Shida haina hodi, mwenzenu nimefika mwisho, naombeni msaada

Shida haina hodi, mwenzenu nimefika mwisho, naombeni msaada

Pole sana mkuu, kwa hali unayoipitia, najua kwa hali unayoipitia sasa msaada pekee unaouhitaji ni shughuli/kazi ama pesa/mtaji lakini acha niandike haya machache kama faraja yangu kwako na hata kwa wengine.

Kuna kipindi nilipoteza kazi nikayumba vibaya mno, nilikonda hadi nikikutana na watu ambao tulionana muda mrefu ikawa wananishangaa. nikiwa katika harakati za kuweza kupata kitu cha kufanya ili mkono uende kinywani, nikapata wazo la kufanya biashara ya kuuza bidhaa ndogo ndogo (dawa za meno, subuni, mafuta nk) ndani ya stendi ya magari.

Changamoto ikawa ni mtaji, nilihitaji angalau shilling elfu thelathini hadi hamsini tu kwa ajili ya kuanzia.

Baada ya kuwaza sana nitafanya nini ili kupata mtaji nikapata wazo nikamshawishi mama mkubwa anipe debe la karanga kwa mali kauli/mkopo.

Nikamshauri bimkubwa nae akanipatia.

Ilikuwa vigumu sana kuingia mtaani kuuza karanga lakini nikiwa katika hali ngumu sikutaka kuipa akili yangu muda wa kuchakata kwamba nani ataniona vipi.

NITAIFUPISHA KIDOGO KUOKOA MUDA MTU AKIWA NA SWALI ATANIULIZA.

Nikazikaanga karanga za maganda na kuingia mtaani, nikawa nauza faida nakula kidogo nyingine naweka, baada ya siku chache nikapata wazo la kwenda kuziuza katika fukwe za bahari muda ambao wavuvi wanarudi baharini, hapo ndipo nilipoanza kujipata, nilikuwa nauza ndoo kubwa mbili kwa siku nakunja elfu 15, debe la karanga lilikuwa ni elfu 10, kipimo changu nilikadiria faida ya elfu 7500-8000 kwa kila debe moja

Yale mawazo ya biashara za stendi yakafa yenyewe. Nikanunua na baiskeli kwa ajili ya kusombea kuni na kuuzia karanga mtaani siku ambazo wavuvi hawaendi bichi.

Nikajisahau kwamba karanga ni za msimu tu zilivoanza kuwa adimu nikayumba kidogo lakini nilikuwa na pakuanzia hivyo sikurudi kwenye sufuri tena.

Lengo la kuandika hii ni nini?
ni kuiunga mkono ile kauli inayosemwa sana na motivation speaker kwamba ANZA NA ULICHONACHO.
Najuwa hata hii jamiiforums ni miongoni mwa vitu ambavyo unavyo kwa sasa ila pia angalia na vitu/watu hapo mtaani ambao/ambavyo vinaweza kukufanya upate shughuli yoyote ile ya kuifanya.

Mungu akufanyie wepesi kwenye hili kaka.

min -me Intelligent businessman Eli Cohen
 
Ilala boss ... Airport hapa
Kaka tafuta popote wanapochinja kuku,kuna pale shekilango tu, ukifika kuna sheli iko pale barabarani, omba uchinja kuku, sheeh unalipwa kulingana na kuku ulizochinja mkuu, 🙏

2.Nenda tafuta mgahawa wowote kazi yako iwe kuosha vyombo mkuu, kula Utakula pale pale(uwe mwaminifu Usione aibu)

3.Nenda ofisi Za azam ice cream, uombe baiskeli mzee, uwe unatembeza unaendesha, waombe deli mkuu /kibegi cha bolicon uwe unazungusha juice Za ukwaju, especially mitaa ya Chuo Chuo unyama ni mwingi, kuna beach, stand hapo uhakika kuuza

This is all I can advice you mkuu
 
Huu ni ukweli ndugu yangu sina kichaa ila nasema hivi , kama nakosea basi naona nipate adhabu ..Huu mfumo wa kuzaana ni utapeli ambao wengi hawajaujua ...Nakumbuka rafiki yangu , alizaliwa familia ya kimaskini huyo mama yao mzazi aliwazaa watano ; kila mtu na baba yake . Nakumbuka jamaa yangu alipofeli darasa la saba miaka hiyo , mother wake alishindwa kumpeleka hata kurudia . Yule mother kazaa watoto wote kwa wanaume tofauti bila ya ndoa na wala hajali .

Amezeeka licha ya kuwaingiza kwenye umaskini bado anataka kuhudumiwa mpaka leo , jamaa wamemuacha na wanawe wawili wamekufa tena wakubwa wa kwanza ; anaulumu tu watoto wakati hata mazingira hakuwajengea , maisha yake na wanawe wamerithi hayo hayo mpaka leo .
 
Nina mazingira magumu sana mbele naona giza tu mpaka sioni thamani ya haya maisha.
Miaka miwili natafuta kazi, naishi kwa ndugu kwenye mazingira magumu, mama yangu ni mgonjwa na namuangalia anavyoteseka kila siku nikiwa sina namna ya kumsaidia.

Yoyote ambaye ana ofisi, biashara, taasisi au shughuli yoyote, SICHAGUI, naomba kazi au hata nafasi ya kujitolea kwa malipo au bila malipo (hata nauli tu inatosha - ili niweze kutoka nyumbani na kushughulisha kichwa).

Mimi ni graduate mwenye shahada, niko tayari kufanya kazi yoyote, tafadhali naamanisha yoyote ile. Mimi ni mchapakazi, naweza kusocialize na watu, napenda kuandika, kusoma vitabu na kufanya shughuli za kijamii.


WASIFU WANGU KWA UFUPI:


Umri - Miaka 30
Jinsia - Mwanaume
Taaluma - Bachelor of Social Work
Makazi - Dar es Salaam



Tunaambiwa wanaume inabidi tujikaze, tuwe strong ila mimi nimefikia mwisho kabisa wa uwezo wangu. NAOMBENI MSAADA WAKUU!
Mbaya zaidi utakuta wewe ni ccm dam dam vp mama anaupiga mwingi eeh!Weka namba yako apa usije ukafa njaa!!!
 
Huu ni ukweli ndugu yangu sina kichaa ila nasema hivi , kama nakosea basi naona nipate adhabu ..Huu mfumo wa kuzaana ni utapeli ambao wengi hawajaujua ...Nakumbuka rafiki yangu , alizaliwa familia ya kimaskini huyo mama yao mzazi aliwazaa watano ; kila mtu na baba yake . Nakumbuka jamaa yangu alipofeli darasa la saba miaka hiyo , mother wake alishindwa kumpeleka hata kurudia . Yule mother kazaa watoto wote kwa wanaume tofauti bila ya ndoa na wala hajali .

Amezeeka licha ya kuwaingiza kwenye umaskini bado anataka kuhudumiwa mpaka leo , jamaa wamemuacha na wanawe wawili wamekufa tena wakubwa wa kwanza ; anaulumu tu watoto wakati hata mazingira hakuwajengea , maisha yake na wanawe wamerithi hayo hayo mpaka leo .
Na sisi ambao wazazi wetu wamewajibika ipasavyo hadi tumekuwa wakubwa unatuambiaje kuhusu kuwalea wazazi wetu?
 
Back
Top Bottom