Netanyahu yuko sahihi kabisa.

Vipi kuhusu kwenu huko Malawi ambapo mtoto wa DGIS anachezea dollars huku kainua kidole cha kati juu kwa raia wa Malawi?
 
Kwamba kabla ya oktoba 7 Israel haikuwahi shambulia Iran, Hezbollah na Hamas? Upo serious kweli? Israel haiihitaji sababu ili ishambulie imefanya sana ugaidi huko westbank ingawa hakuna hao maadui zake uliowataja.

Inaanzaje kuishambulia Hamas, Iran na Hezbollah bila kuchokozwa? Iran ni Taifa kubwa lenye nguvu sana. Usilixhukulie poa.
 
Nilichojifunza hao wenzetu hawana kulea viongozi wazembe wasiowajibika. Huku kwetu mamia ya watu wanatekwa na kuuliwa lkn wakuu wa vyombo vya usalama wanakula Bata tu
 
Hawa wanawajibishwa kwa kushindwa kuwazuia hamas kutekeleza utekaji na uuwaji hiyo siku, sioni kugeukana bali huku ni kuwajibishana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…