Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,359
- 6,568
Mungu aliumba Majini na Wanadamu kwa lengo la kuwa wamwabudu yeye tu. Vilevile hakutaka kutufanya kuwa ni maroboti bali akatupa na utashi wa kujua mema na mabaya, kumuamini ama kutokumuamini.Kabla hajatuchoma moto sisi inatakiwa ajichome yeye kwanza kwa kosa lake mwenyewe la kumuumba shetani wakati yeye anajua yote - Hata anapomuumba shetani alikua anajua Shetani ataasi.
Na kama huyo Muumba ana uwezo wote, basi alitengeneza kila kitu kwa makusudi, ikiwemo uwezo wa kuuliza maswali na kutafuta ukweli kama ninavyokuuliza.
Kwa maekezo yako si sawa na kusema hata hii akili ya kuuliza kanipa yeye au?
Kwanza huyo Mungu unayemtetea Chanzo chake ni nini? Alitokea wapi?
Ukichagua kutokumuamini na kukufuru basi jua huna wa kumlaumu isipokuwa nafsi yako mwenyewe. Kwasababu Mungu alishakupa njia zote za kumjua na kumuamini ila ukachagua kinyume chake.