Shida haina hodi, mwenzenu nimefika mwisho, naombeni msaada

Asante sana Mkuu kwa ushauri wako, chochote kilicho halali Mimi ntafanya
Unasema huchagui kazi lakini mimi nikitazama kwa jicho la uchunguzi naona unachagua kazi ndiyo maana unasema hata ukipata kazi ya kujitolea kwa kulipiwa nauli tu! Kazi ya saidia fundi unaweza? Hii kazi kwa siku hukosi 7500! Na chakula cha Dar kwa mama lishe unapata hadi chakula cha 1500, inayobaki unapeleka home kwa bi mkubwa hata kama itabaki 4000. Au hiyo inayobaki unaweza kuwa unaweka kwa miezi miwili utapata hata ya kutembezea vitu mtaani. Naona kuna watu wanauza mtaani hadi njegere, samaki wabichi n.k.
 
What if kama hauna uwezo kama ndugu yetu hapa mleta mada
Kama sina uwezo atasaidiwa na ndugu wengine. Binafsi namshukuru sana Mungu mama yangu ameshastaafu..hana pesa kama zamani lakini anao uwezo wa kula, bima ya afya na mambo yake mabogo madogo anayaweza. Pia huwa tunamsaidia kila mwezi lazima apate kitu kidogo kutoka kwa watoto wake.

Huwezi kuishi comfortable ukiona mzazi wako anateseka hasa kama ni ugonjwa inaumiza sana so namuelewa mtoa mada.
 
Huruma ni ngumu sana kama wote wangekuwa na huruma , sio kwa wazazi tu hata hawa ombaomba , majirani zetu wengine hata pesa ya kula hawana ..Kiufupi , siwezi kuangalia watu wanateseka bora ya kufa , wenye uwezo wanataka kuwa juu zaidi hakuna mtu anajali mwingine .Dunia yote binadamu ni wabinafsi .
 
Sawa Boss
 
Kaka pole sana mtaani kwako umekosa hat bod boda jnaweza ukaanza kwa udeiwaka hasa kam unaweza kusosholaizi na wenzio mkuu usikate tamaa mi ni boda ktengo cha bajaji na nimesoma pharmacy kazi ni kipimo cha utu
Naangalia huyu jamaa namna ya kumsaidia ila changamoto ni umri, 30 yrs kufanya kazi yoyote ni ngumu. Huwezi kumlaza na shamba boy wa 17 yrs.
 
Wenye mama mshukuruni sana! Yani mama yupo hadi mnakuwa watu wazima!? Naifeel furaha yenu!
 
Unakata tamaa.mapemaa.sana dogolas,30 bado nguvu ya kukomaa imo!ume hitimu mwaka gani chuo?sio dharau weka vyeti pembeni,vua aibu ya usomi,ingia kitaa,najama zangu wana masters ila kitaa wanauza maji dumu miatano,kwa siku wanalaza 30 elfu,toa kula na wanafamilia,mi mwenyewe na kielimu sio haba,ila.niliingia mtaani nikaaza kuperembaaa na kuwa machinga,ninawashikaji wasomi ila wanazama.kusaka kwenye minadaa vijiji....jitoe ufahamu
 
Boss nashukuru

Nakufata PM tuongee kwa urefu
 
Boss asantee nitafanyia kazi hili ntakupa mrejeshoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…