makutupora
JF-Expert Member
- Jul 7, 2015
- 2,482
- 5,138
- Thread starter
-
- #61
Niko maombi Toka JanaUsiache kuomba pia Dua ni muhimu ikimpendeza Mungu Kuna sehemu ntaku connect..Kuna mambo yanakamilishwa najua hauta ni let down maana nimewai kupitia hizo hatua zako for sure siku moja zitabakia story.
Nimewai ku connect watu wakafanya ubadhilifu wa mamilioni ya shilingi nikapata hekaheka nikaacha kusaidia watu.
Naweka Imani Kwako kwa kuweka Imani ya maneno yako so tutachekiana.
Asante sana brother ... Asanteee kwa kunitia moyoMkuu makutupora kaza moyo ndugu yangu usikate tamaa.
Naamini utavuka changamoto hizo maana hakuna changamoto ya kudumu tunapokaza moyo na kufanya jitihada.
Monetary doctor Nomadix Harmful
Kaza ndugu yangu.Asante sana brother ... Asanteee kwa kunitia moyo
Nashukuru sana mkuu
AiseeBora kufa ili usiendelee kuteseka , huyo mzazi muache ajipambanie maana alikuzaa kwa tamaa zake ...Anakupa mzigo sana hata yeye atakufa , anapoteza muda tu ili akupe tabu za kumuuguza.
Asante mkuuTofauti na hapo kajiunge biashara za network marketing Kama eternal international.
(Ukienda waambie huna ela ya kiingilio) Maana Kuna kiingilio
Waambie wakupe mbinu ya kupata wateja kwa njian ya simu ama vipeperushi.
Ukienda hapo huwezi kosa ela ukiwa na bidii
Nyingine angalia hapa chini
👇👇
Pitia hio screen shot muhimu sanaAsante mkuu
Sana mi nikiona wanaume na wasomi Hali ni hii wanawake inakuwaje? Mmmhhhh Mimi nitalea watoto wangu wakike mpaka nife Mimi au wao au waruke ukuta, yote kwa yote njia zitafunguka Allah akufanyie wepesiNikiona mwanaume kafikia hatua hii huwa napata uchungu sana kwani najua wanaume wengi ni wapambanaji.
Nakuombea kwa Mungu ufanikiwe na upate unachohitaji.
Tuko pamoja na wewe.
Asante mkuu nimeipitia nimeelewa naomba niufanyie kazi ushauri wakoPitia hio screen shot muhimu sana
mafanikio yapo kwa wapambanaji wa kweliMkuu makutupora kaza moyo ndugu yangu usikate tamaa.
Naamini utavuka changamoto hizo maana hakuna changamoto ya kudumu tunapokaza moyo na kufanya jitihada.
Monetary doctor Nomadix Harmful
Amina sana sanaSana mi nikiona wanaume na wasomi Hali ni hii wanawake inakuwaje? Mmmhhhh Mimi nitalea watoto wangu wakike mpaka nife Mimi au wao au waruke ukuta, yote kwa yote njia zitafunguka Allah akufanyie wepesi
Wanawake ni rahisi sana kuajiriwa au "kujiajiri"Sana mi nikiona wanaume na wasomi Hali ni hii wanawake inakuwaje? Mmmhhhh Mimi nitalea watoto wangu wakike mpaka nife Mimi au wao au waruke ukuta, yote kwa yote njia zitafunguka Allah akufanyie wepesi
Amina mkuuuMungu akufanyie wepesi!
Mkuu Asante sana .... Umenitia sana moyo! Umenipa na nguvu.Rika langu usikate tamaa , kuna muda nilipitia nyakati ngumu ambazo kiukweli zilinivunja moyo ,nikienda kwenye interview hatua zote za awali nafaulu ila linapofika swala la Oral interview majibu yanakuja nimefeli , daah nilichoka akili ,nikamwambia MUNGU wangu sehemu nilipofanya interview imetosha sitaenda kuomba kazi tena labda niitwe kwa mapenzi yao.
Nilimwambia Mungu ,naenda kuwekeza nguvu yangu shambani , sina mtaji waaina yoyote ile , lakini kwa nguvu zangu nitapambana , nakumbuka ilikuwa mwezi wa 7 mwaka 2023 , nilifika nyumbani nikiwa namaumivu yakukoswa kazi , nilikutana na fursa yakufyatua tofali , sikujua hata wanafyatuaje , kwa kuangalia niliona nikazi ngumu sana , basi kuna sehemu nilikuwa nimepiga kazi nikalipwa kama laki moja na tisini , nikachukua laki moja nikaweka kwenye kufyatua tofali ili hizo tofali nikichoma niziuze nipate mtaji wa kilimo .
Basi nikapambana nikafyatua tofali elfu 3500 , nikazipanga mimi na mdogo wangu , tukakata kuni zakuchomea , tukachoma , tofali zilivyoiva nikapata na mteja nikauza nikapata mtaji wakuanzia kilimo , nikaanda ekari moja kwa ajili ya mahindi ,
Hiyo ekari niliyoiandaa niliamini nitasaidiwa na wafanyakazi kwa sababu ni shamba la mbali , nyumbani napo nikaanda nusu ekari kwa ajili ya pamba na robo nyingine nikaweka mahindi ya matumizi ya nyumbani kama kuchoma na kupika. Mashamba yote ya nyumbani niliyahudumia kwa nguvu zangu ,nilishinda shambani kama mwehu yaani jua linazama lakini natamani niendelee ,kukikucha vile vile nilikuwa naamkia shambani.
Nilifanya hivyo haswa pamba lilinitesa sana hiyo nusu ekari lakini nilipata pesa nzuri sana ilikuwa laki 3 na elfu 16 .
Mahindi nilipata gunia 9 pekee lakini nilimshukuru MUNGU ,moyoni nikisema sitaenda kuomba kazi tena labda niitwe au nafasi zitoke za serikalini.
Basi wakati nimemaliza kuvuna siku moja majira ya jioni nilipigiwa simu nikajuzwa nahitajika kufika ofisi fulani kuanzia kesho na kama nipo tayari wanitumie nauli.
Nami nikawaambia nipo tayari, wakanitumia nauli na kesho yake nikaanza safari,nilifika mambo hayakuwa mengi .
Nilifanyiwa process na Mwajiri nikaingizwa kwenye mfumo , Nikapewa code of conduct , Mkataba, na kazi ikaanza rasmi na sasa namshukuru Mungu kwa hapa nilipo, kilimo naendeleza na kazi naendelea nayo .
Mshahara si mkubwa lkn baada ya makato yote Payroll, Nssf,Nhif sikoswi shilingi laki 450k.
Ushauri wangu ukiona kazi zakuajiriwa zimekuwa ngumu na kila ukiomba msaada huuoni basi amua kupambana wewe kama wewe ,nahapo milango ya Neema itafunguliwa. Usikubali kushindwa kisa umekataliwa au kila sehemu unayoomba kazi haupati , tafuta fursa kulingana na eneo ulilopo , vzr vitajileta ukiwa tayari unajipambania .
Nimekuelewa vizuri sana mkuu
Hakika.
Kuna muda unahisi dunia imekukataa hivyo usikubali hali hiyo .Mkuu Asante sana .... Umenitia sana moyo! Umenipa na nguvu.
Asante mkuu! Nimekuelewa